Benno Malisa awa jasiri, awageuka CCM na kuwatetea CHADEMA Arusha

Hapo kwenye Dowans huyo bwana mdogo anataka kutuzuga. Wanaostahili kuwajibishwa ni wale walioingia mkataba huo na kampuni ya kitapeli. Wakaweka mkataba wenye masharti dhoofu makusudi na matokeo yake ndiyo haya. Sasa inaonekana anafanya makusudi kuhamisha tuhuma kwa wasiostahili na kuzipeleka kusiko.

Hiyo ni dalili tosha kwamba hakuwa sincere na maneno yake na anaongea asichokiamini. Shame on him!!!!!
 
Kijana naona hujajipanga. Nenda kajipange ili uweze kuyashawishi majembe yaungane na magamba. Majembe sio cuf aka ccm b. Umepotea.
 
KAIMU Mwenyekiti wa Umoja Vijana wa CCM (UVCCM), Benno Malisa amewataka vijana wote nchini bila kujali itikadi ya vyama vyao kuungana ili waliosababisha hasara ya mitambo ya Dowans wawajibishwe. Pia amewataka vigogo ndani ya chama hicho tawala kuacha kuingilia mambo ya chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema hasa mgogoro wake na madiwani wa Arusha Mjini na badala yake watafute suluhu ya matatizo ya msingi yanayoikabili nchi kama mfumuko wa bei na tatizo la ajira.

huyu ajichunge wasije wamkolimba........................hawa wanamagamba ni hatari sana..........
 
Wataweza vipi wakati waliosababisha wanawaita kuwasaidia kwenye kampeni.

Haujamwelewa Malisa, anayetaka wawajibike kwa kutokununuliwa mitambo ya Dowans ni Sita,Mwakyemae na wengine a jamii hiyo wala yeye hataki wawajibishwe walioileta kampuni feki kama Rostam na Lowasa!
 
Haujamwelewa Malisa, anayetaka wawajibike kwa kutokununuliwa mitambo ya Dowans ni Sita,Mwakyemae na wengine a jamii hiyo wala yeye hataki wawajibishwe walioileta kampuni feki kama Rostam na Lowasa!
Wewe ndiye hujamwelewa Sitta awajibike vipi wakati mwizi anajulikana yupo na anataka kulipwa.
 
Tuungane katika lipi hasa. Malisa kmwe huwezi kulisukuma kari la CCM Ufisadi ungali umelipanda ndani.

Ni kweli Vijana tumejiandaa kuliko kawaida katika hili la kuwapa somo mafisadi, lakini pamoja na kwamba baadhi yenu ni wa kuweza kufikirika kama vile Bashe, Malisa ... Shy-Rose Bhanji ...

... lakini kwa sasa hakuna ushirikiano wa aina yoyote mpaka mtakapoamka usingizini, kuona mwanga na kuvuka kuja CDM ndipo tutakapoungana kupigania wale wanaolazwahoi na CCM hivi leo hii. Tafakari juu ya hilo kabla hakujachelewa sana.
 
Huu ushirikiano kati ya mlinzi na majambazi kupora taifa ni jukumu letu sote kuwashughulikia kwa pamoja bila ya visingizio vya 'Utawala wa Sheria' unaolenga kuwanufaisha Rostam Azizi, Lowassa na maswahiba wao kutupora kwa ajili ya kujipatia mtaji wa kununulia urais 2015.

Hakipiti kitu hapa pamoja na kulisajili nalo mahakama zetu kuimba nyimbo zenu mpendavyo. Malipo ya Dowans kwenda na wengi ndio mjue hivo mapeeema!!!!!!!!!!!!!

Wewe ndiye hujamwelewa Sitta awajibike vipi wakati mwizi anajulikana yupo na anataka kulipwa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
  • Beno - kaimu mw/kiti UVCCM -Taifa
  • Catherine Magige -MB
  • Fred Lowasa
  • James Milia
  • Mwalusambo –UVCCM (Wilaya Arusha)..
hapo kwenye red,...kwani yuko kambi tofauti na swahiba wake R1?

Huyu Beno mpaka miezi ya hivi karibuni alikuwa anacheza kwenye kambi zote mbili kimyakimya, sijui kwa sasa hali halisi ikoje ingawa kinachomsukuma ni fedha kuliko kingine.
 
Hapo kwenye Dowans huyo bwana mdogo anataka kutuzuga. Wanaostahili kuwajibishwa ni wale walioingia mkataba huo na kampuni ya kitapeli. Wakaweka mkataba wenye masharti dhoofu makusudi na matokeo yake ndiyo haya. Sasa inaonekana anafanya makusudi kuhamisha tuhuma kwa wasiostahili na kuzipeleka kusiko.

Hiyo ni dalili tosha kwamba hakuwa sincere na maneno yako na anaongea usichokiamini. Shame on him!!!!!

Soma vzr umwelewe,
 
Nani aungane na Gamba wewe? Ninyi na Serikali yenu ndo chanzo hadi tumefika hapo! Pambana kivyenu nasi tutapambana kimpango wetu!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwenye thread kama hizi cwaoni vibaraka wa magamba wakina Faizfox ,Kamura,MS,Mwita25 n.k
 
Ninaendelea kuelewa siasa si uadui na si kweli kuwa ndani ya ccm haitatoka kauli nzuri itakayo tufaa, pamoja na maelezo hayo marefu, nimepata point 2 za kuanzia.

1. Maelezo ya Malisa lazima yaponde ccm kidogo ili awe kivutio kwa wakazi wa Arusha waliochoka na siasa za ccm.
2.Lazima afanye hivyo ili kuivuruga kambi ya Lowasa.

La muhimu kwangu ni pale malisa naye kukata malipo ya dowans, akitaka vijana wote bila kujali itikadi za wapinge.naona gamba linamwachia dogo taratibu.
 
CCM isiyo na itikadi na msimamo kwenye mambo ya msingi ni sawa na gulio ama soko linalokusanya watu kwa ajili ya kujitwalia madaraka...
 
Tuungane katika lipi hasa. Malisa kmwe huwezi kulisukuma kari la CCM Ufisadi ungali umelipanda ndani.

Ni kweli Vijana tumejiandaa kuliko kawaida katika hili la kuwapa somo mafisadi, lakini pamoja na kwamba baadhi yenu ni wa kuweza kufikirika kama vile Bashe, Malisa ... Shy-Rose Bhanji ...

... lakini kwa sasa hakuna ushirikiano wa aina yoyote mpaka mtakapoamka usingizini, kuona mwanga na kuvuka kuja CDM ndipo tutakapoungana kupigania wale wanaolazwahoi na CCM hivi leo hii. Tafakari juu ya hilo kabla hakujachelewa sana.
Naungana na we mkuu! Ahamie airtel i,e cdm ajisikie huru! Huko anaogopa kuwataja hao watakaowajibika wakati wanafahamika
.
 
Back
Top Bottom