Bernard Membe. Nyota inayong'aa sana sasa hivi. "Kachero Mbobezi

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,439
Hakuna anayeweza kupinga kwa hoja kwamba kwa sasa ndani ya CCM Tishio namba moja kwa JPM ni Kachero Mbobezi Bernard Kamiliusi Membe.. Huyu mtu Sifa zake Zinakaribia kufanana Sana na za Kikwete.Anaonekana ni mtu mwenye busara na Huruma. Na muonekano wake, anaonekana ni mtu mtulivu sana. Smat. Hana pupa. Ni understand. Muelewa sana. Pia anaonekana ni mtu mwenye damu ya kupendwa Kama ilivyo kwa Jakaya Kikwete.na anaonekana ni mpole na mnyenyekevu sana,

Jana nimeona clip ktk mitandao. Ni Msiba alikuwa anajaribu kumchafua Bernard Membe. Lakini nilichogundua, tuhuma alizotoa Juu ya Membe ni nyepesi sana, yaani Kama tuhuma hizo tu ndio Msiba anategemea amtishe nazo Membe basi namshauri ajipange upya kwa sababu kishindo cha huyu Kachero Mbobezi huko mbele kitakuwa siyo kidogo Kama ambavyo Msiba anafikiri.

Nimkumbushe tu Msiba kuwa hata JPM wakati wa kampeni kulikuwa kunatolewa tuhuma nyingi juu yake Kama vile Kugawa nyumba za Serikali kwa marafiki zake, kuleta kivuko kibovu na kuliingizia Taifa hasara ya mabillioni nk.lakini wananchi waliona tuhuma hizo hazina uzito sana na matokeo wakaamua kumchagua kutokana na record yake alipokuwa wizara ya Ujenzi. Bahati mbaya sana kwa Msiba ni kwamba hizi Tuhuma amekosea na kuzitoa mapema sana, kiasi kwamba mpaka kipindi cha uchaguzi kifike zitakuwa zime expire .

Zaidi kinachomfanya Bernard Membe, Kachero Mbobezi kung'aa sana kwa sasa ni kutokana na utendaji kazi wa JPM ambao Wananchi wengi wanaona haufai. Na hii inatokana na kuporomoka kwa hali za uchumi za wananchi wengi na kusababisha maisha Yao kuwa magumu sana tofauti na miaka minne iliyopita.

JPM anaonekana kutawala Nchi kwa nguvu kubwa sana, jambo linalopelekea wateule wake kufanya kazi kwa woga na bila ubunifu. Kwa sababu mtu Muoga hawezi kuwa Mbunifu.Mtu Muoga hupenda Sifa.

Kwa hali ya Kisiasa ilivyo sasa Hata wapinzani wataona ni bora kumpa sapoti Membe pengine labda kunaweza kuwapa ahueni hali itakawafanya waweze kufanya siasa bila kubughudhiwa Kama ilivyokuwa wakati wa Kikwete. Ndani ya CCM hali ni hivyo hivyo. Wengi wanaugulia maumivu. Watu wamechoka.

Kwa ndugu Membe, kuna hii kauli yake aliyoitoa majuzi. "KAZI NA BATA" hii kauli inaamsha hisia za watu wengi sana,Ndani ya CCM na hata Upinzani. Ni kauli inayowapa watu matumaini mapya baada ya kukata tamaa, Wananchi hawako tayari kuendelea kuvumilia hali hii ngumu ya maisha kwa miaka mingine mitano.
 
Watanzania ......tusisahau kilichotufikisha kwenye hii hali......tubadilike sasa ...la sivyo tutakua tukanimbiza mikia yetu wenyewe miaka yote iliyobakia .....
 
Uchaguzi wa 2020 ndiyo utakuwa uchaguzi mgumu kwa CCM kuwahi kutokea ndani ya CCM. Ninavyojua ndani ya katiba ya CCM hakuna kifungu chochote Kimachosema ni lazima Mtu Atawale kwa vipindi viwili. Huu ni utamaduni tu. Na nikimulika kwa Mbali zaidi Naiona hii timu ya Membe jinsi itakavyotingisha.hata huyu Rostam atakuwa upande wa Membe.
 
Membe ndiye mtu pekee atakayeweza kurudisha uchumi wetu katika hali ya kawaida.... Uchumi kwa sasa umekufa ho bin taaban..
Hilo kila mtu analijua mkuu, isipokuwa wale wachache wanaonufaika na uongozi huu, kwa sababu lazima ujue kuna watu wamekwapua 1.5 Trilion na mpaka sasa hakuna majibu yoyote zaidi ya sarakasi za kitoto, hawa ndiyo wanufaika wakubwa wa uongozi huu, sisi wengine woote tuko hoi bin taabani. Hatuuzi wala hatununui. So Sad
 
Bernard Membe anayo haki kikatiba kugombea Urais comes 2020 kupitia CCM! Katiba ya CCM inatoa nafasi ya Rais kuongoza kwa miaka 5, mambo mengine ni UTAMADUNI tu ambao si lazima kufuata!
Mambo ya kufuata UTAMADUNI fulani ni maamuzi ya Wana CCM na si kulazimishwa!
Mbona suala la KUKEKETA wanawake huko nyuma ulikuwa ni utamaduni safi kabisa! Mbona leo tunapinga UKEKETAJI?!
Hata UTAMADUNI wa Rais aliyeko madarakani kwenda mihula 2 unaweza kutazamwa Upya?
Kama Urais wako hauna tija kwa TAIFA na manufaa kwa Wananchi basi watu wavumilie tu!
Huo ni Uzwazwa uliopindukia!
 
Eeeh bank ya maendeleo ya Africa imetoa ripoti uchumi unakua kwa asilimia saba.....

Malaika mkuu amefurahi sana we ni nani mpaka useme uchumi upo hoi bin taaban
report ya IMF inasemaje?

reality huku nje ni tofauti kabisa. Hali ya uchumi ni mbaya sana sana. Nina kampuni ya ujenzi zaidi ya miaka 3 sijalipwa. Makampuni ya magharibi yoye yameondoka. Yamebaki ya kichina nao wako hoi...
 
report ya IMF inasemaje?

reality huku nje ni tofauti kabisa. Hali ya uchumi ni mbaya sana sana. Nina kampuni ya ujenzi zaidi ya miaka 3 sijalipwa. Makampuni ya magharibi yoye yameondoka. Yamebaki ya kichina nao wako hoi...
Weee Ile ya IMF malaika haikumfurahisha hataki wala kuisikia
 
Anyway kusema 2020 mkulu atatoka madarakani hata kama wapinzani wake watatumia mbinu gani sio rahisi kwa kweli. Tumuombe Mungu tuu tuvuke salama 2025 tupate kiongozi makini basi. Na si vinginevyo japo kama tutakuwa wakweli hali ni mbaya sana huku mitaani
 
Back
Top Bottom