Bernard Membe arithi nafasi ya Maalim Seif, ateuliwa kuwa Mshauri Mkuu wa ACT Wazalendo

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,397
Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemteua Bernard Membe kuwa Mshauri Mkuu wa Chama hicho kuanzia jana, Agosti 02, 2020

Zitto amesema amefanya uteuzi huo kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 85(1) ya Katiba ya Kiongozi wa Chama hicho

Membe aliyehamia chama hicho hivi karibuni akitokea CCM anaenda kushika nafasi ambayo awali ilishikwa na Maalim Seif kabla ya kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho

EefHAvkXoAMCCsn.jpg
 
Duh, tangu Lini Membe ameshaiva na kujua itikadi za ACT. Upinzani wa TZ in pasua kichwa, kichefuchefu tupu. Huko Ufipa wako bize kumpitisha Nyalandu. Halafu kuna mijitu itashangaa na kubisha kuwa wagombea wote mwaka huu siyo wa CCM!!

Kama kawa kama ilivyokuwa 2015, mwaka huu tutegeme mtanange kati ya CCM iliyo ACT, au CCM itakayotoka CDM leo. Then, Matokeo tayari ya OCT. Kwani kuna swali???
 
Huu uzi unahusu ACT wachana na kukitaja chama tawala ifikapo november baada Lissu kuapishwa.
Duh, tangu Lini Membe ameshaiva na kujua itikadi za ACT. Upinzani wa TZ in pasua kichwa, kichefuchefu tupu. Huko Ufipa wako bize kumpitisha Nyalandu. Halafu kuna mijitu itashangaa na kubisha kuwa wagombea wote mwaka huu siyo wa CCM!! kama kawa kama ilivyokuwa 2015, mwaka huu tutegeme mtanange kati ya CCM iliyo ACT, au CCM itakayotoka CDM leo. Then, Matokeo tayari ya OCT. Kwani kuna swali???
 
Nafkiri wamefanya hivo ili mchizi asiondoke, ila time will tell. Jamaa atasepa tu akikosa urais atarudi zake ccm.
 
Hahhahaha... Hiki chama kinachekesha sana muundo wake!

Yani inaonekana Zitto ana mamlaka ya kuteua na kutengua muda wowote akitaka!
 
Zitto ndo DIGALA mwenyewe, anawapangia kazi kina Maalim Seif na Benard Membe.
 
Safi sana, Vichwa makini vikiungana ni sawa na CPU nyingi zifanye kazi kwa kushirikiana, Hapo outcome lazima itakuwa ni more efficient.
Nawapongeza sana ACT kwa kufanikiwa kukileta kichwa kama Membe ndani ya safu ya watu makini.
 
Back
Top Bottom