Bernard Membe. Nyota inayong'aa sana sasa hivi. "Kachero Mbobezi

Membe si ndo huyu huyu aliyekamatwa yule muhindi kule dodoma na mahela kibao ya kuwahonga wajumbe ili wampitishe ??

Nitakuwa wamwisho kumkubali Kama nilivyokuwa wa mwisho kumukubali lowasa
1.5 trilioni
 
Nikweli mkuu ila kwa mtazamo wangu,kwa namna muundo ulivyo ndani hasa ya chama tawala na upinzani kutokuwa na taasisi imara huku ukikandamizwa zaidi,unadhani JPM yeye hajachora namna ya kutoboa 2020? Usije ukashangaa tume ya uchaguzi ikampitisha JPM, Hashimu Rungwe nawengi wakaambiwa form zao zilikosa vigezo.

My concern nikwamba kwanamna CCM ilivyo,upatikanaji wa mwenyekiti wa tume na makamishna kwa siku za karibuni itakuwa ngumu sana unless wajumbe ambao ni wapiga kura watakapokua na akili timamu lasivyo ni ngumu maana president ananguvu nyingi kupitiliza na Membe anaweza kuwa na ushawishi ila akakosa nguvu ya dola
Atakayepitishwa na ccm atakuwa na nguvu ya Soka.
 
Uchaguzi wa 2020 ndiyo utakuwa uchaguzi mgumu kwa CCM kuwahi kutokea ndani ya CCM. Ninavyojua ndani ya katiba ya CCM hakuna kifungu chochote Kimachosema ni lazima Mtu Atawale kwa vipindi viwili. Huu ni utamaduni tu. Na nikimulika kwa Mbali zaidi Naiona hii timu ya Membe jinsi itakavyotingisha.hata huyu Rostam atakuwa upande wa Membe.
Njia Membe naona kama nyeupe ndani ya chama kwani sio Rostam hata akina Bashiri na Polepole kuenda na upepo wa Uchumi na maisha ya Raia yakivyo huko Mitaani na upepo unavyovuma.
Na kumbuka Membe ana hoja mbili tu zenye mashiko ambazo mpaka sasa hivi chama changu ccm hajatoa majibu CAG na IMF haya yote kundi la Membe litasimamia na haya yatakosa majibu kwa hiyo ili kunusuru Chama inabudi maamuzi magumu yafanyike kama ANC
 
Eeeh bank ya maendeleo ya Africa imetoa ripoti uchumi unakua kwa asilimia saba.....

Malaika mkuu amefurahi sana we ni nani mpaka useme uchumi upo hoi bin taaban
Mku kumbuka Bashiri na Polepole wanajua ndo maana hawaongei kwani huko Mtaani wanaoyaishi hayo maisha wanayajua ni kipi pumba na mchele.
Kazi na Bata
 
Niko tayari Kura yangu ipotelee kwa Lissu.. hawa ccm hadi naenda kaburini wapite kwa kura zenu tu.
 
Maccm yote matapeli, watz tunahadaiwa, tatizo ni ccm ila Magufuli ni tatizo zaidi
Hakuna anayeweza kupinga kwa hoja kwamba kwa sasa ndani ya CCM Tishio namba moja kwa JPM ni Kachero Mbobezi Bernard Kamiliusi Membe.. Huyu mtu Sifa zake Zinakaribia kufanana Sana na za Kikwete.Anaonekana ni mtu mwenye busara na Huruma. Na muonekano wake, anaonekana ni mtu mtulivu sana. Smat. Hana pupa. Ni understand. Muelewa sana. Pia anaonekana ni mtu mwenye damu ya kupendwa Kama ilivyo kwa Jakaya Kikwete.na anaonekana ni mpole na mnyenyekevu sana,

Jana nimeona clip ktk mitandao. Ni Msiba alikuwa anajaribu kumchafua Bernard Membe. Lakini nilichogundua, tuhuma alizotoa Juu ya Membe ni nyepesi sana, yaani Kama tuhuma hizo tu ndio Msiba anategemea amtishe nazo Membe basi namshauri ajipange upya kwa sababu kishindo cha huyu Kachero Mbobezi huko mbele kitakuwa siyo kidogo Kama ambavyo Msiba anafikiri.

Nimkumbushe tu Msiba kuwa hata JPM wakati wa kampeni kulikuwa kunatolewa tuhuma nyingi juu yake Kama vile Kugawa nyumba za Serikali kwa marafiki zake, kuleta kivuko kibovu na kuliingizia Taifa hasara ya mabillioni nk.lakini wananchi waliona tuhuma hizo hazina uzito sana na matokeo wakaamua kumchagua kutokana na record yake alipokuwa wizara ya Ujenzi. Bahati mbaya sana kwa Msiba ni kwamba hizi Tuhuma amekosea na kuzitoa mapema sana, kiasi kwamba mpaka kipindi cha uchaguzi kifike zitakuwa zime expire .

Zaidi kinachomfanya Bernard Membe, Kachero Mbobezi kung'aa sana kwa sasa ni kutokana na utendaji kazi wa JPM ambao Wananchi wengi wanaona haufai. Na hii inatokana na kuporomoka kwa hali za uchumi za wananchi wengi na kusababisha maisha Yao kuwa magumu sana tofauti na miaka minne iliyopita.

JPM anaonekana kutawala Nchi kwa nguvu kubwa sana, jambo linalopelekea wateule wake kufanya kazi kwa woga na bila ubunifu. Kwa sababu mtu Muoga hawezi kuwa Mbunifu.Mtu Muoga hupenda Sifa.

Kwa hali ya Kisiasa ilivyo sasa Hata wapinzani wataona ni bora kumpa sapoti Membe pengine labda kunaweza kuwapa ahueni hali itakawafanya waweze kufanya siasa bila kubughudhiwa Kama ilivyokuwa wakati wa Kikwete. Ndani ya CCM hali ni hivyo hivyo. Wengi wanaugulia maumivu. Watu wamechoka.

Kwa ndugu Membe, kuna hii kauli yake aliyoitoa majuzi. "KAZI NA BATA" hii kauli inaamsha hisia za watu wengi sana,Ndani ya CCM na hata Upinzani. Ni kauli inayowapa watu matumaini mapya baada ya kukata tamaa, Wananchi hawako tayari kuendelea kuvumilia hali hii ngumu ya maisha kwa miaka mingine mitano.
 
Mkuu una machungu kama vile nnakuona yan unavyosononeka
Jpm hapana aisee ccm watuelewe wamuondoe dikteta tuunge upya umoja wa taifa tuko radhi kutumia rasilimali zetu kuiunga mkono ccm iwapo itampitisha membe lakini pia kuihujumu kama watatuletea haya matatizo tena kwa miaka mitano mingine
 
Mh, Watanzania wa Leo siyo wajinga. Ukiona mtu yoyote anashambuliwa na Musiba basi jua siyo. Musiba, ila Musiba ametumwa. Kumdhoofisha. Je hujui kuna kesi ya Kachero Mbobezi Membe dhidi ya Musiba Mahakamani?. Na ukiona mtu Mtu yeyote anashambuliwa na Musiba basi jua Mtu huyo ni Tishio kwa JPM , Kumbuka Abrahamu Kinana alivyotoaga tu ile speech ya. "Kiongozi mzuri ni Yule anayewasikiliza anaowaongoza" Je unakumbuka kilichompata Kinana toka kwa Musiba?. Sasa kwa nini hukujiuliza. Kinana alizungumzia Juu ya viongozi wa wananchi, Musiba alimjibu na kwa matusi. Je? Musiba ndiye kiongozi wa Wananchi aliyezungumziwa na Mzee Kinana???!
Mkuu uko gizani bado!! hao wote ni CCM, think twice
 
Kuna hoja watu huwa wanaitoa kuwa upinzani haupo tayari kukabidhiwa nchi ila kwa hali tuliyonayo leo hii, ni bora nimpigie kura yangu Lissu.

Kuna umuhimu mkubwa sana wa kubadilisha chama tawala hata kwa miaka mitano tuu.Kuna watu wamebweteka sana.
 
Back
Top Bottom