#COVID19 Benki ya Dunia: COVID-19 imewarudisha Watanzania takriban 600,000 chini ya mstari wa umasikini

COVID 19 inazidi kurudisha nyuma juhudi za nchi masikini kujikwamua.

Kwa Tanzania watu 500,000 wamerudi kwenye lindi la umasikini, inasikitisha maana itahitaji nguvu nyingi sana kujitoa tena huko.

Kama jamii tuungane kufuata hatua za kupambana na janga hili ili angalau tusiendelee kupata madhara makubwa zaidi.
 
Watu laki tano hao ni wale waliokuwa na uwezo na wameathiriwa na kurudi kwenye umasikini imagine kwa wale ambao hawakuwa na pesa kabisa nahisi wameathirika zaidi nikiwamo mimi.
 
Corona imepiga uchumi wa dunia. Mitaji, biashara zimeyumba, ajira katika utalii, biashara za Kimataifa zimetikiswa. Global political economy kwa sasa ni namna gani ya kurescue sekta ili kupunguza umasikini, kuimarisha sekta binafsi na umma, kutengeneza fursa za ajira, kutafuta na kutumia resources za kunusuru hali.

Hiki nilitegemea kukiona kwa vyama hadi vya upinzani nchini. Badala yake CHADEMA wanakuja na hoja ya Katiba mpya ambayo si ajenda inayoweza kujadili mipango ya dharura kusaidia kampuni za utalii kule Arusha, Kilimanjaro, kusaidia wakulima waweze kurejesha mzunguuko wa biashara, sekta binafsi iamke. Ni muhimu sana wanasiasa wetu wajue ajenda na mahitaji ya watu kwa wakati. #Uchumi kwanza.
Kwa kifupi ajenda ya siasa ya dunia na hata nchini kwa sasa iko driven na hali ya uchumi baada ya kupigwa na Corona. Ni namna gani tunarejesha ajira, kupunguza mnyororo wa umasikini, kupata resources, tutumie vipi zilizopo, tuinue sekta binafsi ikiwemo utalii, kilimo, biashara na Uwekezaji kwa kuvutia mitaji. Sasa leo unakuja na ajenda ya Katiba mpya! Utaonekana kituko tu. Kwa sababu siyo issue ya dharura#Uchumi kwanza.
 
Corona imepiga uchumi wa dunia. Mitaji, biashara zimeyumba, ajira katika utalii, biashara za Kimataifa zimetikiswa. Global political economy kwa sasa ni namna gani ya kurescue sekta ili kupunguza umasikini, kuimarisha sekta binafsi na umma, kutengeneza fursa za ajira, kutafuta na kutumia resources za kunusuru hali.

Hiki nilitegemea kukiona kwa vyama hadi vya upinzani nchini. Badala yake CHADEMA wanakuja na hoja ya Katiba mpya ambayo si ajenda inayoweza kujadili mipango ya dharura kusaidia kampuni za utalii kule Arusha, Kilimanjaro, kusaidia wakulima waweze kurejesha mzunguuko wa biashara, sekta binafsi iamke. Ni muhimu sana wanasiasa wetu wajue ajenda na mahitaji ya watu kwa wakati. #Uchumi kwanza.
Nadhani Chadema wanatest hali baada ya kuwa cornered kwa miaka ya karibu na utawala wa Rais aliyepita. Nikiwaweka wao kwenye uongozi wangeenda na ajenda Lockdown, labda hali ingekuwa mbaya zaidi!
 
Corona imepiga uchumi wa dunia. Mitaji, biashara zimeyumba, ajira katika utalii, biashara za Kimataifa zimetikiswa. Global political economy kwa sasa ni namna gani ya kurescue sekta ili kupunguza umasikini, kuimarisha sekta binafsi na umma, kutengeneza fursa za ajira, kutafuta na kutumia resources za kunusuru hali.

Hiki nilitegemea kukiona kwa vyama hadi vya upinzani nchini. Badala yake CHADEMA wanakuja na hoja ya Katiba mpya ambayo si ajenda inayoweza kujadili mipango ya dharura kusaidia kampuni za utalii kule Arusha, Kilimanjaro, kusaidia wakulima waweze kurejesha mzunguuko wa biashara, sekta binafsi iamke. Ni muhimu sana wanasiasa wetu wajue ajenda na mahitaji ya watu kwa wakati. #Uchumi kwanza.
Kosa lako ni kuwabeza wapinzani wa hapa kudai katiba mpya yenye kuweka usawa kati ya watawala na watawaliwa. Bila katiba nzuri inayodhibiti ubadhirifu na ufisadi na ukanda wa viongozi wetu. Uchumi ni kazi bure.
 
Niko hapa nasikiliza ripoti ya benki ya dunia, kilichonigusa ni watanzania ambao walishatoka kwenye mstari wa umaskini na Covid19 imeamua kuwarudisha, imani yangu sehemu kubwa ya kundi hili inatoka kwenye sekta ya utalii na nyinginezo zilizofungamana na uchumi wa kimataifa. Hapo bado walioyumba lakini hawajagusa mstari wa umaskini.

Positive, Anguko la Tanzania lina ahueni kulinganisha na nchi zilizotuzungua(Labda policy ya kutojifungia ilitusaidia) though uchumi umeshuka

Hivi Serikali ilishafanya mpango wowote kuwakwamua? Hawa jamaa zetu walishayapatia maisha
Watuache

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
- Tunapendekeza Serikali itoe motisha kwa Wafanyabiashara ikiwemo Msamaha wa Kodi au kipindi cha Neema ili kuvuka kipindi hiki kigumu Baadaye wakati mambo yote yakiwa sawa, tunaweza kuzungumza juu ya changamoto za ushuru, sera na mfumo wa udhibiti

- Tunapozungumza juu ya kuboresha Mazingira ya Biashara, tunahitaji kuelewa jukumu la kila mmoja Serikali ni mtunga Sera na Mdhibiti, sisi ndio Wafanyabiashara tunaohusika na miamala na kodi
Natamani Serikali yetu izingatie mapendekezo haya hasa hapo kwenye msamaha wa kodi.
 
Ingawa utalii umeathirika sana na Covid, sekta ya kilimo ndio imekuwa "shock absorber" kwa kiasi kikubwa ingawa nayo imeathirika kiasi hasa kwa ilipokuja suala la usafirishaji wa mazao nje ya nchi.

Nitashangaa sana jukwaa hili la "World Bank" kutoweka mkazo kwenye kilimo. Kama nchi na kwa level yetu ya maendeleo kilimo hakiepukiki kuendelezwa na kusimamiwa vizuri ili kuchangia maendeleo zaidi ya nchi hii.
 
Hiyo Covid isisingiziwe kila kitu, umaskini tumeukumbatia toka tupate uhuru 1961.
 
Kosa lako ni kuwabeza wapinzani wa hapa kudai katiba mpya yenye kuweka usawa kati ya watawala na watawaliwa. Bila katiba nzuri inayodhibiti ubadhirifu na ufisadi na ukanda wa viongozi wetu . Uchumi ni kazi bure
Ndugu yangu, nimejaribu kuwassidia. Hata Rais hajabeza issue ya Katiba. Ila nazungumzia 'timing'. Yes to constitution ila si sasa na hata mjadala wake si sasa. Uchumi umepigwa na Corona. Sisi tumshukuru Mungu kumuongoza JPM hatukujifungia hali ingekuwa mbaya sana.

Sasa katika hali hii ambayo kampuni za utalii ziko hoi, ajira zimeanguka, mitaji, uwekezaji na biashara nyingi zenye mnyororo wa Kimataifa zimetikiswa, sekta binafsi hoi, nilitegemea wanasiasa makini na vyama vyao waje na ajenda hii ya uchumi na kutoa the way out kwamba sasa kama Taifa tunaweza kutokaje hapa.

Tutumie vipi resources zetu na tutafute wapi nyingine. Ni kama vile wanavyoshauri bungeni kwa kutoa Bajeti vivuli. Hii ndiyo siasa iliyokomaa. Inayokuja na ajenda za wakati na kutoa suluhu. Ajenda ya sasa ni uchumi tena mipango ya dharura.
 
Sasa ni muda mwafaka Benki ya Dunia kuelekeza nguvu zao kwenye utalii, ili kuwainua au kuwaangazia Waliowekeza kwenye utalii kama inavyofanya kwenye afya.
 
Ingawa utalii umeathirika sana na Covid, sekta ya kilimo ndio imekuwa "shock absorber" kwa kiasi kikubwa ingawa nayo imeathirika kiasi hasa kwa ilipokuja suala la usafirishaji wa mazao nje ya nchi.

Nitashangaa sana jukwaa hili la "World Bank" kutoweka mkazo kwenye kilimo. Kama nchi na kwa level yetu ya maendeleo kilimo hakiepukiki kuendelezwa na kusimamiwa vizuri ili kuchangia maendeleo zaidi ya nchi hii.
Naona mapendekezo yao yamejikita zaidi kwenye msamaha wa kodi na kuboresha mazingira ya biashara. Japo ukiangalia kwa jicho fulani unapozungumzia mazingira ya biashara kwa Tanzania huwezi tenganisha na kilimo.
 
Pia hawa wanaofanya issue za utalii wanatudharau wazawa. Sasa times kama hizi wazawa ambao bado tumejaaliwa vipato tungewainua.
 
"COVID-19 imewarudisha watanzania takribani 600,000 chini ya mstari wa umaskini"

Na hapa bado hatujafunga hata miaka 2 kamili tangu janga litusabahi. WTF!
 
Tukiachana na hiyo ripoti, aliyeandika habari hii kaidharirisha sana JamiiForums. Matumizi ya vifupisho kama, 'ktk' badala ya 'katika' na kukosekana kwa vituo, kunashusha hadhi ya habari iliyandikwa na Jamiiforums.
 
Hiyo 500,000 izidishe mara ( X ) 5 Wastani wa Watu Tegemezi ndani ya hizi Familia zetu hivyo utagundua kuwa huenda 'Figure' ikawa ni Kubwa kuliko hii yao ( yako ) tajwa hapa.
Extended Families na multiplication effect, Mungu atusaidie.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom