barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,726
- 32,818
Uchambuzi wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni Mstaafu Bernard Kamilius Membe juu ya mwenendo wa CCM chini ya Mwenyekiti Rais Magufuli na Katibu wa Itikadi na Uenezi H.Polepole.
1. VYAMA BORA.
Sanctity(usafi, utakatifu) Ideology (Itikadi, dira) na Organization( Mfumo.) Cold War iliigawa Dunia kwenye Makundi Mawili. East and West, yaani Wakomunist/ Wajamaa(East) vis a vis Capitalism.(West)(1) Vyama vya nchi za kibepari ni tofauti kabisa na vyama vya Kikomunist/ Kijamaa. Vyama vya kibepari vipo pale kwa ajili ya kuandaa kampeni na fedha kwa ajili ya kushinda uchaguzi ujao.
Mwenyekiti wa Chama hawi Rais. Ni Mtu anachaguliwa na mkutano Mkuu (Congress). Kazi zake ni tatu. 1. Kuandaa mkutano ujao wa Uchaguzi. 2. Kukusanya fedha za uchaguzi.3. Kuendesha mikutano ya Primaries(ya mchujo ).
Wanachama ni mashabiki wowote wa kadi tu wa mrengo huo. Mashabiki ndiyo wanatoa fedha za kumsaidia Mbunge ashinde uchaguzi. Mbunge hatoi fedha ili kupata Ubunge.Ndiyo maana husikii sana maneno ya rushwa.Kwa kifupi vyama vya kibepari havina mifumo kama ya vyama vyetu vya mrengo wa Kikomunist/ Kijamaa. Ni kwenye Mabunge yao tu ndiko vyama vyao huo na mfumo wa Party Caucus na vinajitokeza kupambana na wenzao. Na hata huko Bungeni, Mbunge anaweza ku- cross the party line yaani akaunga hoja ya upande mwingine na bado akabaki kwenye Chama chake.
Wabunge hao huitwa "rebels."(waasi)Hawafukuzani. Vyama cha kibepari havina mfumo unaolingana na Serikali wala kuwa na structure za Politburo, Central Committee au NEC. Wana mikutano ya Congress tu. Vyama cha havishiki hatamu za Uongozi. Rais akichaguliwa wanachama hawana lao tena. Wanawaachia wanachama wao Bungeni. Kwenye ngazi za Mikoa hivyo hivyo.Vyama havishiki hatamu. Hii ni part one.
Part two ndiyo inayotuhusu sisi. Hapa nitachambua sanctity, ideology na organisation na ubora wa vyama vyetu.
2. Vyama Vyetu. Ubora wa vyama vyetu vyenye uasilia wa Ukomunisti/ Ujamaa unategemea ushindi wake kwenye vigezo vitano vifuatavyo:
1. Clarity kwenye Itikadi yake. 2. Historia yake iliyotukuka. 3. Mfumo wake. 4. Wanachama wake. 5. Alama/ nembo za utambulisho wake. 1.Je Chama na Serikali yetu inafuata Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea? Ni kitendawili. Azimio la Arusha lipo? Wenzetu Wachina, Wacuba, Warusi, Wa Algeria, Waangola, wapo very clear! Ni Wajamaa kwa maneno na vitendo na Dunia inawatambua hivyo. Sisi tumeandika siasa yetu ni ya Ujamaa lakini tuna practise Free Market Economics ( soko huria)na Azimio la Arusha ni historia. Tunawashindaje hao vingunge kwa hili. 2. HISTORIA. Hapa ndipo penye nguvu ya CCM. Chama chetu kina historia ya Ukombozi kwa nchi yetu na nchi zinazotuzunguka. Heshima yetu ipo kwenye historia. Yaani Uzamani wetu. Huwezi kufuta Uzamani huo ukaleta Upya. Kufanya hivyo ni kujiua.Hapo tumewapiku wengi isipokuwa Cuba. 3.MFUMO. Wenzetu wana Politburo, Central Committee, NEC na Congress.Na wengi wa wanachama wana kofia mbili mbili.
Wajumbe wa Kamati juu kwa mfano, kuna mawaziri, Mabalozi na makatibu wakuu. Balozi Lukoki wa Angola nchini Tanzania kwa mfano, ni mjumbe wa Kamati juu ya MPLA. Wanafanya hivyo ili kuziongoza na kuzishauri Serikali zao ndani kwa ndani. Hawasubiri vikao. Sisi tunauondoa utaratibu huo. Nafasi yetu ya pili inatokana na nini? Mfumo wetu wa kutenganisha kofia? Aidha wenzetu wana utaratibu wa kusimamisha wagombea bila ya kuwashindanisha na wenzao wa Chama hicho hicho kwa baadhi ya majimbo wanayoamini wabunge wao wanafanya vizuri. Ni yale tu ambayo yana Wabunge lege lege ndiyo wanashindanisha wagombea kutoka Chama kimoja. Faida ya utaratibu huo ni kuleta Umoja ktk Chama, kutambua Wabunge wanaofanya vizuri na utaratibu huo unapunguza tuhuma au vitendo vya rushwa. Sisi hatufanyi hivyo. Tunapambanisha wagombea wetu ktk kila jimbo, vitendo vya rushwa vinakithiri,na wengine wanafitinishwa hata kama hawatoi rushwa n.k. Je hiki ni kigezo kinachotupa sifa Duniani? Wenzetu hawakubaliani nasi kwa hili.
4. WANACHAMA.
Sisi Chama chetu ni Mass party. Yaani "kumbakumba", ni Chama cha wengi na ili uwe mwanachama, wala jina lako haliendi Central Committee kuchunguzwa na kisha kupewa kadi ya Uanachama. Sisi ni matakwa yako. Hata mtu wa chama cha Upinzani kwa kutumwa au kujituma anaweza kujiunga na Chama chetu siku yoyote tena kwa sherehe na nderemo.Wenzetu kamwe hawafanyi hivyo. Utakuwa vetted ( kuchunguzwa kwa kina) kabla ya ombi lako la kutaka kujiunga na Chama kukubaliwa. Je hii ndiyo sifa inayotupa nafasi ya Ubora Duniani? Wenzetu hawakubali.
5. MAVAZI/ NEMBO. Kila Chama hujitambulisha kwa Mavazi na Nembo. Vitu hivi ni muhimu lakini hatushindanishwi navyo. La muhimu hapa ni kujua kuwa upya wa Chama hauwi kwenye mavazi, wala nembo wala watu wapya. Upya wa Chama chochote Duniani upo kwenye Historia yake, Itikadi yake na mfumo wake. Kama vitu hivyo vitatu ni constant ( yaani havibadiliki) badala yake tunabadilisha nembo, mavazi na watu, Chama chetu kitakuwa bado ni kile kile. Hakiwi kipya. Uzamani wa Chama ni kama mvinyo. Mvinyo wa zamani ni mtamu sana na una bei kubwa kuliko mpya. Nirudi kwenye hoja na nimalizie. Chama chetu lazima kiwe clear na Historia yake, Itikadi yake na Mfumo wake.
Historia yetu ipo clear lakini lazima tuiishi! Tukasema nini kuhusu Palestine, na Western Sahara kwa mfano. Vinginevyo tutakuwaje wa pili kwa Ubora? Tumejiondoa kwenye Open Government Forum ya Umoja wa Mataifa. Yaani hatutaki tufuatwe fuatwe kuhusu Good Governance na haki za binadamu. Tutasifiwaje? Pili Itikadi yetu haijawa clear. Tupo kama popo! Hatueleweki kama sisi ni ndege au Wanyama! Siasa ya Ujamaa kwenye vitabu na Soko huria kwenye maisha ya kila siku.Wapi na Wapi? Tukitangaza kuwa sisi tunafuata Siasa ya Ujamaa na tunarudisha Azimio la Arusha, Investors wote watakimbia kama bado hawajaanza. Ni itikadi gani tunayosifiwa nayo? Wenzetu China, Urusi, N.Korea, Cuba, Algeria,Ethiopia na Angola wana resources ambazo zipo tapped tayari na wanajitegemea. Ndiyo maana wametamka na kuyaishi matamko yao ya kufuata itikadi ya kikomunisti. Sisi hatujawa clear! Hatuwezi kuwashinda.
Mfumo wetu lazima uendane na maamuzi ya pamoja. Ni kikao gani kimeamua nini, lini, na kwa nini. Hakuna uamuzi wa mtu mmoja wala usio na kikao cha kikatiba. Kule Nje kwa hao wenzetu, kama Party Secretary General Hayupo kwa sababu yoyote ile, Central Committee haifanyiki siku hiyo.
The Party Secretary General is indispensable. Baada ya yote hayo, najiuliza ni kipi kinachofanya CCM iwe na Ubora wa pili baada ya China? Chama chetu lazima kipeleke vijana viongozi kama ndugu yetu Polepole Urusi, Cuba, N.Korea, Algeria, Angola, na Ethiopia ili kujifunza zaidi kwa faida ya Chama chetu na Taifa kwa ujumla.
Kidumu Chama cha Mapinduzi.