News Alert: Bernard Membe ataka Msaidizi wake Jerome Luanda aliyetekwa arudishwe bila Mchubuko, vinginevyo watafikishana Mbali, hela za Kampeni zatajwa

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
1,717
2,000
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Bernard K. Membe amenena yafuatayo :"Tukio la kutekwa kwa Msaidizi wangu Jerome Luanda jana mara baada ya kutua kwenye kiwanja cha Kimataifa cha JK Nyerere international Airport nitalizungumzia kwa undani Saa 10 kamili leo. Nimewapa wahusika wanaodhani siwajui masaa matatu wamwachie akiwa mzima na salama."

News Alert: - Polisi yasema inamshikilia msaidizi wa Membe Jerome Luanda, anatuhumiwa kwa kosa la kutakatisha fedha

Soma: Msaidizi wa Benard Membe, Allan Kiluvya adaiwa kutekwa na watu ‘wasiojulikana’


Screenshot_20200916-153743.png


MEMBE ATAKA MSAIDIZI WAKE ARUDI BILA MCHUBUKO

Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Bernard Membe amesema waliomteka Msaidizi wake, Jerome Luanda na kwenda kumkagua nyumbani kwake wamuachie haraka

Membe amedai kuwa, Jerome alitekwa mara baada ya kutua kwenye Uwanja cha Kimataifa wa Julius Nyerere

Amesema, Septemba 17 ataongea na Waandishi wa Habari ili kuelezea zaidi kuhusu tukio hilo. Aidha, amesema sio vyema kutumia Polisi kama kichaka cha kujificha

#JFLeo #JamiiForums #Uchaguzi2020 #TZ2020
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom