Mtondoli
Member
- Nov 9, 2021
- 70
- 174
Wadau wenzangu wakilimo hiki kinachoitwa benki ya kilimo naona Kama hakina tija yoyote kwa mkulima halisi,najua mkulima yupo kijijini Lyazumbi, Katonto,Muze,Mtowisa,Chikumbulu huku au Ngulugulu huko Ileje ndani na vijiji vyote vinavyohusika na kilimo hawana taarifa na namna ya kunufaika na benki hii,na ninahisi kuna upigaji mkubwa kupitia benki hii.Na ninahisi wanaonufaika na benki hii sio wakulima halisi huenda kuna wajanja tu wanaojuana na familia zao ndio wanufaika.
Wajitokeze wakulima Mia tu wa vijijini walionufaika na mikopo ya benki hii ninauhakika hakuna, naona hivi ni vitu vinavyochelewesha maendeleo ya jumla ya kilimo naona waifute tu haina faida kwetu.
Wajitokeze wakulima Mia tu wa vijijini walionufaika na mikopo ya benki hii ninauhakika hakuna, naona hivi ni vitu vinavyochelewesha maendeleo ya jumla ya kilimo naona waifute tu haina faida kwetu.