Benki zipi wanakubali dhamana ya hati ya nyumba kwa ajili ya mkopo?

Nadhani hamna bank isiyohitaji mali isiyo hamishika kwa wachukuaji mikopo mikubwa
 
Nafikiri lazima kwanza uwe na biashara yenye mzunguko wa pesa kiasi flani ndani ya miaka kadhaa (Cashflow) pia karatasi zenye kuonyesha uhalali wa biashara yako kama usajiri (Brela), TIN, leseni nk
 
Kiutaratibu benki hawaangalii dhamana kama kigezo kikuu cha kutoa mkopo, cha kwanza wanaangalia mzunguko wa hela yako kama utaweza kurudisha hela yao ambapo mara nyingi ni biashara yako ila dhamana ni kama nyongeza tu iwapo kama ukishindwa kufanya marejesho hiyo dhamana ndo irudishe hela yao waliyokukopesha wakiiuza
 
Naomba wenye kufahamu mnisaidie. Ni benki zipi nikiwa na hati ya nyumba nitapata mkopo? Nilikwenda NMB hawakunisaidia. Natanguliza shukhrani
NMB,CRDB tena kwenye Kilimo wanakopesha riba ya 9% mda wa kulipa unakubaliana na Benki.
 
NMB wananyanyasa watumishi kupitia mikopo yao riba kubwa mnoooooooo
 
Nyumba peke yake haifanyi upate mkopo, ni lazima uwe na cash flow ya kueleweka
 
Back
Top Bottom