Benki za Biashara Tanzania zinaogelea kwenye faida. Je, nini kimefanyika awamu ya sita?

DidYouKnow

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
984
1,000
Wachumi mtusaidie hili, Hivi mabenki yetu ya biashara kupata faida ya TZS 471B kwa miezi tisa tu,Wakati huko nyuma yalipata TZS 286B kwa mwaka ina maana gani kwa Uchumi wa nchi yetu?Je! ni Vyuma kulegea?

Mtakumbuka kwa mara ya mwisho hapa Tanzania mabenki yetu ya biashara kurekodi faida ya kihistoria ilikuwa ni mwaka 2015 pale ambapo yalirekodi Jumla ya faida ya TZS 438BL hii ni baada ya kulipa kodi ya Serikali.

Mtakumbuka pia kwamiaka mitano mfululizo iliyopita mabenki haya hayajaweza kabisa kuivunja rekodi hii zaidi sana wakati flani faida zao zilishuka mpaka kufikia Jumla ya Tshs 286BL mwaka 2017 hii ilikuwa ni Jumla ya faida kwa mabenki yote ya biashara nchini kwa mwaka huo.

Leo chini ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan tena kwa kipindi kifupi cha Jan -Sept mabenki hayo hayo kwenye nchi hii hii yameivunja ile rekodi iliyowekwa na Dk Jakaya Kikwete kwa faida ya Tshs 438BL kwa zaidi ya 7.53% na hii ni kwa robo tatu tu ya mwaka.

Kwalugha rahisi miezi michache ya Rais Samia mabenki yamevunja rekodi ya faida ya tangu uhuru ambayo ilivunjwa kwa mara ya mwisho na Mzee Jakaya Kikwete kwa thamani ya faida ya Tshs 438BL leo Samia ameivunja kwa thamani ya faida ya Tshs 471BL na hii ni kwa miezi tu, tunaposema Rais Samia hakamatiki tunamaa hii.

Kwa tathimini iliyofanywa kwa mabenki 13 ya kibiashara nchini kati ya 14 yanayotengeneza faida kila mwaka ni NMB na CRDB tu ndio wamebeba 80% ya faida yote ya Tshs 471BL kwa kuwa na faida ya Jumla ya Tshs 379BL,Wakati huohuo NPL yaani Non Performing Loans au mikopo " Chechefu " ikishuka na kufikia chini ya 35.7% kwa baadhi ya mabank huku thamani yake ikupungua kutoka tshs 395.69BL mwaka 2020 hadi tshs 392.4BL kwa lugha ya kibenki (arrears -zimepungua )

Sababu kubwa yaongezeko hili kubwa la Faida kwa mabenki yetu ya biashara nchini zinatajwa kuwa ni Sera nzuri za ki-Uchumi za Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na miongozo mathubuti toka BOT kama mlezi wa mabenki haya hasa kwenye kupunguza vipimo vya risk kwenye utoaji mikopo ikiwa ni pamoja na kutoa fedha maalumu "Stimulating fund " kiasi cha Tshs 1trl ili kuziongezea Ukwasi baadhi ya Benki zetu za biashara zilizokaukiwa hii imesaidia sana kuinua sekta ya fedha ambayo utoaji mikopo kwa mujibu wa BOT umepanda toka 2.5% 2020 hadi 9.8% hivi sasa,

Kwamsiofahamu zaidi ya 80% ya faida yote ya mabenki ya biashara inabebwa na mikopo na Ukiona mabenki yanapata faida sana maana yake yamekopesha sana na wateja wao wameweza kurejesha mikopo yao ( EMI) kwa wakati na ndio tunasema NPL imeshuka au mikopo isiyolipika|chechefu imepungua na ndio sababu faida imepanda na kwa maana hiyo biashara mtaani inakua au inakwenda vizuri ndio maana mteja X aliyekopa katika benki Y ameweza kuchukua mkopo Benki na kununua bidhaa na kisha kuziuza na mwisho kupeleka marejesho ya Benki kwa wakati yaani ( Purchasing Power-Uwezo wa kununua kwa Watanzania ) umeongezeka , Hongera Sana Rais Samia hakika unaupiga mwingi,


Hadi Kimei mwenyewe anasema mabenki yanapata faida kubwa, riba ipunguzwe.

 

htmm

Member
Jul 14, 2021
22
45
Kumbe Benki zetu bado ndogo sana na hii inawezekana inatokana na udogo wa uchumi wetu hiyo faida combined ni faida ya Equity bank mwaka jana. Hii ni dalili moja wapo ya ukubwa wa uchumi wa Kenya kwa Tanzania.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 

AGGGOT TZ

JF-Expert Member
Sep 14, 2018
910
500
Faida yanapata kutokana na kutupiga riba kubwa
Ne
Kumbe Benki zetu bado ndogo sana na hii inawezekana inatokana na udogo wa uchumi wetu hiyo faida combined ni faida ya Equity bank mwaka jana. Hii ni dalili moja wapo ya ukubwa wa uchumi wa Kenya kwa Tanzania.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
Sekta ya Bank Tanzania iko vizuri tatizo liko kwa walaji,

Watanzania wengi bado hawatumii Bank

Tutafika madamu mama yupo
 

VUGU-VUGU

JF-Expert Member
Feb 24, 2017
723
1,000
Politicization of reports inapotosha hali halisi...katika hiyo faida ya 471 Billion NMB na CRDB ni 80% na benki ya tatu ni kama 40 something billion.

Hivyo ina maana zaidi ya 50% ya mabenki nchini yanaogelea hasara na yapo hatarini kufungwa.lazima tujue hili ili tuyasaidie mabenki yajikwamue
Unaelewa upotoshaji?
 

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
1,669
2,000
Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameipongeza ATCL kwa kupanua biashara ya usafiri na usafirishaji ya anga, hasa baada ya ATCL kuongeza safari zake za kibiashara kwa karibu mara tatu.

Rais Samia ameipongeza zaidi ATCL kwa kurejesha Safari za Kenya Nairobi tena kwa gharama ndogo ya KSh37,525 au $334 sawa na TZS 770, Two ways.

Lazima tufahanu kuwa mwendo huu wa kasi wa ATCL ni kabla ya ujio wa ndege mpya tano za kisasa zinazotarajiwa kuingia nchini ndani ya kipindi kifupi kijacho, hakika hakuna kama Rais Samia.Natangaza rasmi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan,
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom