Benki ya Dunia yatoa Dola Milioni 75 kutekeleza mradi utaoleta mapinduzi katika elimu ya ufundi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326

1574762692655.png

Serikali ya Tanzania inatekeleza Mradi unaolenga kuleta mapinduzi katika Elimu ya Ufundi Afrika Mashariki (EASTRIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Akizungumzia mradi huo wakati wa akifungua mkutano wa pili wa Mwaka wa wadau wa Mradi huo kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dk.Leornad Akwilapo amesema benki ya Dunia imetoa Kiasi Dola za kimarekani Milioni 75 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo katika vyuo vinne nchini ambavyo ni Chuo cha Usafirishaji Dar es Salaam (NIT), Taasisi ya Teknolojia ya Dar Es salaam (DIT) kampasi ya Dar es Salaam na Mwanza na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).

"Fedha hizi zinatolewa na Benki ya Dunia ni kwa ajili ya kuvijengea vyuo vya hivyo uwezo ili viweze kutoa wanafunzi wenye ujuzi stahiki wa kuwawezesha kujiajiri ama kuajiriwa na pamoja na kuvijengea vitu vya umahiri" amesema Dkt. Akwilapo.

Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa mradi huo utawezesha kujenga miundombinu bora na kuweka vifaa Pamoja na kuwajengea uwezo wakufunzi.

Aidha, Dkt. Akwilapo amewataka watanzania kufahamu kuwa elimu ya ufundi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi hasa katika uchumi wa viwanda na kwamba vyuo vya ufundi visiwe chaguo la mwisho kwa mtu anayefeli.


1574762669797.png

"Tunawashukuru Benki ya Dunia kwa maana fedha hizo zitatumika katika kuhakikisha wanawajengea uwezo wanafunzi na pindi wanapohitimu inakua rahisi kuajiriwa viwandani na hasa ikizingatiwa Tanzania inaelekea katika uchumi wa viwanda kwa sasa,"

Naye Mratibu wa Mradi huo kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Noel Mbonde amesema vyuo hivyo vinne vimejikita katika masuala ya Teknolojia ya Habari(Tehama),Gesi asilia, Ngozi na masuala ya anga na mradi huo unakwenda kuongeza udahili wa wanafunzi katika fani hizo katika chuo cha NIT pamoja na ununuzi wa ndege ya mafunzo.

Chanzo: Muungwana Blog


 
Si ndo hao mabeberu yaani wakati tunaomba mikopo na msaada wanaitwa bank ya dunia,au wazungu ila wakati wa uzinduzi wanaitwa MABEBERU.
 
Back
Top Bottom