beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
LICHA ya serikali kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini, Ripoti ya Benki ya Dunia (WB) imetaja vikwazo 12 vya ufanyaji biashara nchini.
Katika ripoti hiyo ya mwaka 2019/20 imeonyesha kuwa Tanzania imeboresha baadhi ya mambo kiasi ya kuifanya kushika nafasi ya 141 kati ya 190 mwaka huu ikilinganishwa na nafasi ya 144 iliyoshika mwaka uliopita.
Maboresho hayo yameifanya Tanzania kushika nafasi ya nne katika nchi za Afrika Mashariki baada ya Rwanda, Kenya na Uganda.
Ripoti hiyo imeitaja Rwanda kushika nafasi ya 29 kati ya 190 ikiwa imeboresha kutoka nafasi ya 41 iliyoshika mwaka jana, huku Kenya ikishika nafasi ya 80 ikitoka nafasi ya 61 hadi mwaka 2018 ikilinganishwa na nafasi ya 80 mwaka 2017. Uganda imeshika nafasi ya 127 na Burundi 168, huku New Zealand ikiongoza.
Baada ya kutoa ripoti hiyo mwaka jana, Tanzania iliboresha baadhi ya mazingira ya ufanyaji biashara mojawapo ikiwa ni kuondoa urasimu, kubadilisha baadhi ya sheria, kupunguza baadhi ya kodi zilizokuwa kero kwa wafanyabiashara, pamoja na kupambana na rushwa.
Baadhi ya mabadiliko yaliyofanyika ni majukumu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na kuwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).
Pia Tanzania imeanzisha kitabu cha maboresho kwa wafanyabiashara (Brueprint) ikiwa na dhumuni la kuweka mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara kwa wafanyabiashara.
Ripoti hiyo ilitaja vikwazo 12 ambavyo ilikuwa inaviangalia katika nchi husika ambavyo wafanyabiashara wanakumbana navyo.
Vikwazo hivyo ni mazingira ya kuanzisha biashara, kupata kibali cha ujenzi, upatikanaji wa umeme, usajili wa bidhaa, kuwalinda wawekezaji, makato katika kodi, uingizaji wa bidhaa mipakani, uingiaji wa mikataba, kuajiri wafanyakazi, pamoja na mikataba kati ya wawekezaji na serikali.
Ripoti hiyo ilieleza kuwa kipengele cha uanzishaji wa biashara walikuwa wakiangalia utaratibu, muda na gharama za uanzishaji wa biashara katika nchi husika.
Kwenye kigezo cha kibali, waliangalia utaratibu, muda, gharama za kumaliza ujenzi wa maghala ya kuhifadhi bidhaa, kwenye kigezo cha umeme waliangalia upatikanaji wa umeme wa kutosha kuwezesha viwanda kufanya kazi kwa wakati wote.
Ripoti hiyo ilieleza kuwa kwenye usajili wa bidhaa, waliangalia utaratibu wa kusajili biashara, muda na gharama za kukamilisha taratibu zote hadi mfanyabiashara anaanza kufanya biashara.
Kuwalinda wawekezaji, ripoti hiyo ilieleza kuwa waliangalia namna serikali husika inavyolinda haki za wawekezaji, kwenye ulipaji wa kodi na muda wanaopewa wafanyabiashara wa ulipaji kodi.
Kwenye kipengele za uingizaji bidhaa mipakani, ripoti hiyo ilieleza kuwa iliangalia muda na gharama za kuingiza bidhaa kutoka ndani na nje ya nchi.
“Togo ni miongoni mwa nchi zilizoboresha mazingira ya kufanya biashara kwa mwaka wa pili sasa, wameboresha ada ya kibali cha ujenzi, pamoja na usajili wa bidhaa. Nigeria ipo katika marekebisho ya baadhi ya viashiria,” ilieleza ripoti hiyo.
Aidha, ilieleza kuwa baadhi ya nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kama Afrika Kusini, Liberia, Burundi, Afrika ya Kati na Namibia zimeendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara ikiwamo upatikanaji wa umeme wa kutosha, mfano wafanyabiashara wanalipa zaidi ya asilimia 3,100 ya wanachoingiza kwa siku ili waunganishwe katika gridi.
Ripoti hiyo ilieleza kuwa katika kipengele za kufanya biashara mipakani pamoja na ulipaji wa kodi, wafanyabiashara wanatumia zaidi ya saa 96 kushughulikia nyaraka zao ili kuingiza bidhaa.
Alipotafutwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, kuzungumzia ripoti hiyo, simu yale ilikuwa ikiita bila majibu.