Benki za Zimbabwe zimeanza kutoa noti na sarafu mpya

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Messages
318
Points
1,000

Nyendo

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2017
318 1,000
HARARE,ZIMBABWE

BENKI za Zimbabwe zimeanza kutoa noti na sarafu mpya zilizotolewa na benki kuu ya nchi hiyo RBZ ili kupunguza ukosefu wa sasa wa pesa taslim.

Watu walitarajia kuanza kupata pesa hizo kuanzia jumatatu kutokana na tangazo la awali la benki kuu, lakini noti hizo hazikupatikana kutokana na benki kutumia siku hiyo nzima kukusanya pesa hizo kutoka benki kuu.

Hata hivyo baadhi ya wateja wamelalamika kuwa kiwango cha chini cha kuchukua pesa katika benki yake ni dola 50 kwa wiki, ingawa kiwango cha juu zaidi cha kuchukua pesa ni dola 300. Mhudumu mmoja wa benki ya biashara amesema, wanatarajia kuongeza kiwango cha kuchukua pesa, kama wakiendelea kupata pesa za kutosha kutoka benki kuu.
 

Forum statistics

Threads 1,379,335
Members 525,390
Posts 33,743,508
Top