Beraking lakini sio News Waliokunywa dawa ya babu Kupukutika kidogo kidogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Beraking lakini sio News Waliokunywa dawa ya babu Kupukutika kidogo kidogo

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Feb 12, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  ]Wagonjwa wote wa kisukari waliokunywa dawa kwa Mchungaji Ambilikile Masapile ‘Babu' kijijini Samunge, Loliondo watakufa (au watapukutika) ikiwa wataacha kutumia dawa za hospitalini, Uwazi limegundua.

  Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, watu wengi waliokunywa dawa ya Babu ambao walikuwa na ugonjwa wa kisukari wamefariki dunia baada ya kuacha kutumia dawa za hospitalini.
  Baadhi ya ndugu waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa, mara baada ya ndugu zao kunywa dawa ya Babu, waliacha kunywa dawa za hospitali na matokeo yake sukari ilipanda au kushuka, hivyo wakaaga dunia.

  Ndugu wa marehemu Juliani Lyasenga mkazi wa Arusha ambaye alibahatika kunywa dawa ya Babu kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari, alikufa baada ya kuacha kutumia dawa kama alivyoelekezwa na daktari wake.
  Mwingine ambaye alikufa baada ya kunywa dawa ya Babu kutokana na kuugua kisukari ni John Piswa, mkazi wa Tandika, Rafael Kisijo mkazi wa Kijitonyama, Saidi Mohamed mkazi wa Buguruni na Hausi X. Hollo "HH", mkazi wa Gongo la Mboto.

  HAITIBU KISUKARI
  Licha ya dawa hiyo ya Babu kuaminika kuwa inatibu magonjwa kadhaa sugu ukiwemo wa kisukari, imeelezwa kuwa hadi sasa hakuna dawa iliyothibitishwa kitaalam kuwa na uwezo wa kutibu maradhi hayo.

  "Kwa kifupi, hii ni aibu. Serikali haipaswi kuogopa kusema ukweli kuwa dawa ya Babu haitibu kisukari. Wote wanaosumbuliwa na ugonjwa huo nawaomba wasiache kutumia dawa za hospitali.
  Wakifanya hivyo watapoteza maisha, najua kwa kusema hivi sasa mawaziri wapo matumbo moto, lakini huo ni ukweli," alisema daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambaye aliomba jina lake kuhifadhiwa kwa kuwa si msemaji.

  Aliitaka serikali kusema ukweli juu ya hilo ili kuokoa maisha ya Watanzania wengi ambao wanaamini kisukari kinaponywa kwa kikombe cha Babu, hali inayofanya baadhi yao kuwa hoi kwa kuzidiwa na ugonjwa huo.

  AINA MBILI ZA KISUKARI
  Alifafanua kuwa, kuna aina kuu mbili za kisukari kama wataalam wa tiba walivyoweza kuzigawa. Aina ya kwanza ni kisukari ambacho mtu anakipata tangu wakati anazaliwa hadi anapofika umri wa miaka 35, ikamaanisha kuwa katika muda huo mtu anaweza akaugua kisukari.
  Aina ya pili ni kile ambacho mtu hukipata anapofika umri wa miaka 40 na kwenda juu. Vile vile kuna kisukari humtokea mtu anapokuwa na mimba, akasema hicho huitwa kisukari cha mimba.

  "Aina mbili za kisukari nilizoelezwa zina tiba zinazotofautiana. Mgonjwa anayepata kisukari cha kwanza hutakiwa kufuata miiko (kutokula vyakula vya sukari), kisha hutakiwa kuchoma sindano yenye dawa ya Insulin ambayo hufanya kazi ya kuiweka sukari ndani ya mwili katika kiwango kinachotakiwa.

  "Mgonjwa wa kisukari wa aina hii hutakiwa kuchoma sindano ya Insulin mara mbili au tatu kila siku. Mara nyingi wagonjwa hufundishwa kujichoma wenyewe sindano au kwa watu walio karibu nao. Kutokana na hayo, sikuona sababu ya serikali kutongoja uchunguzi wa kisayansi kuhusu dawa ya Babu kabla ya kuiruhusu kutumika," alisema daktari huyo.

  MAJIBU YA WAZIRI BUNGENI
  Akijibu swali bungeni katika kikao cha bunge kilichopita mjini Dodoma , Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya alisema kuwa, hadi sasa tafiti za kitaalam zilizofanywa nchini na duniani zimeonesha kuwa, dawa zote zilizopo pamoja na za asili zina uwezo wa kudhibiti ugonjwa usisababishe madhara zaidi lakini hazina uwezo wa kuponyesha kabisa.
  [​IMG]"Katika mfumo wa tiba asilia, kuna dawa nyingi zinazotumika kudhibiti ugonjwa wa kisukari mwilini kama ilivyo katika mfumo wa tiba za kisasa. Wizara kupitia Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na Taasisi ya Tiba Asili ya Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba ya Jamii Muhimbili, hufanya tafiti mbalimbali za dawa asili zinazosadikiwa kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo kisukari.
  Matokeo ya tafiti hizo hayajaonesha dawa yoyote ya asili yenye uwezo wa kutibu kisukari,"alisema Dk. Nkya.

  Dk.Nkya ambaye alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kidawa Hamisi aliyetaka kujua tamko la serikali kuhusiana na wimbi la waganga wa tiba za asili wanaojitangaza kutibu ugonjwa wa kisukari, alisema kuwa dawa inapotangazwa kwenye vyombo vya habari lazima iwe imefanyiwa utafiti wa kitaalam na kuthibitishwa kuwa ina uwezo wa kutibu, kinyume chake ni uvunjwaji wa sheria namba 23 ya mwaka 2002 kuhusu tiba mbadala na kanuni zake.

  Alisema wataalam wa miti shamba kabla ya kutangaza hizo dawa zao kwa umma wanapaswa wawasiliane na waganga wakuu wa wilaya na mikoa ili taratibu za kuzifanyia dawa hizo utafiti wa kisayansi zifanyike.

  Dk.Nkya aliitahadharisha jamii kuhusiana na dawa hizo asili zinazotajwa kutibu ugonjwa wa kisukari kuwa hazitibu zaidi ya baadhi kuthibitika kuudhibiti ugonjwa na kwamba wananchi wajenge tabia ya kwenda kuchunguza hali ya afya zao mara kwa mara ili kuwezesha kudhibiti ugonjwa mapema.
  [​IMG]Hata hivyo, uchunguzi wetu umebaini kuwa licha ya majibu hayo mazuri ya naibu waziri huyo, hivi sasa serikali imekuwa ikiacha watu, wakiwemo mawaziri na wafanyabiashara mbalimbali wakienda kwa Babu Loliondo na kunywa dawa ambayo bado haijathibitishwa kisayansi kama inatibu magonjwa yanayotajwa.

  Wakati huo huo, viongozi mbalimbali wa serikali wamelaumiwa na wananchi kwa kitendo chao cha kwenda kwa Babu kwa ‘mgongo' wa serikali kumbe wana nia ya kunywa dawa.

  Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti walisema viongozi wa serikali wakiwemo mawaziri, wakuu wa mikoa, majaji, wakuu wa wilaya na hata makamanda wamekunywa dawa ya babu kwa kutokaa kwenye foleni.

  "Mara baada ya kufika nyumbani kwa Mchungaji Masapila, huwa wanaandaliwa eneo maalum na hujifanya wana mazungumzo ya kiserikali lakini baadaye kila mmoja hupata kikombe cha dawa, na kuwaacha wananchi kwenye foleni. Hili ni kosa kubwa kabisa kiimani," alisema mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Aloyce Ngongoa.

  Baadhi ya mawaziri waliopata kikombe kwa Babu wa Loliondo ambao picha zao zipo ukurasa wa mbele wa gazeti hili ni William Lukuvi, Steven Wassira, John Magufuli, Teresya Hovisa na Wakuu wa Mikoa Abbas Kandoro, Yohana Balele, mtoto wa baba wa taifa, Rose Nyerere na Mbunge Nimrodi Mkono.
  [​IMG]Wengine ni Augustino Mrema, mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa, (pichani) Frederick Sumaye, Mkuu wa Wilaya, Edmund Mjengwa na viongozi wengine wa chama na serikali.

  Raia wa kigeni
  Mamia ya raia wa kigeni kutoka nchi mbalimbali duniani nao wamekuwa wakimiminika katika Kijiji cha Samunge kupata tiba ya magonjwa mbalimbali.

  Kwa mujibu wa takwimu zinazokusanywa katika eneo la utoaji wa dawa, raia hao wa kigeni wametoka Kenya, Marekani, Finland, Uholanzi, Sri Lanka, Jumuiya ya Falme za Kiarabu (UAE), Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Uganda, Rwanda, Burundi na Comoro.

  Nayo Idara ya Uhamiaji tayari imepeleka ofisa wake ambaye ameweka kambi Samunge kupitia nyaraka mbalimbali za wageni wanaoingia kijijini hapo kunywa dawa.
  [​IMG]


  chanzo. http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/dawa-ya-loliondo-waliokunywa
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Bado kwa imani yangu siamini katika miujiza, katika Mungu aliye hai. Ingekuwa nchi nyingine babu angenyongwa hadharani kwa utapeli wake wa wazi wazi na kusababisha vifo.

  Mungu wa babu naamini si Mungu aliyeumba dunia na vilivyomo ndani. Kauli ya Mungu siyo ya kujichanganya kama tulivyo binadamu tuseme hafafu tusitekeleze.
   
 3. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Babu kawatia changa la macho wengi.....
   
 4. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Babu mwenyewe hakunywa kidogo?
   
 5. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Hivi JF sasa itakuwa inajadili magazeti ya udaku? hakuna members humu aliyewahi kusoma hata Newsweek?
   
 6. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  babu genious balaa
   
 7. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2012
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Unajua dawa ya babu imeathiri mapato ya matapeli wengi wa dini, sasa wanajitahidi kila njia kuipiga vita dawa hiyo
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mleta mada naamini haelewi kuwa sasa hivi Babu anapata wageni wengi sana wa nchi za mbali!
  Haya maneno ya gazeti ni ya kutunga ili kuuza!
   
 9. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Habari yenyewe kuisoma mpaka mtu ujipange
   
 10. H

  Hassanali Member

  #10
  Feb 13, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata baba aliwaambia lazima waendelee na za hospitali. Alafu heading yako iko misleading kidogo: waliokunywa watapukutika! means you are going to die just because ulikunywa dawa ya babu.
  Kwa wengi waliotumia hiyo dawa kutibu kisukari chao, walipata improvement kubwa. Walichotakiwa, just like any dawa, was to keep taking the dose. Walitakiwa kuendelea na dosi za za hospitali hata baada ya kupata nafuu.
   
 11. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2012
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Rekebisha kichwa cha habari
   
 12. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  babuuuu!aliniacha hoi pale aliposhindwa kumponya mtoto wake.
   
 13. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160

  Mkuu vipi na wewe ulipitia kimkombe cha babu nini? mbona unakitetea kwa nguvu zote? Kwa upande wangu hii habari ni nzuri kwa Taifa hasa kama hao waliokunywa watakufa kweli basi babu ametusaidia kwa kiasi fulani cha kusafisha mafisadi walio serikalini wengi walienda kunywa hizo dawa. Kama ni kweli watakufa basi tutegemeeni maajabu ya Mafisadi kuondoka muda wowote.
   
 14. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160

  Tapeli tu huyu babu hana lolote, kashaua watu wengi mno mpaka sasa.
   
 15. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2013
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  hii kitu yaweza kuwa kweli!
   
 16. b

  bidada Senior Member

  #16
  Feb 15, 2013
  Joined: Jan 12, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hiyo dawa ilikaa kiimani zaidi mi nina ndugu wawili wamepona sukari mpaka sasa wazima kabisa.
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2013
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mpaka "Tyson"? Watanzania tunajidai wajanja kumbe tunaptikana kwa vitu vidogo tu!
   
 18. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2013
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ukiwa na maana kuwa unatoka nyumbani kwako, unatowa fedha za usafiri, unahimili mikiki halafu yote hayo huna imani na unachokifuatia?
   
 19. Root

  Root JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2013
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,301
  Likes Received: 13,011
  Trophy Points: 280
  Hahahah wajinga ndio wanao liwa.
  Mkanywa maji machafu,mkapanga foleni,mkapoteza hela
  We toka lini hela ya safari ikawa ndefu kuliko ya matibabu?
   
 20. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2013
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  naombeni mlioenda kutibiwa india mniambie kati ya nauli na malipo pale appolo ni ipi kubwa?
  baada ya hapo nitajua nani **** kati ya babu na mteja.
   
Loading...