Benki ya Posta!

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,700
Heshima wakuu! Naomba msaada kwa yeyote anayepata huduma za kibenki na benki ya posta, je huduma zao ni nzuri? Maana nimechoshwa na foleni za nmb.
 
Binafsi ni mteja wa bank ya posta na nina akaunti bank ya posta. Ukweli ni nzuri na haina foleni hawana longo longo, titizo lipo kwenye mikopo mkopo ukiomba hadi kuupata mwezi mzima upite ndo uupate wakati bank nyingine mfano crdb ukimaliza taratibu zote leo keshokutwa mkopo wako unakuta umewekewa pesa yako.
 
benki ya hovyo
1. Very poor customercare
2. Ukifungua akaunti tegemea kupata atm card baada ya miezi sita
3.mkopo ni hadi upitishe mshara mmoja kwao
4.uzuri wao hawana foleni ndeeeeeeeeefu km nmb na crdb
5.hawapo mikoa yote na baadhi ya mikoa waliopo hawana ATM mashine so ukisafiri mikoani cha kufanya ni kuchek kwanza kama atm ipo ili uchukue mzigo mapema. Mkoa mmoja wapo wenye tawi bila atm ni Iringa
 
Hii ndiyo bank ya ajabu kuliko bank nyingine kwa sababu:-

  1. Mtandao wake ni mdogo yaani kimatawi, mfano D'Salaam wapo Kariakoo, Posta yapo matawi maawili na Mwenge. Arusha ni Posta Meru na tawi lingine karibu na Clocktower. Hawana ATM za uhakika na kama zipo speed yake ni slow sana.
  2. Huduma duni kuanzia mikopo mpaka ufunguaji na upatikanaji wa ATM zao.
Siyo bank ya kufungua akaunti heri ubaki huko huko NMB wana NMB Mobile ambayo ni simple kuitumia kwa kila mtu. ATM zake zina speed na nyingi kiasi. Vumilia foleni ya mwisho wa mwezi au kafungue CRDB lakini usiende NBC nao ni wale wale.
 
nadhani kwa bongo, benki inayojitahidi angalau ni CRDB pekee, zingine ni kizunguzungu ndugu yangu
 
Heshima wakuu! Naomba msaada kwa yeyote anayepata huduma za kibenki na benki ya posta, je huduma zao ni nzuri? Maana nimechoshwa na foleni za nmb.

Baki NMB, hii si benki, ni mfano wa benki!!
Nilikwisha tupa kadi yao kitambo!!!
 
tulia nmb au fungu a/c nyingine mfano crdb..benki ya posta ipo ipo tu,usijiunge nao kabisa!.
 
Asanteni kwa ushauri, kufungua akaunti benki ya posta "no", nitavumilia nmb au crdb!
 
Baki NMB, hii si benki, ni mfano wa benki!!
Nilikwisha tupa kadi yao kitambo!!!
Ulifanya kosa, kwa sasa siyo bank mbaya tatizo lake kuelemewa na wateja wengi kuliko uwezo wake ambao wengi hawaendi banki zaidi ya mara mbili hususan mwisho wa mwezi.
 
Mi naona haya ni mapungufu ya benki hii.
1.Poor customer care hasa sehemu za maulizo
2.ucheleweshaji wa atm card tena ni kero kubwa kwa walio wengi
3.sio wabunifu na hata baadhi ya vihuduma wanavyoiga wanashindwa kuviendesha kwa ufanisi
Kiukweli kama mahitaji yako ya kibenk ni ya kawaida kuweka na kutoa pesa utapa unafuu kwa haya
1. huku foleni sio tatizo
2 makato ktk ac sio mengi yanaridhisha
4.matumizi ya atm za umoja switch ambazo nawe ni shahidi kwa wingi wake
 
Hivi nani Meneja Mkuu wa benki Ya Posta? Yule mzee Kihwele alishastaafu au bado yupo?
 
Heshima wakuu! Naomba msaada kwa yeyote anayepata huduma za kibenki na benki ya posta, je huduma zao ni nzuri? Maana nimechoshwa na foleni za nmb.

Nilijaribu kutoa pesa pale Arusha kwa ATM yao, niliingiza kadi mara 3 na kila saa inasema "error", amount niliyokuwa nachukua ni 150,000 kutoka kwenye VISA Card yangu! Nilingia ndani na risiti za kukosa hela nikaambiwa sijakatwa hela, few days later nikiwa safarini (nje ya nchi) nikagundua kwamba akaunti yangu imekuwa deducted (from same ATM)!! What i did niliporudi Arusha after few months nikaenda tena pale na risiti zao pamoja na bank statement yangu inayoonyesha deductions....HAWAKUWA COOPERATIVE, Mwishowe nikaona niaachane nao, since that day nimejaribu kuitafiti nikagundua kuwa NI BENKI YA KIJINGA!! Usipoteze muda wako kufungua akaunti pale....huduma zao ni mbaya na hawana wataalamu! Hata kukiwa hakuna foleni bado wapo too slow, bora huko huko NMB!!
 
benki ya hovyo
1. Very poor customercare
2. Ukifungua akaunti tegemea kupata atm card baada ya miezi sita
3.mkopo ni hadi upitishe mshara mmoja kwao
4.uzuri wao hawana foleni ndeeeeeeeeefu km nmb na crdb
5.hawapo mikoa yote na baadhi ya mikoa waliopo hawana ATM mashine so ukisafiri mikoani cha kufanya ni kuchek kwanza kama atm ipo ili uchukue mzigo mapema. Mkoa mmoja wapo wenye tawi bila atm ni Iringa

Of course hawana foleni ndefu kwa sababu hawana wateja. Na hawana wateja kwa sababu ulizozitaja.
 
vipi kuhusu Barclays na Stanbic?

Foleni sio tatizo na ATM sio tatizo sana (Stanbic), mikopo faster labda issue interest rates, tatizo labda ni makato ya mwezi na kwa huduma zao kidogo ni juu zaidi ya bank nyingine!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom