Benki ya Dunia: Uchumi wa Tanzania umeimarika, mtandao wa barabara kuipaisha zaidi


FikraPevu

FikraPevu

Verified Member
Joined
Jan 2, 2010
Messages
303
Likes
122
Points
60
FikraPevu

FikraPevu

Verified Member
Joined Jan 2, 2010
303 122 60
Licha ya uchumi wa Tanzania kuimarika na kuchangia kukua kwa pato la ndani la Afrika, Tanzania imetakiwa kuboresha miundombinu ya barabara ili kuwavutia wawekezaji kuwekeza katika sekta za uzalishaji na biashara.

Kulingana na takwimu kutoka Benki ya Dunia, Tanzania ni miongoni mwa nchi tano za Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi, ambapo hadi kufikia 2015 uchumi wake ilikuwa umekua kwa zaidi ya asilimia 5.4. Kulingana na takwimu za serikali uchumi umeimarika na kukua kwa asilimia 6.8 kwa mwaka 2017

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Masuala ya Uchumi wa Benki ya Dunia katika nchi za Afrika, Dkt. Albert Zeufack, wakati wa mjadala uliondaliwa na Benki ya Dunia Tanzania kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kujadili Mchango wa Tanzania katika ukuaji wa bara la Afrika, ambapo amesema nchi za Afrika ikiwemo Tanzania zinakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya uhakika kwenye usafirishaji.

Mtandao wa barabara katika nchi za Afrika bado haujaunganisha maeneo muhimu ya uzalishaji licha ya nchi hizo kuwa na rasilimali nyingi ambazo hazijatumika. Afrika ina jukumu la kuimarisha mfumo wa usafirishaji ili wawekezaji wajitokeze kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Afrika ambao unakuwa kwa kiwango kizuri.

“Uchumi wa Afrika umekuwa kwa asilimia 2.4 mwaka 2017 na unatarajiwa kukua kwa 3.2% mwaka 2018. Ukuaji wa Afrika unaakisi kuimarika kwa hali ya uchumi wakati wakitekeleza mikakati ya kutatua changamoto za kutokuwepo kwa usawa wa kiuchumi katika nchi zao”, amesema Dkt. Zeufack

Ameeleza kuwa wawekezaji binafsi kutoka katika nchi zilizoendelea wana mitaji na teknolojia ambayo wanatafuta nchi yenye mazingira mazuri ya kufanyia biashara na miundombinu ya usafirishaji wa malighafi na bidhaa za viwandani.

Ameishauri Tanzania kuweka kipaumbele katika miradi ya barabara ambayo ina manufaa kwa nchi, kuunda vyombo vya usimamizi wa miundombinu ambavyo vitahusika na manunuzi na kufanya utafiti wa maeneo muhimu ambayo yanatakiwa kuunganishwa na mtandao wa barabara ili kuwawezesha wawekezaji binafsi kuziendeleza rasilimali za nchi.

Zaidi, soma hapa => Benki ya Dunia: Uchumi wa Tanzania umeimarika, mtandao wa barabara kuipaisha zaidi | FikraPevu
 
number41

number41

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
1,153
Likes
642
Points
280
number41

number41

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
1,153 642 280
Tuliambiwa iko 7..... Imekuaje tena mbona sielewi au serikali izo number huwa inatunga
 

Forum statistics

Threads 1,237,639
Members 475,675
Posts 29,295,468