Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,011
- 144,371
Kwanza kabisa napenda kuwapongeza sana NMB kwa kuleta huduma hii ambapo mfanyakazi anakuwa na uwezo wa kukopa mpaka asilimia 40 ya mshahara wake(take home bila shaka)
Huduma hii ya mkopo ambayo mfanyakazi atalipa mkopo huo kwa kukatwa mshahara wake mara utakapoingia Benki, utawasadia sana wafanyakazi wanaopata dharura na kulazimika kukopa mitaani kwa riba kubwa.
NMB wao wanasema hawatozi riba bali unatozwa asilimia 6 tu ya kiwango cha mkopo unaochukua kama gharama ya ku-process mkopo husika.
UKweli ni kwamba hata kama hiyo 6% ingekuwa ndio riba bado ni ndogo sana ukilinganisha na riba wanazotozwa wafanyakazi huku mitaani ambapo mtu akikopa kwa mfano shilingi 100,000 anatakiwa kurudisha shilingi 120,000 na wengine mpaka 130,000 mwisho wa mwezi akipata mshahara.
Huduma hii itaokoa wafanyakazi wengi ambao wengi huishi kwa kukopa kwani mishahara ni midogo na matatizo ni mengi huku siku 30 za kusubiri mshahara utoke zikiwa ni nyingi mno.
Huduma hii ambayo imeanza kutolewa kuanzia tarehe 13/03/2018 kwa mujibu wa kipeperushi chao, inapatikana kwa kupiga *150*66# then unachagua "mkopo" ambayo ni option number 5.
Mkopo unaingizwa kwenye akaunti yako ya mshahara wa NMB moja kwa moja.
Kwa maelezo zaidi ikiwa ni pamoja na kujua mashariti na vigezo ingia:
www.nmbbank.co.tz.
Huduma hii nasikia hata CRDB nao wanayo.
Ushauri:
Kama NMb wameweza ni wazi hata serikali nayo inaweza kuangalia kuanza utaratibu wa kulipa watumishi nusu mshahara kila ifikapo nusu ya mwezi ili kupunguzia watumishI wake ugumu wa maisha maana sasa hivi hata ukijiongeza ukafanya biashara ili uongezi kipato biashara nazo zimekuwa ni ngumu hivyo unajiongeza lakini bado inakuwa haisadi sana.
Vile vile nawashauri NMB malezo kuhusu mashariti na vigezo vya kupata mkopo yatolewe kwa lugha ya kiswahilI pia ili watu waweze kuelewa vizuri na kwa urahisi zaidi terms za mkopo huu kwani kujua mashariti na vigezo kabla ya kuchukua mkopo ni jambo la muhimu sana.