Benki ya Wanawake yapata Mkurugenzi mpya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,492
9,263

pic+benki+ya+wanawake.jpg



Kwa ufupi
  • Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Beng’i Issa, imeeleza kuwa kabla ya kujiunga na TWB, Justine alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Ushirikiano na Usambazaji wa Benki ya Afrika,(BankABC) Mkoa wa Mara.
Dar es Salaam. Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Wanawake Tanzania,(TWB) imemtangaza Japhet Justine kuwa Mkurugenzi mpya wa benki hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Beng’i Issa, imeeleza kuwa kabla ya kujiunga na TWB, Justine alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Ushirikiano na Usambazaji wa Benki ya Afrika,(BankABC) Mkoa wa Mara.

“Justine ana ujuzi wa hali ya juu katika masuala ya usimamizi, biashara na wa huduma za kibenki alioupata katika maeneo mbalimbali aliyofanya kazi ikiwamo hapa nchini na Kusini mwa Jangwa la Sahara, Rwanda, Botswana, Zambia, Mozambique na Zimbabwe” imesema taarifa hiyo ya Bodi.

Japhet amepata shahada yake ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Biashara cha Stellenbosch, Cape Town, Afrika Kusini.

Awali, Mkurugenzi wa TWB, alikuwa Margreth Chacha.


By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers
 
Kwanini wamemtoa ke na kumuweka me kwenye bank ya kina ke
 
Ke wanapenda sana ligi
Sure! Wanawake wanapewa mikopo wafanyie biashara wao wanaenda kununulia mawigi, mikoba, madera na mikorogo.
Elimu ya ujasirilia mali inapaswa kutolewa kwanza kabla hawa wanawake hawajachukua mikopo...
 
Back
Top Bottom