Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 975
- 47
Mchezaji mpya wa Timu ya Manchester United Dimitar Berbetov ametakiwa kupunguza kama si kuacha kabisa tabia yake ya uvutaji sigara kama anataka kuendelea kupata namba kwa muda mrefu kwenye kikosi cha Man U. Imefahamika kuwa Berbetov anavuta sana sigara na kitu ambacho kilionyesha walakini wakati wa kufanyiwa Medical Checkup aliposign na klabu ya Man U. Pumzi yake haikuwa sahihi sana na vipimo vya mapafu vilionyesha moshi na ukungu baada ya kumuuliza alikiri kuvuta sigara lakini mwenyewe alisema kwa sasa amepunguza kilisema chanzo cha habari hii ndani ya klabu ya Man U. Hata hivyo mchezaji huyo bado hajajiunga rasmi na klabu ya Man U kwani alikuwa akiiwakilisha timu yake ya Bulgaria kwenye mchezo wa awali kucheza fainali za kombe la dunia ilipocheza na Montenegro na kutoka droo ya 2-2.