Bernard Membe: Nina maadui 11, ikifika 2016 watakimbilia Kenya!

Kwa hiyo na hizo "Ze Komedy" za kuoteshwa unazimeza nzima nzima siyo?
Mkuu Kiranga, kauli ya kuoteshwa ni tamathali za semi tuu kuwa bado anatafakari na kusikilizia the "inner calling", which honestily its good!. Kabla mtu hajakimbilia kwenye urais, lazima asikilize "sauti" from within itakayomwambia "gombea ni wewe!", hivyo kuufanya urais kuwa ni wito na atakayechaguliwa awe kweli ni "chaguo la Mungu!".
 
ila mi nimeona kaongea pumba kupita maelezo alichokua anafanya pale ni kuonyesha kile kiatu (travolta)alichonunua Italia
 
Hii kitu angependekeza Lusine, Komba,Manyanya ama aina ya mtu kama Mwigulu nisingeshangaa,lakini Membe? Anaweza akatoa mfano hata mmoja nchi ambayo mkuu wa kambi ya upinzani anawekwa kitimoto bungeni?! Huyu hastahili kuwepo mambo ya nje!
 
Yawezekana Mh Membe akaiokoa CCM, kama hataenda upinzani, he is a great thinker. Nimependa sana mazungumzo ya kipindi hiki cha Dk 45, Mh Membe amenigusa sana, ingawa si kila kitu ninakubaliana nae, ila mwenye hekima hatapingana nami. Kuna mengi vyama vingine kujifunza kwa Mh Membe.
prof sina la kukwambia usiku huu,,,wanasiasa umewasahau????
 
Mkuu Kiranga, kauli ya kuoteshwa ni tamathali za semi tuu kuwa bado anatafakari na kusikilizia the "inner calling", which honestily its good!. Kabla mtu hajakimbilia kwenye urais, lazima asikilize "sauti" from within itakayomwambia "gombea ni wewe!", hivyo kuufanya urais kuwa ni wito na atakayechaguliwa awe kweli ni "chaguo la Mungu!".

hakuna kitu weweeeeeeee
 
Hapana. Kwa maneno yao utawajua. Membe anaamini kwamba yeye anaweza kuwa chaguo la mungu, akaoteshwa kama manabii walivyokuwa wanaoteshwa.

Katika nchi secular viongozi wenye fikra hizi ni wa hatari, kwa sababu hawaheshimu sana rule of law na the masses, wanaheshimu sauti "ya kuoteshwa" ambayo hatujui hata inapotoka.

Ndiyo haya haya ya kina Idi Amin, mtu anaamka anasema "nimeoteshwa wewe unataka kuniua" anakuchukua na kukuuilia mbali.

Kwa nini mtu mwenye umakini aongee vitu vague kama kuoteshwa katika kinyang'anyiro hiki ?

Wengine tukisikia mtu anaongelea sana kuoteshwa tunaanza ku suspect labda jamaa ni schizophrenic au ana matatizo fulani ya kisaikolojia.

Atuambie kitu cha kueleweka, hizo habari za kuoteshwa awaachie wahubiri na wachuuzi wengine wa maneno.

Of course anaweza kututhibitishia kwamba hata na yeye ni mchuuzi wa maneno asiye na la zaidi kwa kuendelea kukazania habari ya "kuoteshwa"
 
Hlo wazo la kuulizwa maswali ya papo kwa papo kama
Pinda ni wazo zuri.

Swali langu ni Je ataulizwa maswali
gani? Mbowe hana serikali ambayo ina ahadi
ambazo inabidi zitekelezwe.

Labda wamuulze maswali kuhusu
chadema . Na hapo tayari bunge
litakuwa jukwaa la kupgia kampeni za
vyama.

Nadhani Membe hakufkiria jambo hlo
wakati anaropoka ***** huo.
 
Nimemsikia for the first time he looks genuine and determinant kuwalipua!. Kwa vile alishagabatizwa kuwa yeye ni "Joka la mdimu", wakimaanisha he is only a "barking dogs, seldom bite", kwa jinsi nilivyomsikia akiongea kwa msisitizo, naamini this time itakuwa kweli, na ata prove beyond reasonable doubt kuwa yeye sio "joka la mdimu"!.

Sikufurahishwa alipowataja "Chadema wameenda kwake na njaaa zao, akawapa chakula"!.
Nimependa alipowataja wabaya wake 11 wakiwemo waandishi wa habari wawili na kuahidi muda muafaka ukiwadia, atawalipua kwa kuwataja hadharani!.

Pia nimeipenda ile ya sababu za yeye kuandamwa na hao wabaya wake, ni kwa sababu wao wana jicho la tatu la kuona 2015 itakuwaje, hivyo fitna zote ili ili kumzuia` na kitakachotokea 2015 na kutoa 'ole' kali kuwa "ole wao asioteshwe" kwani akioteshwa...(watakiona cha mtema kuni-emphasis mine!)

Pia nimeipenda confidence aliyoionyesha na sound ya "commanding voice" na "authority" kuthibitisha anaweza kuwa amiri jeshi mkuu!.

Kwa sisi tunaopenda mageuzi ya kweli ya nchi hii, nawashauri tuweke sala zetu kwa umoja wetu ili Membe aoteshwe na tumpigie debe la nguvu ili awe mgombea wa CCM, candidature yake ni muhimu sana kutupeleka kwenye ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

Kama tutamkosa EL, then Membe atatufaa sana!.

Membe for 2015!.

Mkuu bado una imani na 'nyerere?' Ila ni fikra huru hata hivyo. Kiukweli Membe anajua kuongea kwa kujiamini sana, na sijui anatoa wapi hizi confidence. Nadhani kwa upepo unavyokwenda itafika siku atasema 'nimeota'. Nami binafsi sikupenda jinsi alivyowakarimu cdm. Ile ni dharau.

Kuhusu joka la mdimu kakumbushia bifu lake na Mudhihiri katika sakata la kiwanda cha saruji huko kwao. Ni bora angekuwa jibwa liso meno. Maana halisi ya joka la mdimu ni kuwa kuna nyoka hupenda kukaa kwenye mndimu. Hali ndimu wala nini ila waendao kuchuma ndimu huambulia kugongwa na joka hilo. Hivyo joka la mdimu si la kuchezea (hapa simsemi Membe).
 
Hapana. Kwa maneno yao utawajua. Membe anaamini kwamba yeye anaweza kuwa chaguo la mungu, akaoteshwa kama manabii walivyokuwa wanaoteshwa.

Katika nchi secular viongozi wenye fikra hizi ni wa hatari, kwa sababu hawaheshimu sana rule of law na the masses, wanaheshimu sauti "ya kuoteshwa" ambayo hatujui hata inapotoka.

Ndiyo haya haya ya kina Idi Amin, mtu anaamka anasema "nimeoteshwa wewe unataka kuniua" anakuchukua na kukuuilia mbali.

Kwa nini mtu mwenye umakini aongee vitu vague kama kuoteshwa katika kinyang'anyiro hiki ?

Wengine tukisikia mtu anaongelea sana kuoteshwa tunaanza ku suspect labda jamaa ni schizophrenic au ana matatizo fulani ya kisaikolojia.

Atuambie kitu cha kueleweka, hizo habari za kuoteshwa awaachie wahubiri na wachuuzi wengine wa maneno.

Of course anaweza kututhibitishia kwamba hata na yeye ni mchuuzi wa maneno asiye na la zaidi kwa kuendelea kukazania habari ya "kuoteshwa"

Hapa una hoja. Suala hilihili la kuoteshwa linaweza kugeuzwa na likampindua Membe vibaya mno kiasi hataamini. Cha msingi tu kama anataka urais aachane na dhana za kuoteshwa. Na akishaoteshwa kugombea urais na kwa bahati akaupata, itafika siku atasema kaoteshwa kuwa upinzani hautakiwi
 
Vizuri nimeipenda hiyo,sijuhi kilaza atajibu nini manake tuliona ata yule jamaa aliyegombea ubunge wa EAC kupitia chaema alivyokuwa anajieleza kwa kukwama kwama kama vile gari inatembea kwenye makorongo wenzake walikuwa wanajieleza vizuri na kueleweka kama vile gari inatembea kwenye lami yeye alijitumbukiza baharini wakati kuogelea hajuhi kutafuta umaarufu matokeo yake kahaibika sidhani kama atakuja kurudi tena kilaza yule ha ha ha ha ha ha yule bwana Anton Komu!
 
Tatizo letu tunaangalia sana theatrics kuliko substance.

Ndizo habari hizi hizi za "Membe ana confidence" zilizofanya watu wamchague "JK handsome".

Kwa kweli mie sijaona kitu hata kimoja alichofanya Membe ambacho kina merit presidential ambitions hata za kuota tu.

Labda mniambie, kipi kikubwa alichofanya? Sanasana naona blunders na corruption tu, fiasco na flops tu, hakuna anachoweza kujivunia kwamba kafanya cha kueleweka mpaka sasa.

Tatizo letu wengi hatuwezi kuona past the theatrics na kuchambua mantiki i wapi na maigizo yaso mshiko ya wapi.
 
shida ya huyo dogo wa ITV anauliza leading questions zaidi...anashindwa kuuliza maswali ya kumfanya mtu afunguke zaidi.

ana opportunity kubwa sana huyu dogo lakini haitumii...sorry for him.
Usimlaumu dogo, Membe na wengine huwa huwa wanalipia airtime yao, kwa hivyo hupeleka maswali wanayotaka waulizwe.
 
Halafu kusema "watakimbilia Kenya" kunaonyesha kijamaa kilivyo mufilisi katika diplomasia.

Rule number 3 of diplomacy, kama huna haja ya kutaja jina usitaje jina, angeweza kusema watakimbilia nchi jirani, or better yet, watakimbia nchi.

Sasa Wakenya wakianzisha beef naye kwa kuwasema kwamba nchi yao ndiyo ficho la maadui wa watu influential Tanzania atasema nini?

Na huyu ni one of the top diplomats wetu, hata diplomasia hajui!!
 
Huyu ndio Pasco ninaemjua?
Vin Diesel, Pasco ni yule yule, juzi, jana na hata kesho!. Sikuzote ninasimama kwenye ukweli, kuwa kwa 2015, mgombea bora kuliko wote kwa CCM ni EL, ila kiukweli, afya ya EL inanitia mashaka kwa mikiki mikiki ya 2015, hivyo nawaomba wale mashabiki wangu na chaguo la EL, kama tutamkosa, tuhamishie majeshi kwa Membe, huyu kwa 2015, atatusaidia sana kupata ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania!.
 
Hapa naona kama Membe ametumia nguvu kubwa sana kufikiria ili aonekane ni mwanasiasa mbunifu! Waziri mkuu ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni. Maswali kwa waziri mkuu ni kutoka kwa wawakilishi wa wananchi kwenda kwa mpokea/mtumia kodi (executive rep) ambaye ni waziri mkuu. Kupitia kwa wawakilishi wao wananchi wanauliza ukekelezaji wa miradi mbalimbali.

Sasa anataka mkuu wa kambi ya upinzani aulizwe nini kama si kutaka kutumia muda wa wananchi vibaya huko bungeni? Upinzani wanakusanya kodi? Upinzani wanaandaa sera? Upinzani wana-sign mikataba na makampuni ya nje au wanatoa misamaha ya kodi? Upinzani wanandaa sera? CCM wana tatizo gani?

Well said, jamaa anashida sana kwani bado anatamaka terminology n aupuuzi unaotokea katika jumuia ya kimataif atoka ka nchi zilizo na uongozi dhalimu.Ni kama vile alivyokuwa akisisitiza kuwepo kwa majadiliano na GHaddafi .Yani kama leo mtu asisitize mazungumzo ya madaktari na serikali wakati mambo kama ya ulimoka yakitokea.

Membe yupo too artificial.Namuombea ajikute katika midahalo na jembe lolote la CDM live katika TV na Masako ili pasiwepo n akubebwa au kupotezewa issues.Huyu jamaa tutaoa posi lake kam la sanamu likotoka.

Sijui hajajiliza pamoja na kwamba CCM si wapinzani rasmi kama walivyojisahau,ila hajafikiria majibu yanayoweza toka kwa kiongozi wa upinzani kwa maswali yahusuyo: Ulizni wa raia(ulimboka, wabunge wa CDM), chaguzi huru(wizi wa kura), mahusiano ya kimataifa(Israel), ufisadi, serikali legelege, na bunge linalochikiliwa na akili ndogo juu ya kubwa etc.Membe mstaarabu wa kuigiza anachekesha saaaaana.
 
Back
Top Bottom