Benki ni Dalali kati ya Watu wa makundi ya daraja la chini,daraja kati la kipato dhidi ya Matajiri

Jemedal_bin_chichi

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
539
579
Jina la Makala: The brilliant Definition of a Bank

Mwandishi: _Anil Gupta, CEO Kunashi India Limited_

Mchambuzi: Frank-Mromba Prosper 'don_prospa'

MAANA ADHIMU YA BANK

Mwandishi anaanza kwa kusema: Benki ni Dalali kati ya Watu wa makundi ya daraja la chini,daraja kati la kipato dhidi ya Matajiri.

Watu wa daraja la chini, daraja la kati, wanaotajwa hapa ni Wafanyakazi( employees) na Kundi la Matajiri linalotajwa hapa ni Wafanyabiashara, Wamiliki wa Biashara, wajasiriamali na Wawekezaji.

Mwandishi anasema kuwa, Mahali pekee, ambapo, makundi haya mawili, wanakutana ni Benki Tu!

Mwandishi anaendelea kusema kuwa, Watu wa daraja la Chini na daraja la kati kimapato, hupeleka fedha zao Benki, kwa lengo la kuweka Akiba( saving), na Matajiri Huichukua Fedha hiyo kwa Njia ya KUKOPA. Watu wa daraja la Chini na la kati, Huweka Akiba ya Fedha zao kwa sababu, wana Fedha nyingi Kuliko Uwezo wao wa Kufikiri. Kwahivyo, huhifadhi pesa zao Benki na hurudi majumbani mwao wakifikria ni nini cha kufanya na Fedha zao zilizopo Benki.

Kwa upande mwingine, Watu Matajiri, wanakuja Benki na kuzichukua hizo Fedha kwa mtindo wa Kukopa, Hii ni kwa sababu, Matajiri, wao Wana Mawazo( ideas) kibao kichwani, kuliko kiwango cha Fedha walizonazo.

Mwandishi anatoa ushahidi, kwa kuuliza swali kwa kusema, Kama unakataa hili, Hebu, tafadhali, Nionyeshe japo mtu mmoja katika Nchi yako, aliyewahi kuwa Bilionea au hata milionea, kwa kuweka Fedha zake Benki kwa njia ya Saving. Na Mimi nitakuonyesha mamilioni ya Wahindi au hata nje ya India ambao, wameweka Fedha zao benki kwa kufanya Saving, na bado wanaishi nyumba za Kupanga, huku kundi la Matajiri, wakijenga Majengo ya Kifahari kupitia Fedha waliokopa, zilizowekwa Benki kama Saving na kundi la Watu wa daraja la chini na daraja la kati!
 
Back
Top Bottom