Benki na ATMs ambazo zipo kwenye Malls na Supermarkes

Chief

Platinum Member
Jun 5, 2006
3,442
2,953
Si mara chache, kwenye Malls na Supermarkets, huwa kuna upungufu wa fedha kwenye ATMs, na ukitaka kutoa fedha ili ukafanye manunuzi kwenye baadhi ya maduka ambayo hayapokei kadi za Visa, unakwama. Hi adha huwa inaonekana sana nyakati karibia na sikukuu, mfano Iddi, Chrstmas etc wakati watu wakifurika kwa wingi kwenye maduka haya. Aidha, si watu wengi waliozoea kutumia kadi hizi kwenye kufanya manunuzi kwenye maduka haya. Wengi wetu tunapendelea kulipa kwa pesa taslim.

Wazo ambao ninalo na nafikiri kwa technologia iliyopo, linawezekana, ni kuwa hizo ATM machines wakabidhiwe wenye maduka hayo, mfano Nakumatt, ambapo mauzo yao ya pesa taslim (notes) wataweka kwenye machine hizo. Machine hizo zinakuwa configured kwamba mtu ukitoa pesa hapo, account yako ndo itatoa hela na akaunti ya Mall hiyo inaingiziwa hela. Kwa mtindo huu, itakuwa nadra sana kwa ATMs kuishiwa na fedha, na benki husika itaongeza mapato kwa bank charges na kupunguza gharama na ku replenish hizi machine na risks associated ya kusafirisha pesa nyingi, na wenye Malls hawatakuwa na haja ya kupeleka hela zao benki na mauzo kuongezeka. Haya jamaa wa IT depts wa banks!! Wazo hilo.
 
Unaweza kununua bidhaa kwa kutumia kadi yako ya benki, nadhani hiki ndo ulichotaka kuzungumzia.
 
Kwa wazo lako hilo nafikir pia Mkeo/Mumeo akabidhiwe boss yaani akishikwa ashki ofisini boss iwe ruksa kumpunguza hizo ashki hivyo kuongeza UFANISI kazini.
 
Wazo halitekelezeki hili

And that's the challenge we have in Tanzania....changing our mindsets. Kuna vitu vingi sana technology ingeweza kutusaidia kama taifa. Lakini bado wengi tunaogopa mabadiliko (tofauti na mazoea).
 
Back
Top Bottom