Beno Malisa; kwa hili la NYALANDU unastahili PONGEZI.......

Kama Baba lao liliingia Ikulu kwa EPA na Kagoda, nani atamnyoshea mwenzie kidole?

Nyalandu alitumia tshs.62,000,000 kupata ujumbe wa NEC kutoka wilaya yake ya singida vijijini,Uongozi wake wote ikiwemo na Ubunge alipata kwa kutumia Rushwa kubwa, hivyo huyo jamaa ni mtoa Rushwa mzoefu.
 
Pamoja na Makonda kuadhibiwa kutokana na kuungwa mkono na watu flani ila vile vile ilionekana kuwa kauli ya Raisi wakati akitoa hotuba yake kwamba "vijana wasichague watu wenye ndimi 2" ilimlenga Makonda na ilimgharimu vile vile kwani amekuwa akisikika na kuonekana akitoa kauli tata mara nyingi dhidi ya Chama chake.



Niwapongeze walioshinda hasa huyu dada Mboni Mhita kwa kuwa kama vita hii ya kwake ilikuwa kama ile ya Iraq...... Hongereni sana mkajipange sasa kuendelea kuijenga Jumuiya kama ambavyo wenzenu walijitahidi na kuifikisha hapo ilipo! Msije mkawa vichaa kwa kuchukua mabaya na kuacha mema.......... Kubwa achaneni na makundi

Kumbe kukikosoa chama ni dhambi kubwa kwa CCM????

Yaani mnakubali kumtosa mtu anayekikosoa chama na kumchagua kibaraka wa mafisadi akina EL na kisha mnampa pongezi kwa kushinda vita???????

CCM mna safari ndefu sanaaaaaa
 
Hivi kama chaguzi za ndani za CCM ni kununua kura hivi huyo EL ataweza kununua kura za wtz
wote kwenye uchaguzi mkuu2015? Hamuoni kuwa watz wa sasa ni tofauti na wale wa 2005 wa kanga na tisheti?
Kumbukeni kauli mbiu ya kule Arumeru Mash.''kula ccm, kura CDM''.
 
Kaka katika hili hamna jipya kwani mie nabaki mdomo wazi kuwa nani ni msafi. Baba kaingia madarakani na EPA, siasa chafu, mtoto katajirika sekunde, mama mjumbe wa nec taifa, na bia mawaziri takribani wote maswaiba. Kwa haya yote mta tudanganya watanzania mna lengo lakujenga nchi kweli, ebu wazalendo tuungane tudai nchi yetu kwani hata sasa wana saka kusaini mikataba ya gasi, mafuta na ureniam ili waweke ten percent yao kwakweli umefika mda hata kama ndani ya ccm tu elezane wazi jamani hawa fisi wata tumaliza jamani.
 
Back
Top Bottom