The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,503
- 2,046
Baada ya kuwasikiliza wagombea wa upinzani ambao tayari wameshaanza kampeni zao, nimejaribu kubainisha tofauti zao, ambapo kwa mtazamo wangu naona Bernard Membe ana uwezo Mkubwa sana wa kuongelea mambo ya wananchi kwa lugha rahisi na inayoeleweka.
Aliongea kuhusu mazao ya kilimo na changamoto za masoko, wavuvi na changamoto zao, watumishi wa umma na kuporwa mishahara yao kwa lugha rahisi mno. Kwa upande wake Tundu Lissu, ana uwezo mzuri wa kuongea, lakini anaongea kwa jazba, anatumia muda mwingi kuongelea mambo ya haki za binadamu, kumuongelea Dkt. Magufuli na kuongelea jinsi wapinzani walivyofungwa kusumbuliwa na Polisi, alivyopigwa risasi.
Haya mambo hayana impact kubwa kwa wananchi wa kawaida walio wengi. Kwa maoni yangu ajikite kuelezea matatizo yanayogusa watu wote, na jinsi atakavyoyatatua.