Benki ya Dunia yaipongeza Kenya kwa kupunguza umaskini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1575528286894.png

Benki ya Dunia imetoa ripoti kuwa Kenya imepiga hatua katika kupunguza umaskini na kutimiza haki ya usawa katika miaka kumi iliyopita.

Mchumi wa Benki ya Dunia Bw. Utz Johann Pape, amesema ingawa mafanikio yamepatikana, lakini kiwango cha umaskini bado kiko juu katika kundi la nchi zenye mapato ya kati ya chini.

Pia amesema, ongezeko la pato la taifa la Kenya kwa mwaka katika mwaka 2005 hadi mwaka 2015 limekuwa asilimia 5.3 ambalo limepita kwa kiasi kikubwa ongezeko la wastani la nchi za kusini mwa Sahara ambalo ni asilimia 4.9.

Ripoti hiyo pia imesema, sekta ya kilimo ya Kenya inachukua nafasi muhimu katika kupunguza umaskini, lakini inategemea sana mvua.


Chanzo: Muungwana Blog
 
Mi nilijua labda awa mabeberu wanawapongeza wamekabiliana na wasomali.izo kiki waache wapeane ila tunafahamiana umaskini kunya hauwezi kupungua
 
Back
Top Bottom