VeroEretico
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 505
- 388
Haya mabadiliko yanagusa na waliokopa hapo kabla au wakopaji wapya tu?
ina maana husikilizi hata radio au kusoma magazeti maana wametangaza na wameandika kwenye magazeti ya guardia au unasoma magazeti ya udaku tuMbona hao BancABC interest rate ni 19% au ww umetoa wapi hiyo 11%?
BancABC
Cheki kwenye personal loan
mzandiki ni wewe na mama yako anayekufundisha mdomo mchafuSio kweli, Bank ABC ni 17% sio 11% acha uzandiki.
Muda Una Affect Vipi Hela ya Kukopa?.. Wakati inabaki pale paleBank wana akili sana, hapo hamna kilichopunguzwa
@gui1 kwa mujibu wa hii comment anayenufaika ni bank...Absolutely right! Rejea jedwali la BancABC (BancABC) mikopo ya mwaka 1, 2, na 3 (miezi 12, 24, 34). Kwa mfano, ukichukua mkopo wa TZS. 35,000,000 hesabu yake inakuwa kama ifuatavyo:-
Kwa miezi 36: 1,282,960.70 x 36 = 46,186,585.20 (benki inachukua 46,186,585.2 - 35,000,000 = 11,186,585.20)
Kwa miezi 24: 1,764,301.60 x 24 = 42,343,238.40 (benki inachukua 42,343,238.40 - 35,000,000 = 7,343,238.40)
Kwa miezi 12: 3,225,480.24 x 12 = 38,705,762.88 (benki inachukua 38,705,762.88 - 35,000,000 = 3,705,762.88)
I have now got the concept; mikopo ya muda mrefu ni balaa. Na walivyo, they never clarify this to customers! Some sort of utapeli fulani.
NMB kukoje ,Riba haijapungua! nataka chukua milioni nane kwa miaka 6
Dar es Salaam. Benki ya CRDB imeongeza muda wa marejesho kutoka miezi 60 hadi 84 huku ikishusha riba kwa asilimia nne kwa wateja wake, hasa wafanyakazi.
Benki hiyo imeshusha riba kutoka asilimia 21 mpaka 17 huku muda wa marejesho ukitofautiana kati ya wafanyakazi wa sekta binafsi na watumishi wa umma.
Wateja wa benki hiyo wameanza kunufaika na punguzo hilo tangu wiki iliyopita pindi menejimenti iliporidhia kufanya mabadiliko hayo.
Akizungumza na Mcl Digital leo Mei 13, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk Charles Kimei amesema mabadiliko hayo yanalenga kumpa mteja unafuu wa kukamilisha malengo yake kwa wakati.
“Punguzo hili linatolewa kwenye matawi yetu yote. Tangu wiki iliyopita huduma hiyo imeanza kupatikana,” amesema Dk Kimei.
Watumishi wa umma ambao awali walikuwa wanafanya marejesho mpaka miaka sita ambayo ni sawa na miezi 72, sasa wanaruhusiwa kufanya hivyo mpaka miezi 84 au miaka saba wakati wafanyakazi wa sekta binafsi waliokuwa na miaka mitano wameongezewa mpaka miaka sita.
Hatua ya CRDB imekuja baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kushusha riba ya mikopo inayotoa kwa benki za biashara mara mbili mfululizo.
Machi mwaka jana, ilipunguza riba hiyo kwa asilimia nne kutoka asilimia 16 mpaka 12.
Mwaka mmoja baadaye, BOT ilipunguza tena kwa asilimia moja na kushusha kiwango cha akiba ambacho benki hizoa zinatunza kwake kutoka asilimia 10 mpaka nane ili kuzipa uwezo zaidi wa kuikopesha sekta binafsi.
Chanzo: Mwananchi
Hawa jamaa kama vinyesi, hamna kitu.ila crdb wasidanganye watu benki pekee iliyoshusha riba ni BankABC ambayo riba ni 11% wao wanaweka kiini macho
Pumba tuHongera JPM watakuelewa tu.
Bank zilikuwa zinatumia fedha ya Serikali kuikopesha Serikali
Hii ni biashara kama biashara nyingine sio msaada.HAKUNA KILICHOPUNGUZWA HAPO... NI UHUNI TU.. MIAKA IMEONGEZWA 7 TOKA 6.. NA RIBA WAMEPUNGUZA TO 17% KITU NI KILE KILE.. FANYA MATHS UTAONA AT THE END UNALIPA KILE KILE AU ZAIDI. Riba bado kubwa mno mnoooo... mnoooooo... 17% kwa 7 yrs..? Banks zingeweza toa kwa 11% na kupata faida kubwa kwa sbb:
1: watapata wateja wengi sana wakishusha riba to 11%
2: kama BOT wamewashushia banks riba hadi 8% na banks binafsi ikamkopesha mwananchi kwa 11% ana faida ya 3%... Hiyo 3% ni kubwa sana sanaaaa sbb wakishusha to 11% watapata wateja wengi sana na faida yao ya 3% itakuwa kubwaa ..
17% bado kubwa mnoo mnoooooo... Hakuna kitu hapo
Mhhmm hebu fafanua nduguNa ifahamike kuwa hiyo 17%,kwa miaka 7 inakuwa 67%.
Hii hesabu ya riba unaipataje kwa miezi 12,24 au 36Absolutely right! Rejea jedwali la BancABC (BancABC) mikopo ya mwaka 1, 2, na 3 (miezi 12, 24, 34). Kwa mfano, ukichukua mkopo wa TZS. 35,000,000 hesabu yake inakuwa kama ifuatavyo:-
Kwa miezi 36: 1,282,960.70 x 36 = 46,186,585.20 (benki inachukua 46,186,585.2 - 35,000,000 = 11,186,585.20)
Kwa miezi 24: 1,764,301.60 x 24 = 42,343,238.40 (benki inachukua 42,343,238.40 - 35,000,000 = 7,343,238.40)
Kwa miezi 12: 3,225,480.24 x 12 = 38,705,762.88 (benki inachukua 38,705,762.88 - 35,000,000 = 3,705,762.88)
I have now got the concept; mikopo ya muda mrefu ni balaa. Na walivyo, they never clarify this to customers! Some sort of utapeli fulani.
Pole sana.. vp huwezi pambana ili ulipe kiasi kilichobaki bila riba kama utamudu lakini.. kama ishalipiwa 20millions unalipa 10 fasta bila ribaMi sirudii tena kukopa mikopo ya bank ya muda mrefu....
Nilichukua mkopo WA nyumba ktk bank moja, wakati huo sikuwa hata na elimu Sana ya mikopo na wao hawakunielewesha kivilee...
Sasa ni mwaka WA tisa naingia mwaka WA kumi, mkopo WA 35 mil, Nikihesabu hadi 2020 nitakua nimelipa jumla ya 80 mil! Roho imeniuma ila Sina jinsi...ila tena nikifikiria ingekua Si huu mkopo labda nisingekuwa na hiyo nyumba pia hapo ndo napata kamoyo kidogo ila kiukweli sio poa kabisa hiyo mikopo, ni shida! ..
Sent using Jamii Forums mobile app