Bernard Membe azungumza Star TV, adai anachambua hali halisi na kushauri

TOILET PEPA

Member
Jan 24, 2016
6
2
Fuatilia umsikie...

===========

Kupitia kipindi cha Mahojiano cha Star Tv, aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali ya Awamu ya Nne ya JMT, Mhe Bernard Membe yuko Live kuzungumzia masuala kadha wa kadha kuhusu mwenendo wa serikali mpya iliyopo madarakani.

Update:

Mhe. Membe anasema wazi kuwa ufutwaji wa matokeo yote huko Zanzibar kumeishangaza dunia, hasa ukitilia maanani kuwa uchaguzi ule ulikuwa na waangalizi toka Marekani, Jumuiya ya Ulaya, African Union na SADC na waangalizi wote hao walitoa taarifa zao kuwa uchaguzi ule ulikuwa huru na haki, kwahiyo walishangazwa na uchaguzi ule kufutwa wote..

Anaendelea kusema, ilimradi Jecha keshatangaza tarehe ya marejeo ya uchaguzi huo tarehe 20/03/2016, anavisihi vyama vyote vishiriki uchaguzi wa marejeo.

Anawazungumzia pia watu ambao hawakumuunga mkono Rais Magufuli wakati wa kampeni na kuwaita ni wanafiki na wamesubiri mpaka awe Rais ndio wanajitokeza na kuanza kujinasibu nae..

Kwa maoni yake, Mhe Membe anasema yeyote anayekihama chama hapaswi kuruhusiwa kurejea tena, na anapokivua nguo chama huko pia ashughulikiwe huko huko huku akitolea mfano wa jinsi chama cha ANC cha South Africa kilivyokuja na sera ya "gate valve" kwa wale wanaotoka na kuhamia vyama mbadala kutoruhusiwa kuwa wanachama wa chama hicho pale wanaojisikia kufanya hivyo.
 
Ila hapa jf ukifuatilia kwa makini topic zinazoanzishwa na bavicha unapotea. Membe anaongea tofauti na ilivyokua inaelezwa hapa
 
Amasemaje kwani ,nilivyo ona tangazo kuwa ni Star tv nikajua tu ataenda kusema yeye hakumaanisha kilicho andikwa kwenye magazeti
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom