Benki ya NMB na kampuni ya simu ya Vodacom, huduma yenu ya mobile banking ni mbovu na inakula hela za wateja bure tu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,991
144,326
Huduma hii ya mobile banking inayotolewa kwa ushirikiano baina kampuni hizi mbili kwa kiasi fulani imegeuka kero na zaidi ni huduma inayogharimu hela za wateja bila kujali mteja amepata huduma husika au laa.

Mfano ni pale unapojaribu kuangalia salio la fedha kwenye akaunti yako ya benki kwa kutumia simu ya mkononi au unapotaka kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya benki kwenda Mpesa ambapo mara nyingi huduma inafeli huku mchakato ukiwa ama mwanzoni kabisa,katikati na hata ikiwa katika hatua ya mwisho kabisa ya kusubiru jibu lakini licha ya kutopata huduma uliomba(majibu) hela kwenye akaunti yako ya benki wanakata na pia salio kwenye simu yako pia wanawakata bila kujali umepata huduma ulioombaa au laa.

Hili tatizo limekuwa kwa muda sasa na sioni kama jitihada zinafanyika kulimaliza na hii ni kwasababu haya makampuni yenyewe haya hasara zaidi tu ya kuingiza fedha hata kama hawajakupa huduma unayoihitaji(hawajakamilisha).

Inawezekana hali hii ni kutokana na utaratibu wao wa kusema mashariti na vigezo vinazingatiwa hivyo ukubali lolote litakalotokea hata kama sio jambo sahihi.

Binafsi naona wakati umefikika jambo hili litazapwe upya na taasisi au mamlaka zinazosimamia utendaji kazi wa taasisi hizi(NMB na Vodacom) ili kulinda wateja wa makampuni haya maana tunakamuliwa fedha nyingi sana.

Ni fedha nyingi kwasabbu ukishakatwa hela mfano wakati unahamisha fedha kutoka benki kwenda Mpesa,bado tena unakuja kukatwa hela nyingine kubwa tu wakati unatoa fedha kutoka kwa wakala wa Mpesa hivyo makato haya si madogo na si ya kupuuza hasa kama unafanya muamala wa kuhamisha fedha nyingi kidogo(kuanzia laki moja na kuendelea).

Nashauri serikali kupitia taasisi/mamlaka husika, kuingilia kati na kuzitaka taasisi hizi zikate hela ya mteja pale tu mteja anapokuwa amepata huduma husika na kwa kufanya hivi, ninahaki Benki ya NMB na kampuni ya Voda wataboresha huduma hii ili wasipate hasara kwani kwa sasa hasara anapata mteja na sio wao na huenda hii ni moja ya sababu ya kuwafanya wasishituke.

Nimeongelea Voda kwasababu ndio mtandao naoutumia kupata hii huduma hivyo sijui hali ikoje kwa mitandao mingine ila inawezkana hali ni hii hii.

Inakera sana!!
 
Naunga mkono hoja na kubwa kuliko lote kwanini NMB ukitoa pesa wanakutumia sms kuwa umetoa tu pesa kiasi fulani hawakupi balance ni kama kukulazimisha kutumia mitandao ile ukatwe kwa kuangalia salio tu. Bank nyingi duniani ukitoa au kuingiza unapata kiasi na salio. NMB boresheni hivi vitu vidogo lakini vinakera sana.
 
Ubunifu sifuri;ukamuaji, asilimia mia moja!!
 
Tatizo ni voda sio NMB, yaani wanakukata hela kwa kila hatua unayofanya.
Kwa ufupi voda si rafiki, hakuna menu ya benki yeyote utaingia bila kukatwa hela.
Upande wa kukatwa hela kutoka NMB kwenda MPESA na kisha ukatwe wakati wa kutoa, ni heri utoe kwa wakala wa NMB kwa sababu siku hizi wamesambaa kila sehemu.
 
Yaani mimi mfumo wa kutumia internet kwa shughuli zangu za kifedha hapa Tanzania bado sana. Yaani nimekutana na watu kibao wamepoteza pesa kupitia huo mfumo na wameshindwa ku recover pesa yao! Alaf kutwa wanashinda kupongezana kwa kufikisha target!
 
CRDB na Vodacom ni muungano wa jini na Shetani lengo lao ni kutuumiza wenye vijisenti vya kawaida.
 
Nadhani hiyo ni shida ya Vodacom. Mimi walikuwa wanakata nikahamia Airtel sasa wanakata kwa account tu
 
kama unatumia smartphone download app ya NMB inaitwa NMB klik, huduma zote za mobile banking na zaidi unazipata, app inatumia data kidogo tu,
tena kuangalia salio ilikua bure sijui kama wamebadilisha.

kuwa makini kudownload app halisi kutoka playstore
 
Huduma hii ya mobile banking inayotolewa kwa ushirikiano baina kampuni hizi mbili kwa kiasi fulani imegeuka kero na zaidi ni huduma inayogharimu hela za wateja bila kujali mteja amepata huduma husika au laa.

Mfano ni pale unapojaribu kuangalia salio la fedha kwenye akaunti yako ya benki kwa kutumia simu ya mkononi au unapotaka kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya benki kwenda Mpesa ambapo mara nyingi huduma inafeli huku mchakato ukiwa ama mwanzoni kabisa,katikati na hata ikiwa katika hatua ya mwisho kabisa ya kusubiru jibu lakini licha ya kutopata huduma uliomba(majibu) hela kwenye akaunti yako ya benki wanakata na pia salio kwenye simu yako pia wanawakata bila kujali umepata huduma ulioombaa au laa.

Hili tatizo limekuwa kwa muda sasa na sioni kama jitihada zinafanyika kulimaliza na hii ni kwasababu haya makampuni yenyewe haya hasara zaidi tu ya kuingiza fedha hata kama hawajakupa huduma unayoihitaji(hawajakamilisha).

Inawezekana hali hii ni kutokana na utaratibu wao wa kusema mashariti na vigezo vinazingatiwa hivyo ukubali lolote litakalotokea hata kama sio jambo sahihi.

Binafsi naona wakati umefikika jambo hili litazapwe upya na taasisi au mamlaka zinazosimamia utendaji kazi wa taasisi hizi(NMB na Vodacom) ili kulinda wateja wa makampuni haya maana tunakamuliwa fedha nyingi sana.

Ni fedha nyingi kwasabbu ukishakatwa hela mfano wakati unahamisha fedha kutoka benki kwenda Mpesa,bado tena unakuja kukatwa hela nyingine kubwa tu wakati unatoa fedha kutoka kwa wakala wa Mpesa hivyo makato haya si madogo na si ya kupuuza hasa kama unafanya muamala wa kuhamisha fedha nyingi kidogo(kuanzia laki moja na kuendelea).

Nashauri serikali kupitia taasisi/mamlaka husika, kuingilia kati na kuzitaka taasisi hizi zikate hela ya mteja pale tu mteja anapokuwa amepata huduma husika na kwa kufanya hivi, ninahaki Benki ya NMB na kampuni ya Voda wataboresha huduma hii ili wasipate hasara kwani kwa sasa hasara anapata mteja na sio wao na huenda hii ni moja ya sababu ya kuwafanya wasishituke.

Nimeongelea Voda kwasababu ndio mtandao naoutumia kupata hii huduma hivyo sijui hali ikoje kwa mitandao mingine ila inawezkana hali ni hii hii.

Inakera sana!!

Yaani upo NMB na unategemea huduma nzuri...ni sawa na kupanda DCM ya Gongo la mboto na kulalamika haina AC.
 
Back
Top Bottom