Benki ya Dunia: Tanzania kwa muongo mmoja uliopita imekuwa na uchumi imara na ukuaji mkubwa wa pato la taifa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Takwimu za Benki ya Dunia zinaonesha kuwa Tanzania kwa muongo mmoja uliopita imekuwa na uchumi imara na ukuaji mkubwa wa pato la taifa wa wastani wa asilimi nane.

Kwa mujibu wa takwimu hizo Tanzania imehakikisha pia ukuaji wa ajira rasmi na zisizo rasmi unabaki katika kiwango kizuri, kikiwa kwenye wastani wa asilimia 1.9.

Mafanikio hayo makubwa ya kiuchumi na soko la ajira pia yanaelezwa kuchangiwa kwa kiasi fulani na sekta binafsi na biashara ambayo ni mihimili katika sekta hiyo ikijumuisha teknolojia, ujenzi na mawasiliano.

Taarifa zaidi zinasema makampuni katika maeneo hayo matatu yametoa ajira kwa idadi kubwa ya watanzania na pia huduma zake zinahitajika katika sekta nyingine zote za uchumi.

Inaelezwa kuwa sekta ya mawasiliano ya simu imekuwa ikitoa ajira kupitia maeneo yake mbalimbali kama vile kupitia mawakala wa fedha, wasambazaji na wauzaji wa huduma za simu, wataalamu wa huduma kwa wateja na wengineo.

Zaidi ya hiyo, sekta hiyo pia inahitaji wataalamu kutoka maeneo mengine mengi mfano wahandisi wa mitambo ya mawasiliano na wachambuzi wa takwimu na wako wataalamu lukuki wa fani mbalimbali ambao wanahakikisha saa 24 mitambo iko sawa ili wateja waweze kupata huduma na kutumia simu zao bila tatizo mfano kuperuzi mtandaoni, kununua bando, kutuma na kupokea fedha, kutuma ujumbe mfupi na nyingine nyingi.

Kampuni ya Tigo Tanzania ni mfano mmojawapo wa kampuni hizo na inatajwa kama mwajiri muhimu nchini ikiwa na zaidi ya wafanyakazi 115,000 wenye ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja na kwa msingi huo nchi haina budi kuendelea kuunga mkono sekta hii na wadau wake wa namna hiyo ili kusukuma zaidi gurudumu la maendeleo ya uchumi wetu.
 
Hongera Magufuli

Wale wasaliti wa nchi sijui wataweka wapi sura zao

Walikuwa wanatudanganya uchumi unashuka
 
Waliozoea pesa za kwenye sandarusi hawakuelewa, wao uchumi kukua ni mpaka waibe pesa za wanyonge
 
Mkuu anataka ibaki kampuni moja tuu ya ttcl kama ethiopia.Sasa wewe unasena tigo
 
Hapa kazi tu,NA bado kuna dreamliner inaingia Ijumaa tarehe 26 hizo zote ni ajira kwa watanzania...
 
Ukilala ukiamka unawaza magufuli tu,umeambiwa muongo mmoja uliopita,hujui maana ya muongo au ,chukua miaka minne ya Magufuli toa kwenye kumi unapata 6 hivyo kuna waliofanya kazi kubwa kabla yake.Usione vinaelea vimeundwa
Hongera Magufuli

Wale wasaliti wa nchi sijui wataweka wapi sura zao

Walikuwa wanatudanganya uchumi unashuka
 
Ukilala ukiamka unawaza magufuli tu,umeambiwa muongo mmoja uliopita,hujui maana ya muongo au ,chukua miaka minne ya Magufuli toa kwenye kumi unapata 6 hivyo kuna waliofanya kazi kubwa kabla yake.Usione vinaelea vimeundwa
Tatizo kubwa la watu wetu ni ujinga...ndo mtaji Wa ccm
 
Takwimu za Benki ya Dunia zinaonesha kuwa Tanzania kwa muongo mmoja uliopita imekuwa na uchumi imara na ukuaji mkubwa wa pato la taifa wa wastani wa asilimi nane.

Kwa mujibu wa takwimu hizo Tanzania imehakikisha pia ukuaji wa ajira rasmi na zisizo rasmi unabaki katika kiwango kizuri, kikiwa kwenye wastani wa asilimia 1.9.

Mafanikio hayo makubwa ya kiuchumi na soko la ajira pia yanaelezwa kuchangiwa kwa kiasi fulani na sekta binafsi na biashara ambayo ni mihimili katika sekta hiyo ikijumuisha teknolojia, ujenzi na mawasiliano.

Taarifa zaidi zinasema makampuni katika maeneo hayo matatu yametoa ajira kwa idadi kubwa ya watanzania na pia huduma zake zinahitajika katika sekta nyingine zote za uchumi.

Inaelezwa kuwa sekta ya mawasiliano ya simu imekuwa ikitoa ajira kupitia maeneo yake mbalimbali kama vile kupitia mawakala wa fedha, wasambazaji na wauzaji wa huduma za simu, wataalamu wa huduma kwa wateja na wengineo.

Zaidi ya hiyo, sekta hiyo pia inahitaji wataalamu kutoka maeneo mengine mengi mfano wahandisi wa mitambo ya mawasiliano na wachambuzi wa takwimu na wako wataalamu lukuki wa fani mbalimbali ambao wanahakikisha saa 24 mitambo iko sawa ili wateja waweze kupata huduma na kutumia simu zao bila tatizo mfano kuperuzi mtandaoni, kununua bando, kutuma na kupokea fedha, kutuma ujumbe mfupi na nyingine nyingi.

Kampuni ya Tigo Tanzania ni mfano mmojawapo wa kampuni hizo na inatajwa kama mwajiri muhimu nchini ikiwa na zaidi ya wafanyakazi 115,000 wenye ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja na kwa msingi huo nchi haina budi kuendelea kuunga mkono sekta hii na wadau wake wa namna hiyo ili kusukuma zaidi gurudumu la maendeleo ya uchumi wetu.
Source
 
Hongera Magufuli

Wale wasaliti wa nchi sijui wataweka wapi sura zao

Walikuwa wanatudanganya uchumi unashuka
acha ujinga muongo mmoja unaanzia 2009, Mpaka sasa most statistics ni za kipindi cha Jakaya, subiri ifike 2023 usikie taarifa yao.
 
Back
Top Bottom