Benki ya Posta yapata mabilioni ya faida: Mkapa tupe sababu za kubinafsisha NBC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Benki ya Posta yapata mabilioni ya faida: Mkapa tupe sababu za kubinafsisha NBC

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Synthesizer, Apr 25, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Benki ya Posta (TPB) inayomilikiwa na serikali na iliyopo nchini ya uongozi wa wazalendo, imeripoti kupata mabilioni ya faida (3.8bn/-, ongezeko la asilimia 338). Benki hiyo ilikuwa ndogo sana wakati Mkapa ameshika bango la kubinafsisha NBC hadi kuwatukana wabunge waliokuwa wakipinga suala hilo. TPB imekua taratibu chini ya uongozi wa kizalendo hadi kuwa na rekodi iliyopo.

  NBC ilikuwa moja wapo ya taasisi za serikali zenye ufanisi sana na kuweza kufikisha huduma karibu sana kwa wananchi, katika maeneo fulani hadi ngazi ya kata. Matawi mengi ya NBC yaliyokuwa karibu na wananchi yalifungwa baada ya NBC kubinafsishwa.NBC ilitoa riba kubwa kwa wateja iliyokuwa juu ya kiwango cha inflation, na haikuwa ikitoza "bank fees". Hili lilionekana kikwazo kikubwa kwa kampuni zilizotaka kuwekeza benki nchini, ambazo zinatoza ada (bank fees) kila uchukuapo fedha na pia kutoa riba ndogo sana iliyo chini ya kiwango cha inflation. Wawekezaji walikataa kuanzisha bank nchini katika mazingira haya ya kuwapo kwa NBC kwa kuwa wasingepata wateja, na wakamshawishi Mkapa aibinafsishe NBC kwanza.

  Wabunge na Nyerere walipinga sana kitendo cha kubinafsisha NBC. Inasemekana kiongozi wa ngazi ya juu nchini alipewa zawadi ya hoteli huko Afrika Kusini baada ya kufanikisha ubinafsishaji wa NBC.

  Original source (with edits): IPP Media
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  wachotaji wameshasikia, maana baada ya kuimaliza NSSF sasa wataisogelea hiyo ili waifilisi
   
 3. bona

  bona JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  usiwe fooled, uendeshaji wa mashirika yasiyoitaji akili kubwa kama benki na bima sio kigezo cha kusema yanafanya vizuri,yana nafasi ya kufanya vizuri zaidi ya apo kwa mfano benki kama nbc na nmb zimekua kwa kasi ya ajabu baada ya kubinafsishwa na serikali bado imeretain hisa kadhaa! mashirika ambayo watanzania tunatakiwa tujivunie kua tunaweza ni kuendesha yale ya technical kama shirika la ndege, reli, uda, machine tools, nyumbu nk na sio mashirika kama benki au bima kwani uendeshaji wake hauitaji ujuzi au akili kubwa!
   
Loading...