Benki za Biashara Tanzania zinaogelea kwenye faida. Je, nini kimefanyika awamu ya sita?

Ni mwendo wa faida tuu👇

Screenshot_20220131-112006.png

Screenshot_20220129-203859.png
 
Hakuna miujuzi kwenye kutengeneza faida.

Kwa miaka ya karibuni benk zimejitahidi sana kuboresha huduma na miundombinu yao.

Ile dhana ya financial inclusion imetekelezeka almost 90% kwa sasa. Huku ndipo benk zimejichotea sana fedha.

Kuwepo kwa mawakala,huduma za benk mkononi kuimarika kumefanya watumiaji wapate urahisi.

Kuongezeka kwa gharama za miamala na wingi wa wateja.

Namna nzuri ya utoaji mikopo na ufuatiliaji katika kulipa.

Lakini pia uminyaji wa gharama za endeshaji hizi benki umekuwa mkubwa.

Hii ni pamoja na mishahara duni ya wafanyakazi. Huku uzalishaji ukiwa mkubwa.

Kwa kifupi serikali inamchango mkubwa sana katika kuzifanya hizi benk zifanye vizuri. Janja janja imepungua sana.

Pongezi pia kwa ma CEOs wanapambana kuacha alama.
 
Hebu nyie wajuvi wa JF naomba kuuliza, watumishi wenye mikopo kwenye taasisi za kifedha kwa mwezi januari wameshuhudia mabadiliko kwenye makato yao..yaani mfano unakatwa elfu kumi ili kupunguza deni benki lakini ki mahesabu inaonekana umekatwa elfu 20 bila kuathiri take home ya mtu, je hiyo ni makusudi ya serikali au ni makosa ya ki mfumo?
 
Makato yapo kama awali, hayajabadilika! unless kama ulikuwa na arears!
 
Wachumi mtusaidie hili, Hivi mabenki yetu ya biashara kupata faida ya TZS 471B kwa miezi tisa tu,Wakati huko nyuma yalipata TZS 286B kwa mwaka ina maana gani kwa Uchumi wa nchi yetu?Je! ni Vyuma kulegea?

Mtakumbuka kwa mara ya mwisho hapa Tanzania mabenki yetu ya biashara kurekodi faida ya kihistoria ilikuwa ni mwaka 2015 pale ambapo yalirekodi Jumla ya faida ya TZS 438BL hii ni baada ya kulipa kodi ya Serikali.

Mtakumbuka pia kwamiaka mitano mfululizo iliyopita mabenki haya hayajaweza kabisa kuivunja rekodi hii zaidi sana wakati flani faida zao zilishuka mpaka kufikia Jumla ya Tshs 286BL mwaka 2017 hii ilikuwa ni Jumla ya faida kwa mabenki yote ya biashara nchini kwa mwaka huo.

Leo chini ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan tena kwa kipindi kifupi cha Jan -Sept mabenki hayo hayo kwenye nchi hii hii yameivunja ile rekodi iliyowekwa na Dk Jakaya Kikwete kwa faida ya Tshs 438BL kwa zaidi ya 7.53% na hii ni kwa robo tatu tu ya mwaka.

Kwalugha rahisi miezi michache ya Rais Samia mabenki yamevunja rekodi ya faida ya tangu uhuru ambayo ilivunjwa kwa mara ya mwisho na Mzee Jakaya Kikwete kwa thamani ya faida ya Tshs 438BL leo Samia ameivunja kwa thamani ya faida ya Tshs 471BL na hii ni kwa miezi tu, tunaposema Rais Samia hakamatiki tunamaa hii.

Kwa tathimini iliyofanywa kwa mabenki 13 ya kibiashara nchini kati ya 14 yanayotengeneza faida kila mwaka ni NMB na CRDB tu ndio wamebeba 80% ya faida yote ya Tshs 471BL kwa kuwa na faida ya Jumla ya Tshs 379BL,Wakati huohuo NPL yaani Non Performing Loans au mikopo " Chechefu " ikishuka na kufikia chini ya 35.7% kwa baadhi ya mabank huku thamani yake ikupungua kutoka tshs 395.69BL mwaka 2020 hadi tshs 392.4BL kwa lugha ya kibenki (arrears -zimepungua )

Sababu kubwa yaongezeko hili kubwa la Faida kwa mabenki yetu ya biashara nchini zinatajwa kuwa ni Sera nzuri za ki-Uchumi za Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na miongozo mathubuti toka BOT kama mlezi wa mabenki haya hasa kwenye kupunguza vipimo vya risk kwenye utoaji mikopo ikiwa ni pamoja na kutoa fedha maalumu "Stimulating fund " kiasi cha Tshs 1trl ili kuziongezea Ukwasi baadhi ya Benki zetu za biashara zilizokaukiwa hii imesaidia sana kuinua sekta ya fedha ambayo utoaji mikopo kwa mujibu wa BOT umepanda toka 2.5% 2020 hadi 9.8% hivi sasa,

Kwamsiofahamu zaidi ya 80% ya faida yote ya mabenki ya biashara inabebwa na mikopo na Ukiona mabenki yanapata faida sana maana yake yamekopesha sana na wateja wao wameweza kurejesha mikopo yao ( EMI) kwa wakati na ndio tunasema NPL imeshuka au mikopo isiyolipika|chechefu imepungua na ndio sababu faida imepanda na kwa maana hiyo biashara mtaani inakua au inakwenda vizuri ndio maana mteja X aliyekopa katika benki Y ameweza kuchukua mkopo Benki na kununua bidhaa na kisha kuziuza na mwisho kupeleka marejesho ya Benki kwa wakati yaani (Purchasing Power-Uwezo wa kununua kwa Watanzania) umeongezeka, Hongera Sana Rais Samia hakika unaupiga mwingi.

Kweli pesa ipo kwa sasa, Tuchape kazi kwa bidii,
 
Mama anaupiga mwingi kwelikweli
 
Back
Top Bottom