Benki zapewa siku tatu kurejesha vitakasa mikono katika ATMs

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesisitiza miongozo yote iliyotolewa kwa umma kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya CORONA (COVID - 19), izingatiwe.

Mkurugenzi wa Idara ya Kinga wa Wizara hiyo, Dkt. Leonard Subi amesema Tanzania ni salama hata hivyo kwa kuwa bado kuna tishio la maambukizi ya Virusi hivyo duniani, ni muhimu kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga.

Dkt. Subi amesema hayo leo alipohojiwa na moja ya chombo Cha habari jijini Dodoma ni hatua gani Tanzania inaendelea kuzichukua kuhakikisha jamii inakingwa dhidi ya wimbi jipya la maambukizi ya COVID - 19.

"Tanzania tupo salama lakini tunatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi hayo ambayo kwa takriban mwaka na nusu sasa bado yanaikabili dunia.

"Wizara kazi yetu ni kuendelea kihimiza wananchi kujikinga dhidi ya COVID - 19, tuendelee kuchukua tahadhari, tuliona katika wimbi la kwanza 2020 wananchi waliitika wito wa kunawa mikono, kuvaa barakoa, kukaa umbali, kufanya mazoezi, lishe bora na masuala mengineyo," amesema.

Ameongeza "Tunataka kusisitiza kinachotokea Afrika maambukizi yanaongezeka na baadhi ya Wakuu wa Nchi wanatoa matamko kama tulivyomsikia Rais wa Uganda na sisi Tanzania tumekuwa na mwingiliano na uhusiano mwema na nchi jirani.

"Watanzania kinga ni bora kuliko tiba tusije tukasubiri kuingia kwenye mitungi ya oksijeni, tuendelee kujikinga. Hali ni shwari hata Rais Samia Suluhu Hassan anachukua tahadhari kujikinga na maambukizi akikutana na watu mbalimbali," amesema.

Amesisitiza "Mashuleni, vituo vya afya tuliweka vifaa kwa kunawa kwa maji safi tiririka, tunawe mikono.

Akitolea mfano wa Ma-benki kwenye 'ATM' waliweka vipukusi 'sanitizers', Ila Kwenye ATMs sasa hivi havipo na watu wanashika wanabonyeza bonyeza pale inaweza kuwa chanzo cha maambukizi.Alizitaka benki zote wahakikishe wanarejesha vitakasa mikono na kuwapa siku tatu.

"Hatua tulizopiga tusije tukarudi tulipotoka, sisi Serikali tunaendelea kufuatilia kwenye mikusanyiko, mabasi, ndege wachukue tahadhari.

Amesema Serikali imeimarisha hatua za ufuatiliaji kwenye maeneo ya mipaka, viwanja vya ndege watu wanapimwa hali zao za afya.

"Tunafahamu kuna tishio kubwa la anuwai mpya (aina mpya ya kirusi cha CORONA) duniani, kuna cha India, Uingereza, Afrika Kusini na Brazil ambavyo vimeendelea kugharimu maisha ya watu.

"Tunashirikiana na Mamlaka za mikoa, Serikali za Mitaa kuhakikisha tunaendelea kuwafikia wananchi," amesema.

Dk. Subi pia ametoa rai kwa vyombo vya habari kuendelea kuelimisha jamii na kuihamaisha kujikinga dhidi ya maradhi hayo.

"Tunaomba vyombo vya habari mtumie muda wenu kidogo hata mara moja au mbili kwa siku kuwakumbusha wananchi kuchukua tahadhari juu ya COVID - 19.

"Suala la mapambano dhidi ya magonjwa si la hiyari, tuna maafisa afya pia, Watanzania suala la afya ni la muhimu na la msingi kwa Maendeleo ya Taifa tukicheza tutarudi nyuma, kila mmoja atimize wajibu wake.

"Kwenye familia ndoo za kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni ziwepo, bebeni vipukusi na katika maeneo ya mikusanyiko tunashauri barakoa zivaliwe kwa kuzingatia mwongozo tuliotoa na kwenye nyumba, magari kuwe na mzunguko wa hewa, tujikinge," ametoa rai Dk. Subi.

Michuzi Blog
 
Nyie madalali uchwara wa corona hebu mtupishe!

Hivi kwani huwa mnalipwa shilingi ngapi kuwajaza watu hofu na kushadadia hayo machanjo feki?

Hiyo corona kama kweli ingekuwa ni gonjwa halisi, basi tungekuwa tunaona huku mitaani watu wakijifia na kuugua.

Nipo kariakoo hapa, watu wanadunda tu. Hakuna cha barakoa wala bibi yake barakoa.

Kwendeni huko na makorona yenu ya kufikirika.

WE ARE FINE AND SAFE.
 
Kwa hio mpaka sasa hivi kweli hop njia ya kunawa mikono kwa sabuni na maji au alcohol ndio njia moja wapo sahihi ya kujikinga na corona?
 
Nyie madalali uchwara wa corona hebu mtupishe!

Hivi kwani huwa mnalipwa shilingi ngapi kuwajaza watu hofu na kushadadia hayo machanjo feki?

Hiyo corona kama kweli ingekuwa ni gonjwa halisi, basi tungekuwa tunaona huku mitaani watu wakijifia na kuugua.

Nipo kariakoo hapa, watu wanadunda tu. Hakuna cha barakoa wala bibi yake barakoa.

Kwendeni huko na makorona yenu ya kufikirika.

WE ARE FINE AND SAFE.
Don't be so selfish! Ni kama kusema hujawahi kutumia chandarua, dawa ya malaria au kuugua malaria, kwa hiyo hakuna malaria au hujawahi kuugua matende na ugongwa wa matende haupo. Kama hujaathiriwa na ugonjwa huu usidhani hata wengine hawajaathiriwa pia. Kuna watu wamepoteza wazazi, ndugu na marafiki na bado wako kwenye majonzi na wakisikia hivyo ni kama unawachekelea. Labda kutaka kujua kama ugonjwa upo au la jifanye haupo na usichue tahadhari yoyote na utakapougua ndipo utakapopata fundisho. Lakini pia kwa kufanya hivyo, utakuwa umehatarisha maisha ya wengine kwa kuwa obstinate. Haiwezekani nchi zote ambazo zina idadi kubwa ya wagonjwa na vifo vinavyotokana na corona waseme uwongo na haiwezekani pia nchi zinazotuzunguka kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa na vifo waseme uwongo na wewe tu ndiyo uwe unasema ukweli kwa sababu haujaugua. Labda unaongea hivyo kwa sababu ya 'ignorance' au familia au ndugu zako hawajaathiriwa na ugonjwa huu.
 
Dalali Kojoa ukalale
 
Mkuu kwani hujui mtu akifa anazaliwa tena ila hawezi kuwa na kumbukumbu wala kuwa kwenye ukoo wenu kwahiyo usiwe na hofu na kifo
 
Dalali Kojoa ukalale
Komaa hivyo lakini usihatarishe maisha ya wengine. Huwezi kutumia mfano wako halafu u'generalise' kwa wote, eti kwa sababu hujaugua malaria/corona, kwa hiyo hakuna malaria/corona. Logic gani hii?
 
Don't be so selfish! Ni kama kusema hujawahi kutumia chandarua, dawa ya malaria au kuugua malaria, kwa hiyo hakuna malaria au hujawahi kuugua matende na ugongwa wa matende haupo. Kama hujaathiriwa na ugonjwa huu usidhani hata wengine hawajaathiriwa pia. Kuna watu wamepoteza wazazi, ndugu na marafiki na bado wako kwenye majonzi na wakisikia hivyo ni kama unawachekelea. Labda kutaka kujua kama ugonjwa upo au la jifanye haupo na usichue tahadhari yoyote na utakapougua ndipo utakapopata fundisho. Lakini pia kwa kufanya hivyo, utakuwa umehatarisha maisha ya wengine kwa kuwa obstinate. Haiwezekani nchi zote ambazo zina idadi kubwa ya wagonjwa na vifo vinavyotokana na corona waseme uwongo na haiwezekani pia nchi zinazotuzunguka kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa na vifo waseme uwongo na wewe tu ndiyo uwe unasema ukweli kwa sababu haujaugua. Labda unaongea hivyo kwa sababu ya 'ignorance' au familia au ndugu zako hawajaathiriwa na ugonjwa huu.
Dalali
 
Acha umbea
 
Hivi nyie msioamini kwenye Corona kwanini msikae kimya tu. Kwanini roho zinawauma sana mtu mwingine akiamini upo huu ugonjwa au mtu mwingine akiwataka watu wachukue tahadhari? Si mpotezee tu mkae kimya, kwanini mnaita watu madalali, wamewadalalia nini?

Kama unaamini duniani hakuna korona piga kimya tu au kama unaamini korona ipo ila ni kwa ajili ya mataifa mengine si Tanzania piga kimya tu na uendelee kupuyanga kwani ukienda kwenye ATM ukakuta sanitaiza umelazimishwa kuitumia? Si utoe hela zako kisha ujiondokee tu bila kutumia, kwanin roho ikuume wengine wakitaka kutumia.
 
Don't be so selfish! Ni kama kusema hujawahi kutumia chandarua, dawa ya malaria au kuugua malaria, kwa hiyo hakuna malaria au hujawahi kuugua matende na ugongwa wa matende haupo.
Acha blah blah wewe dalali wa makorona.

Mbona mme wako hajafa?
 
Back
Top Bottom