Benki ya dunia yasema ukuaji wa uchumi wa Tanzania utaongezeka 2020 kwa 5.8% na si kwa 7%

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Uchumi wa Tanzania utakuwa kwa asilimia 5.8 mwaka 2020 ikilinganishwa na makadirio ya asilimia 5.6 mwaka huu na ukuaji utaongezeka hadi asilimi 6.1 mwaka 2021, kulingana na ripoti ya benki ya dunia siku ya Jumanne.

Matarajio ya benki ya dunia yapo chini ikilinganishwa na makadirio ya asilimia 7.1 , ikiwa ni mara ya pili mwaka huu kwa makadirio hayo kutofautiana kwa kiwango kikubwa na yale ya serikali kulingana na chombo cha habari cha Reuters.

Benki ya dunia inakadiria kwamba ukuaji wa uchumi wa taifa la Tanzania utakuwa asilimia 5.6 kutoka asilimia 5.4 mwaka 2018.

Serikali ya Rais Magufuli imewekeza mabilioni ya madola katika sekta ya viwanda ambayo inashirikisha ujenzi wa reli mpya, kuimarisha shirika la ndege la taifa pamoja na kiwanda cha umeme.

Lakini uingiliaji wa serikali katika sekta za uchimbaji madini na kilimo umesababisha kushuka kwa uwekezaji wa kigeni katika taifa hilo ambalo ni la tatu kwa ukubwa wa kiuchumi Afrika mashariki.

Licha ya kujiimarisha katika uuzaji wa bidhaa nje ya nchi, mapato bado yamesalia kuwa ya kiwango cha chini ikilinganishwa na wastani wa kihistoria, imesema benki ya dunia, ikiongezea kwamba uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni umeshuka kwa thuluthi moja na kufikia dola bilioni 1 kutoka dola bilioni 1.5 katika mwaka 2015 na 2018.

Serikali inasema kwamba uchumi ulipanuka kwa asilimia 6.9 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2019 ikilinganishwa na asilimia 6.8 mwaka ulliopita, kutokana na uwekezaji wa kiwango cha juu na uuzaji wa bidhaa katika mataifa ya kigeni unaotokelezwa na raia, ilisema benki ya dunia.

Waziri wa fedha Phillip Mpango aliambia wabunge mnamo mwezi Juni kwamba uchumi utakuwa kwa asilimia 7.1 kutoka asilimia 7.0 mwaka 2018.

Mnamo mwezi Julai, Benki ya dunia ilisema kwamba uchumi wa Tanzania umekuwa kwa asilimia 5.2 mwaka 2018.

Hazina ya fedha duniani IMF pia imeripoti viwango vya chini vya ukuwaji wa uchumi wa Tanzania mwaka huu.

Mnamo mwezi Aprili , IMF ilisema kwamba sera zisizotabirika na zinazoingilia kati zinakandamiza ukuaji kulingana na ripoti iliofichuliwa na chombo cha habari cha Reuters.

Benki ya dunia ilionya siku ya Jumanne kwamba shinikizo ya matumizi kutokana na uchaguzi mkuu mwaka ujao inamaanisha kwamba tafa hilo litalazimika kuimarisha usimamizi wake wa fedha.

Utabiri wa mapato yake ni dhaifu , swala linalopunguza uaminifu wa bajeti na kusababisha mkusanyiko wa malimbikizo ya madeni katika biashara za ndani, "benki ilisema katika ripoti yake.

''Upungufu wa matumizi ya fedha umepanuka na kufikia asilimia 3.2 mwaka 2018/19 kutoka asilimia 1.9 ya ukuaji wa kipindi cha fedha cha 2017/18'', iliongezea.

"Lengo kuu la mapato la asilimia 17.1 ya Pato la Taifa (katika mwaka wa fedha uliopita asilimia 14.0 zilikusanywa) na matumizi ya juu ya bajeti yanaweza kuifanya iwe ngumu kufikia lengo la upungufu wa asilimia 2.3 ya Pato la Taifa mwaka 2019/20,"

1575435614815.png


Chanzo: BBC
 
Back
Top Bottom