Bernard Membe, Edward Lowassa, Fredrick Sumaye sio viongozi wa kuigwa

DOMBWELA

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
682
1,000
Hao ni baadhi ya viongozi ambao sitamani tena kuwa mfano wa kuigwa kwangu tena katika maisha ya kisiasa na maisha kwa ujumla.

Nikiangalia heshima waliojijengea na waliyojengewa katika utumishi wao na maisha ya kisiasa siwaelewi lakini pia wananiumiza!.

Juzi nikawa najiuliza, hivi hawa wazee wangu na viongozi wangu nini kilichopelekea kukosa msimamo katika maamzi yao ya kisiasa mpaka kupelekea maisha haya ya kutoaminika, katika jamii na kisiasa pia?.

Je ni tamaa ya fedha au tamaa madaraka imepekea maisha haya waliyoyachagua?.

Kwenye chama Chetu pendwa hatuna imani nao, huko walikotoka nako pia ndio usiseme, na ndani ya jamii yetu ya Kitanzania hatuwaelewi kabisa!.

Yote na yote itoshe kusema ukweli wa ndani ya nafsi yangu, hawa wazee wangu na viongozi wangu wananiumiza moyoni mwangu!. Nimeamini maneno ya jamii yangu yanayosema, "mwanaume hujigeuza kitandani nasi katika msimamo au katika kauli zake".

Mungu awasaidie katika maisha hayo waliyoyachagua.
 

Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
11,812
2,000
Ulitaka wafanye nini labda ili personality zibaki pale juu?

Maana kushuka kwao ki siasa kulitokana na ku m under estimate boss wao mpya(JPM). Na kutaka kuonesha wao ni wanamabawa makubwa kuliko Bro JPM matokeo yake wakakaa wao.

CCM ni kubwa kuliko hata hao wakina Lowasa, Sumaye na Membe.
 

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
31,597
2,000
Hao ni matapeli wa kisiasa, ni ma opportunist tu. Aibu yao aibu ya familia zao. Walimsema vibaya sana JPM walipokuja kutafuta fursa huku upinzani lakini sasa hivi hata akiwaita kwa ishara ya vidole wanaitika.
 

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
3,075
2,000
Ulafi wa Mbowe uliwaponza ila wanasiasa hawaonagi aibu.
Mbowe a.k.a baba wa taifa wa pili atawatoa roho ,kaeni nae hacheni kujikuta, mh mbowe ni mwenyekiti wa chama kwanye wafuasi si chin ya m 14 KWA Sasa ,je mwajua hilo? anapendwa KWA asilimia 81,mwajua hilo ?
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
13,688
2,000
inabidi upinzani wawe careful na kiongozi yoyote anayetokea CCM na kutaka kujiunga nao...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom