Invisible
JF Admin
- Feb 26, 2006
- 16,285
- 8,363
Wakuu,
Nimefanya kufuatilia kwa karibu kukua kwa sekta ya biashara ya mabenki kwa Tanzania.
Binafsi nilifurahishwa na kasi ya watanzania kuweka fedha zao benki na kujitahidi kwa kiwango kikubwa kuchukua mikopo kwa wingi.
Kuna mengi niliyofurahishwa nayo lakini mengi sana yamenikera. Mojawapo ya yaliyonikera ni jinsi benki hizi zilivyojengwa kwa viwango duni na huku BoT ikifanya ukaguzi na kuzikubalia benki hizi kuendelea na kazi. Teller counters zikiwa zimejengwa kienyeji, na nyingine zikiwa na teller counters nyingi tu lakini watendaji wawili au mmoja.
Ningependa tujaribu kujadili na kugusia vipengele kadhaa ikiwa ni pamoja na:
Natumaini tutatoana tongotongo katika mengi na huenda ukawa mwanzo wa watanzania kujua utendaji wa benki zetu na namna gani aidha wanaweza kufungua akaunti wakiwa ndani na nje ya nchi na usalama wa fedha zao utakuwaje

- Uwingi wa benki na faida na hasara zake.
- Mikopo itolewayo na benki hizi na urahisi/ugumu wa kuipata
- Usalama wa benki zenyewe kwa viwango vinavyokubalika
- Wizi unaofanywa na baadhi ya benki ambao watanzania hawajaushtukia.