Benki ya kilimo(TAB) na Waziri wa Kilimo vina faida gani?

nyundo2017

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,358
2,000
Ni kwanini ni ngumu sana kupata mkopo kutoka Benki ya Kilimo?

Kwanini ili kukopa yabidi muanzishe kikundi ndiyo mpewe mkopo wakati kila mtu ana mopango yake malengo yake?

Waziri anafaida gani iwapo anaona kabisaaa matawi ya benki ya kilimo yako miji mikubwa yenye lami na vijijini hakuna hata wakala na ametulia tu?

Vikao na semina zimetawala na wahudhuriaji ni ni watumishi na matajiri wetu wenye kilimo cha makaratasi wanalipana posho tu kila kukicha?

Vijana wanaomba mikopo wananyimwa wanaambiwa waungane na ikibidi waanzishe shamba kwanza sasa huo mtaji wanautoa wapi?

Kila kitu kinaanzia kwa mmojammoja baadae ndiyo wanaungana kulingana na juhudi zao na ufanisi pia mtaji ndiyo kikwazo kikubwa.

Kuna haja gani ya kuwa na benki ya kilimo iwapo mkopo wa kilimo hadi upitie PASS then uwalipe nao wakupeleke benki nyingine ambako mkopo utapitia kutoka TAB huu si urasimu!

Mh Rais Samia tukomboe kwa hili kama vipi vunja tu hii benki fedha zikafanye mambo mengine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom