Benki ya Posta kwanini risiti za ATM hazioneshi salio? Nina wasiwasi hamtaki kuonesha mmetuibia tozo kiasi gani

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,373
73,975
Nimekwenda kutoa pesa ATM ya Posta, ikatoka risiti ambayo inaonyesha kiasi kilichotolewa lakini salio/ baki (balance) haionyeshwi.

Tangu miaka yote risiti imekuwa inatoka na kuonesha salio/baki/(au kwa kizungu balance). Leo kwa mara ya kwanza salio halikuoneshwa.

Maana yake nini?: Ni kuwa kwa vile wanakata TOZO hawataki uone wamekuibia kiasi gani. Hii siyo sawa. Mwigulu kuna siku utalipa madhambi haya ya kuwaibia Watanzania.

Unashibisha tumbo lako na wanao wako Feza wanasoma, wa walala hoi wanakatwa TOZO za wizi na kukosa mikopo.

Kuna siku utalipa madhambi haya hata ukiwa kaburini.
 
Usirule out ni mapema mno huenda tu kulikuwa na matatizo kwenye mfumo ila kama litaendelea hapo kutakuwa na jambo.
 
Umetafiti na Benki zingine mf CRDB, NMB, EXIM nk kabla ya conclusion?
 
Back
Top Bottom