Benki ya Dunia kugharamia reli kuna lengo la kuigeuza Tanzania kuwa lango kuu la kanda

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,688
2,000

Mabadiliko ya mtandao wa reli ya Tanzania ni pamoja na kuendeleza njia zote kwa kipimo cha kiwango na kupanua Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ili kuiunganisha na mitandao ya reli za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Idhini ya Benki ya Dunia ya hivi karibuni ya dola milioni 300, fedha za kusaidia miundombinu ya reli ya Tanzania inatoa ahadi ya kuleta mabadiliko ya msingi katika mfumo wa usafiri wa nchi na kusaidia kukuza maisha ya watu maskini wa kanda hii.


Mradi huo, ambao utatekelezwa na Shirika la Reli Tanzania, utafanyika pamoja na sehemu ya Dar es Salaam-Isaka ya Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Una lengo la kusaidia kuchukua shinikizo la bandari ya Dar es Salaam, kuwezesha usafirishaji wa bidhaa kwenda na kutoka nchi jirani za Tanzania zisizo na bahari, na kukuza uchumi wa ndani.

Benki ya Dunia alitangaza mwezi uliopita kwamba ilikuwa imetoa fedha kusaidia juhudi za Tanzania za kufungua reli ya ukanda wa Afrika Mashariki, ambayo hutumikia Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

"Mradi huu utasaidia kuboresha kiungo muhimu katika mtandao wa reli ya kikanda ambayo ni muhimu kwa ushindani na uboreshaji wa ushirikiano wa kiuchumi kikanda na kimataifa," Kiongozi wa Kikosi Kazi cha Benki ya Dunia Henry des Longchamps alisema tarehe 24 Aprili.

Fedha hizo, zinazotolewa kutoka Ushirika wa Benki ya Dunia kwa Maendeleo ya Kimataifa, pia utaimarisha uwezo wa Shirika la Reli Tanzania wa kusimamia miundombinu, utendaji kazi wa trafiki na mtandao wa kanuni, Benki ya Dunia ilisema katika taarifa.

Utekelezaji wa mradi wa Benki ya Dunia utakuwa kazi kubwa zaidi kufanywa na Shirika la Reli Tanzania mpaka sasa, msemaji wa kampuni ya Midladjy Maez alisema.

Uboreshaji huo ni pamoja na kuimarisha kipimo cha sasa cha mita, ujenzi wa madaraja ya treni na kuendeleza muundombinu wa reli kutoka Dar es Salaam hadi Isaka, ambako reli za Rwanda na Burundi zitaungana, Maez aliiambia Sabahi.

Rwanda, Burundi na Tanzania pia zinafanyakazi kila moja pekee katika mradi tofauti inayofadhiliwa ambayo hatimaye itaboresha njia za reli katika nchi zote tatu kwa kipimo cha kiwango, hivyo kuhakikisha uunganishaji wa treni.

Kuendeleza Isaka kwa huduma za treni za kuaminika kutasaidia mipango ya kuanzisha tena mji kama 'bandari za nchi kavu', ambapo bidhaa zitakazopakuliwa kutoka Dar es Salaam zinaweza kupelekwa kwengine ili kulipia ushuru, na hivyo kuondoa vikwazo katika bandari ya Dar es Salaam na kupunguza gharama, Maez alisema.

Mradi huu ni sehemu ya Mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa, inayojumuisha mipango ya kuongeza uwezo wa usafirishaji wa reli wa Tanzania kutoka tani milioni 1.4 za sasa hadi kufikia tani milioni 3 kwa mwaka.

"Hadi Disemba mwaka huu tutakuwa tumeshaagiza kutoka nje injini mpya 21 na tuna lengo la kuwa na injini mpya 50 ifikapo mwaka 2015," alisema. "Kwa msaada wa Benki ya Dunia tutakarabati madaraja 28 na kuimarisha reli ya sasa."

'Fursa ya dhahabu' kwa maendeleo
Huduma ya reli huanzia Dar es Salaam na kuelekea ukanda wa kaskazini-magharibi hadi mkoa wa Tabora, ambapo hugawika na kuelekea mikoa ya Kigoma na Mwanza. Tawi linalokwenda Mwanza, hugawika tena katika eneo linaloitwa Tinde, ambapo inakwenda Isaka. Tawi la Mwanza pia huhudumia Uganda, wakati tawi la Kigoma huhudumia DRC.

"Eneo na ukubwa wa Tanzania, rasilimali zake za madini na kilimo, uwezo wake wa utalii na mchango wake muhimu kama kitovu cha usafiri kwa nchi jirani zisizokuwa na bandari kutoa fursa zisizo na ushindani kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu ya usafiri wa kisasa na huduma," Mkurugeni wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Philippe Dongier alisema katika taarifa.

"Mradi huo pia utasaidia kukuza biashara ya kilimo sio moja kwa moja, utatoa ajira na maisha kwa ujumla kwa nchi kwa watu 'maskini zaidi' wa nchi jirani," alisema.

Reli ya ukanda wa kati ilijengwa mwaka 1906 na Waingereza na tangu wakati huo haijafanyiwa ukarabati wowote mkubwa.

Prosper Honest Ngowi, mhadhiri mwandamizi wa uchumi katika Chuo Kikuu Mzumbe, alisema mradi huo ni fursa kwa Tanzania ambayo lazima iikumbatie ili kupunguza umaskini uliokithiri.

"Hii ni nafasi ya dhahabu ambayo nchi inapaswa kuchukulia kwa umakini. Kupata dola milioni 300 maalum kwa ajili ya miundombinu ya reli kwa mara moja ni uwekezaji mzuri," aliiambia Sabahi.

Ngowi alisema reli iliyofufukwa inapaswa kutazamwa kama fursa ya kiuchumi kwa jamii zinazohudumiwa na njia za reli, na sio tu kama njia ya usafiri tu.

Kwa mfano, alisema, jamii ambayo haishiriki katika kilimo cha biashara lazima kipatiwe elimu juu ya jinsi ya kushiriki, sasa ambapo kutakuwa na njia ya kuaminika kusafirisha bidhaa.

"Wananchi wanaoishi jirani na reli lazima waarifiwe fursa hii ambayo inakuja kwao," alisema. "Serikali inapaswa kuwapa uwezo wa kuwa wakulima wakubwa na kusafirisha mazao yao kwa kutumia reli hii iliyoboreshwa, ambayo ni nafuu ikilinganishwa na barabara na usafiri wa anga."

Anthony Kayanda, mwandishi wa habari anayeishi katika mkoa wa Kigoma, alisema mradi huo utakuza uchumi wa ndani, kuanzisha usafiri wa treni wa kuaminika zaidi na kuwasaidia wakazi kupata fursa za biashara.

"Hii ni habari njema. [usafiri] wa treni ni usafiri pekee uliopo kwa ajili ya wakazi wa Kigoma. Kuna vijiji kama Uvinza, Malagarasi, Kazimaramimba, Kandaga, Kalenge na Nguruka, ambavyo havina aina yoyote ya usafiri isipokuwa treni," Kayanda aliiambia Sabahi.mia

Chanzo: Sabahi
 

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,115
2,000
ingawa ni fursa nzuri na tumaini la ukombozi wa mlalahoi wa kitanzania,sidhani kama itapokelewa na viongozi wetu wa ccm kwa moyo mkunjufu maana wao wananufaika na biashara ya malori nchini,pamoja na uwekezaji kwenye vituo lukuki vya mafuta.
binafsi nakuskhukuru kwa dhati mleta taarifa hii kwani ni habari njema kwa watanzania,nashangaa kwa nini haijapewa kipumbele kwenye vyombo vyetu vya habari:israel:
 

bwegepeponi

Member
Sep 16, 2013
74
70
ingawa ni fursa nzuri na tumaini la ukombozi wa mlalahoi wa kitanzania,sidhani kama itapokelewa na viongozi wetu wa ccm kwa moyo mkunjufu maana wao wananufaika na biashara ya malori nchini,pamoja na uwekezaji kwenye vituo lukuki vya mafuta.
binafsi nakuskhukuru kwa dhati mleta taarifa hii kwani ni habari njema kwa watanzania,nashangaa kwa nini haijapewa kipumbele kwenye vyombo vyetu vya habari:israel:
Porojo at work! To good to be true under this government! Malori yetu itakuwa vipi?
 

manning

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
3,524
1,250
Hii ndo habari bora tangu mwaka huu uanze. Tumechoka kusoma habari za matusi ya siasa za katiba. Hofu yangu ni hujuma itakayoukumba mradi huu kwa sababu watawala ndiyo wana malori na mabasi yanayosafirisha watu na mizigo ndani na nje ya nchi.
 

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,688
2,000
ingawa ni fursa nzuri na tumaini la ukombozi wa mlalahoi wa kitanzania,sidhani kama itapokelewa na viongozi wetu wa ccm kwa moyo mkunjufu maana wao wananufaika na biashara ya malori nchini,pamoja na uwekezaji kwenye vituo lukuki vya mafuta.
binafsi nakuskhukuru kwa dhati mleta taarifa hii kwani ni habari njema kwa watanzania,nashangaa kwa nini haijapewa kipumbele kwenye vyombo vyetu vya habari:israel:
Ndiyo maana Tanzania inahitaji kupata katiba mpya. vinginevyo hakuna kitakacho fanyika sababu mtuhumiwa ndo huyo huyo hakimu. mia
 

ROBERT MICHAEL

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
4,922
2,000
Siaminiamini reli kujengwa na haya malori ya wakuu na familia zao yatafanya kazi gani sasa.Yetu macho.
 

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,519
2,000
Yaani reli ijengwe wakati Lake Oil ndio kwanza anatandaza mitandao mipya na yeye kashatangulia bungeni kuwahi masirahi. Hii ni ndoto , tusubiri tuone.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom