Benki ya Dunia yaipa Tanzania fedha zaidi

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
MAISHA zaidi ya Watanzania milioni 6.6 walioko katika kundi la watu masikini na uhaba wa chakula yataboreshwa baada ya Benki ya Dunia kutoa nyongeza ya fedha za Dola za Marekani milioni 200 (sawa na bilioni 400 za Tanzania) kwa ajili ya miradi ya kuondoa umasikini.

Taarifa ya Benki ya Dunia kwa vyombo vya habari jana ilisema Bodi ya Wakurugenzi Watendaji imekubali kutoa msaada mpya kwa ajili ya programu zinazoendelea kwa ajili ya usalama wa jamii zinazotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mradi wa Kaya Salama chini ya ufadhili wa TASAF, utasaidia mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kuongeza misaada ya fedha bila masharti, sambamba na kuongeza ushiriki wa walengwa kufaidika kwenye programu mpya zinazohusisha kuboresha nguvu kazi kubwa ya umma, uwekaji akiba na vitegauchumi.

Desemba mwaka jana, mradi huo ulipata maendeleo makubwa kwa kufikia lengo la kaya milioni 1.1, au wastani wa watu milioni 6.6 miongoni mwa asilimia 15 ya watu masikini jumla ya idadi ya Watanzania milioni 45.

“Kuongezwa kwa kiwango hicho cha fedha katika kusaidia mtandao wa uzalishaji wa jamii salama kutaleta mageuzi makubwa katika mradi huo wa kusaidia kaya masikini Tanzania.,” alisema Bella Bird, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia wa Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia.
 
Tanzania ni nchi tajiri inayopewa misaada na mikopo lukuki.

Analegezwa mtu hapo.
Tanzania ya viwanda mtaisikia tu midomoni
 
Inawezekana ni mikopo iliyokwishapitishwa tangu serikali ya awamu ya tatu bakuli zilipopitishwa.

Usicheze na tabia ya umatonya ni mbaya sana.
 
Jamani situlisema hatutaki misaada na kwamba tunataka sisi ndo tuwe donor country?
Tangu Magufuli awe Rais Tanzania haijawahi kuomba msaada wa fedha. Hata hivyo, Tanzania kama Nchi, haijawahi kutangaza huo msimamo wa kukataa msaada. Magufuli alichosema ni kwamba tTUNATAKIWA kuwa Donor country na sio omba omba
 
Hii mikopo mbona inakua haipo wazi ina riba asilimia ngapi tunasikia tuu baada ya muda deni la Taifa limeongezeka...Tasaf wanaongeza kununua Landrover Puma tuu hao wanapunguza wapi umasikini ?
 
Hizo bil 400 ni ndogo sana! Inabidi wazifanyie mkakati vizuri maana zitaishia kwenye facilitation magari yao na posho! Hiyo miradi iwe na tija basi maana hatuoni direct effect ya miradi yao hao TASAF labda kuzunguka tu vijijini na kulipana posho
 
Tangu Magufuli awe Rais Tanzania haijawahi kuomba msaada wa fedha. Hata hivyo, Tanzania kama Nchi, haijawahi kutangaza huo msimamo wa kukataa msaada. Magufuli alichosema ni kwamba tTUNATAKIWA kuwa Donor country na sio omba omba
Tokea lini mtu akapewa kitu ambacho hakukiomba au unataka kusema benki ya dunia wana huruma sana na watanzania wanaweza kuwapa pesa bila kuomba?
Toka lini serikali ikiomba msaada inatangaza kua sasa tumeomba msaada flani hadi useme serikali ya magufuri haijawahi kuomba msaada.

Rais na mawaziri wake wanapokutana na mabalozi wa marekani, umoja wa ulaya nk hua wanaenda kupiga soga au hao mabalozi ndio wanaomba mawaziri wetu na rais wetu watupatie msaada.

By the way viwanda mnaanza kujenga lini? Zile milioni 50 kila kijiji zinaanza lini kuletwa vijijini?
 
MAISHA zaidi ya Watanzania milioni 6.6 walioko katika kundi la watu masikini na uhaba wa chakula yataboreshwa baada ya Benki ya Dunia kutoa nyongeza ya fedha za Dola za Marekani milioni 200 (sawa na bilioni 400 za Tanzania) kwa ajili ya miradi ya kuondoa umasikini.

Taarifa ya Benki ya Dunia kwa vyombo vya habari jana ilisema Bodi ya Wakurugenzi Watendaji imekubali kutoa msaada mpya kwa ajili ya programu zinazoendelea kwa ajili ya usalama wa jamii zinazotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mradi wa Kaya Salama chini ya ufadhili wa TASAF, utasaidia mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kuongeza misaada ya fedha bila masharti, sambamba na kuongeza ushiriki wa walengwa kufaidika kwenye programu mpya zinazohusisha kuboresha nguvu kazi kubwa ya umma, uwekaji akiba na vitegauchumi.

Desemba mwaka jana, mradi huo ulipata maendeleo makubwa kwa kufikia lengo la kaya milioni 1.1, au wastani wa watu milioni 6.6 miongoni mwa asilimia 15 ya watu masikini jumla ya idadi ya Watanzania milioni 45.

“Kuongezwa kwa kiwango hicho cha fedha katika kusaidia mtandao wa uzalishaji wa jamii salama kutaleta mageuzi makubwa katika mradi huo wa kusaidia kaya masikini Tanzania.,” alisema Bella Bird, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia wa Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia.
Mbona mlisema hamhitaji wafadhili walipo ondoa MCC!!??
 
Jamani situlisema hatutaki misaada na kwamba tunataka sisi ndo tuwe donor country?
Poleni sana si mnasema Rais Dikteta?! Hivyo mlitegemea kunyimwa misaada. Of course VIION ya Mh. Rais haiwezi kufa kwa maneno yenu yasiyo na kichwa wala miguu!
 
Good news!
Good news kwa kupewa misaada wakati sisi ndio tulitakiwa kuwa tunasaidia nchi nyingine zenye shida na uhitaji? Yaani Mwenyezi Mungu katujalia baraka na neema ya pekee ya kuwa na rasilimali za kila aina,lakini leo eti mtu mzima kabisa anafuahia kusaidiwa kuondoa umasikini ambao haukutakiwa uwepo?
 
Tanzania ni nchi tajiri inayopewa misaada na mikopo lukuki.

Analegezwa mtu hapo.
Tanzania ya viwanda mtaisikia tu midomoni
Mkui sensor,chukia like. Ni akina jesika tu ndio wanaoweza furahia hii misaada na kuiita good news au eti ni neema. Hawajui hii nchi ni tajiri kupindukia na hao wanaotusaidia wana lao jambo,si kwa good faith.
Someni Hard Choices: A Memoir ya Hillary Clinton na Confessions of An Economic Hitmen cha John Perkins mjue nini kinaendelea.
 
Inahitaji akili pevu, pana, kubwa ili kufungua hii minyororo ya hawa wanyonyaji wa dunia ya kwanza otherwise hawa wa akili matope nothing they'll do.
 
Back
Top Bottom