Benki ya Dunia yasema Tanzania haikuwa serious na COVID19 mwaka 2020, yatushauri kujiandaa tu kabisa na ugawaji wa chanjo

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
771
1,000
World Bank imetuchamba kizungu:

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bi. Mara Warwick amesema katika hotuba yake kuwa Serikali ya Tanzania ilichukua hatua za mapema za kuondokana na athari za kiafya na kiuchumi za COVID-19 ingawa zilikuwa za kawaida sana na za muda mfupi kulinganisha na nchi nyingine katika ukanda.

Ingawa mporomoko wa kuichumi uliepukwa, kukosekana kwa taarifa rasmi kuhusu maambukizi ya COVID-19 na idadi ya vifo inaweka ugumu katika kufanya uchambuzi wa ubora wa hatua zinazochukuliwa.

Chanjo:

Wakijua kabisa hatutaki chanjo, Mara akasema hivi:


Kuokoa Maisha kunategemea jitihada endelevu katika kukinga, kutambua na kutibu COVID-19 ikisaidiwa na uwazi wa taarifa na utoaji wa ripoti kwa wakati. Uwazi utasaidia kutambuliwa kwa mapema, kuzuia ueneaji na kuisaidia jamii

Kuwekwa kwa mfumo wa ndani kwa ajili ya ufuatiliaji wa COVID-19 itaiweka Serikali katika nafasi nzuri chanjo mpya zikizidi kugunduliwa. Tunaishauri Serikali kuhusisha wadau wenye ujuzi waandae mpango wa kutekeleza ugawaji wa chanjo ya COVID-19.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom