Bernard Membe huna sifa wala uwezo wa kuwa 'campaign manager' wa Rais Samia

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,666
15,065
Aliyekuwa mgombea urais wa ACT Wazalendo kwenye uchaguzi mkuu wa 2020 na akaishia kufanya kampeni kwenye kijiji cha Rondo huku akijinasibu kuwa anataingia na kufunga goli dakika ya 90 bwana Bernard Membe, leo mbele ya waziri mkuu ametangaza kumuunga mkono rais Samia na kusema yupo tayari kuwa kampeni meneja wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025!

Bwana Membe huwa anapenda kujitwisha sifa ambazo hana, ikumbukwe mwaka 2015 aliingia tano bora kwenye mchujo na kuishia kubwagwa hadi na kijana mdogo January Makamba.

Bwana Membe amekuwa waziri kwa miaka 15 lakini hakuna alichoifanyia nchi hii na wala hana legacy yoyote aliyowachia Watanzania

Membe asema yuko tayari kurudi mahali fulani | Mwananchi - Membe asema yuko tayari kurudi mahali fulani
 
Ni waziri gani kwenye nchi hii unaweza sema kweli wakati akiwa waziri wizara yake aliitendea haki, na atakumbukwa na Watanzania? Kwanza huo ufanisi wa waziri utaupimaje, leo yupo hapa, kesho pale, badaye anawekwa benchi, kabisa, baada ya muda tena unamsikia amepewa wizara fulani!!

CCM mbona kazi mnayo, na membe ndio huyo sasa anaingia na usije shangaa ana pewa na nafasi ya uteuzi!!yaani magamba ni kama ushirika wa wachawi , kiongozi anaingia na timu yake, wengine wanabaki yatima kwa muda, BASHIRU, na POLEPOLE, ki ukweli wanapata tabu sana!!kweli ONDOKA UDHARIRIKE.
 
Humjui membe benard hajafanyia nn nchi hii jamani hebu mpeni heshima yake

Ungesema ukaribu wake namama unaweza kua kipengere kingine kwn anahamu Sana na urais
 
Mchokozi ni Majaliwa aliyemfata BCM hadi kijijini kwake. Membe alikaa zake kimya kijijini ila mmemfuata ili msikie atasema nini. Ameongea sentensi mbili tu Sukuma Gang wameanza kujiharishia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom