Beno Malisa; kwa hili la NYALANDU unastahili PONGEZI....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Beno Malisa; kwa hili la NYALANDU unastahili PONGEZI.......

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Meitinyiku L. Robinson, Oct 24, 2012.

 1. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku ya jana ilikuwa ngumu na kipekee kwa vijana wa CCM hasa ulipowadia wakati wa uchaguzi na hasa baada ya kudondoshwa kwa kipenzi cha mtoto wa Raisi A.S HAPI. Mgombea huyu aliyetajwa kuungwa mkono na kijana huyo wa Rais kwa kuwezeshwa kuzunguka Nchi nzima alidondoshwa katika awamu ya kwanza kwa kura za hasira baada ya kujulikana kwa aliyekuwa nyuma yake.

  Baada ya kudondoshwa walirudi Makonda na Mboni ambao walipigiwa kura tena baada ya kuonekana kuwa hawakufikia 50% kama ambavyo Kanuni inahitaji. Sasa baada ya kurudi kwa majina haya ile kambi ya kijana wa Rais ilihamisha nguvu kwa Makonda na nguvu hiyo iliongozwa na Mh. Lazaro Nyalandu, Catherine Magige, Wakuu wa Wilaya na vyombo vya usalama.

  Nyalundu alionekana akiita baadhi ya vijana na kuwakatia fungu akiwa pamoja na Catherine ili waamishie nguvu kwa Makonda jambo ambalo likiwapa hasira wajumbe wa Mkutano Mkuu na kuona kuwa Nyalandu hakustahili kuwafanyia hivyo. Jambo hili liliwapelekea wajumbe kupuga kura za hasira hata wale waliokuwa wakimuunga mkono Makonda waligeuka na kuamua kumpigia kura Mboni na kushinda kwa zaidi ya kura 200.

  Baada ya Beno kusikia Nyalandu anafanya funo ya hela nje kama kawaida yake aliicha meza kuu na kumfuata huyu Waziri nje na kumwomba ama aondoke eneo hilo au aingia ndani na kumtaka awaache vijana wafanya maamuzi wao wenyewe na si kuwashurutisha. Hatua hii ilimshtua sana Nyalandu na kwa aibu aliamua kuondoka kabisa eneo la tukio.

  Pamoja na maelekezo aliyokuwa nayo msimamizi mkuu wa uchaguzi William Lukuvi na timj yake yote iliyotumwa ukumbini wajumbe wa mkutano mkuu walikuwa wakisimamia maneno haya "kura kwanza maelekezo baadae." Bado haijajulikana jamaa watapeleka majibu gani kwa wale waliowatuma kuhakikisha kuwa yule wanaomtaka anashinda.

  Pamoja na Makonda kuadhibiwa kutokana na kuungwa mkono na watu flani ila vile vile ilionekana kuwa kauli ya Raisi wakati akitoa hotuba yake kwamba "vijana wasichague watu wenye ndimi 2" ilimlenga Makonda na ilimgharimu vile vile kwani amekuwa akisikika na kuonekana akitoa kauli tata mara nyingi dhidi ya Chama chake.

  Wakati huo huo vijana wamesikika wakimshauri kijana wa Raisi ahamie moja kwa moja Marekani kwani inasemekana kuwa ameshanunua nyumba huko na ameshapeleka familia huko alikuwa anasubiri upepo wa chaguzi hizi za Taifa. Hivyo baada ya kushindwa kuweka watu aliowataka yeye kuanzia ngazi za Wilaya, Mkoa na Taifa ndani ya Jumuiya zote na Chama vile vile hana jingine.

  Niwapongeze walioshinda hasa huyu dada Mboni Mhita kwa kuwa kama vita hii ya kwake ilikuwa kama ile ya Iraq...... Hongereni sana mkajipange sasa kuendelea kuijenga Jumuiya kama ambavyo wenzenu walijitahidi na kuifikisha hapo ilipo! Msije mkawa vichaa kwa kuchukua mabaya na kuacha mema.......... Kubwa achaneni na makundi
   
 2. j

  jakamoyo JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  ndio siasa za bongo, zipo kibiashara zaidi.
  Ccm msipobadilika mtapata shida sana 2015.
   
 3. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumekucha.

  Timu ya CCM inapanguliwa na kupangwa upya.

  Tunasubiri kama ni timu ya ushindi 2015.
   
 4. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kumbe huyu nyalandu naye mchafu tu,alikuwa anajibaraguza kuwa ni mwadilifu kumbe walewale 2,shame on u magamba
   
 5. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna aliye salama Ndani ya ccm
   
 6. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Hopngereni vijana wa CCM kwa kukataa rushwa (kama kweli mlikataa maana tujualo ni kuwa mmekula, hata mwenyekiti wenu JK kalalamika)...lakini pamoja na hayo, hamna msaada wowote kwa vijana wa Tanzania kwa kuwa mmechaguana kwa visasi kuwa yule anasaidiwa na mtoto wa Rais basi tumchukie..mkachagua yeyote yule bora hana affiliation na mtoto wa Rais...majungu, chuki binafsi, tamaa..ndio siasa zenu hizo na vigezo vya kuachaguana!
   
 7. I

  Isango R I P

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nyalandu nakusubiri sana Singida use ueleze jinsi ulivyodanganya watoto uakawaapeleka Arusha kuwaonyesha kwaw watalii ukachukua pesa zao. Tania yako si njema sana.mtoa rushwa mkuu. We u atuaibisha sana watu wa Singida. Ovyoa kabisa Nyalandu
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Naamini uchaguzi wao utawapa nafasi ya kumlaumu rizimoko pale hawa waliochaguli wataposhindwa kutekeleza majukumu yao kwa kiwango cha kuwashawishi vijana waiunge mkono ccm. pengine kutomuunga mkono rizimoko inaweza kuwa ni kosa kubwa sana kwa uvccm na wataligundua hilo jua likizama. poleni uvccm kwa kuchagua magalasa na kuacha mizungu.
   
 9. S

  Shembago JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magamba ni janga la kitaifa!
   
 10. m

  makelemo JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shondola Mbona uchaguzi wenyewe unaonekana wa ovyo, nafikiri pengine alichokitaka Riz 1 kilikuwa bora kuliko hao magalasa, tusubiri ikifika jioni tutajua.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. t

  tupel Member

  #11
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  kura za hasira maana yake bora liende Pasipo kujali ubora wa kiongoz hapo tutegemee bora kiongoz
   
 12. C

  Concrete JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mkuu acha hasira tulia kwanza. Hii ni kazi ya mmasai, anaendelea kuwanyoa vipara magamba wanafiki kwa kutumia wembe wake unaoitwa mikakati.
   
 13. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nilisikia huyu Nyalandu kule Marekani aliacha vimeo sana!!!
   
 14. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,830
  Trophy Points: 280
  Tegemeeni mengi ya uyo Mboni ambayo yalikua yamefichika.
  Mboni - kambi ya Lowassa.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Niko hapa Chuo cha Mipango uchaguzi unakofanyika... hata Malisa anatuhumiwam pia kumwaga pesa na kufanyan kampeni za wazi jukwaa kuu kwa ajili nya mboni na wagombea wengine wa NEC kupitia vijana. Nilichokishuhudia ni kwua kila kundi lina dhambi kubwa sana ya kugeuza harakati za kutafuta uongozi kuwa biashara
   
 16. piper

  piper JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Rushwa is part n' parcel ya nyinyiemu tabia ni kama ngozi ya mwili.
   
 17. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  duh lowasa anatsha
   
 18. N

  Ng'ongoampoku Member

  #18
  Oct 24, 2012
  Joined: Sep 18, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aisee huyu jamaa ni mchafu sana ila watu wananyamaza tu kiafrika africa, lakini ukitaka kumchambua ni balaaaaaaa, anyway pia anauzoufu na siasa chafu, hata sisi huku bushi ni noma sana, ukimchagua usipomchagua mambo ni yale yale hakuna aliyemsafi wala hakuna kinachobadilika hata kidogo. anyway God help us
   
 19. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Kama Baba lao liliingia Ikulu kwa EPA na Kagoda, nani atamnyoshea mwenzie kidole?
   
 20. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  bado rushwa ya ngono itakuwa ilitembea sana ..
   
Loading...