Benki Kuu yachapisha noti mpya ya shilingi 2,000 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Benki Kuu yachapisha noti mpya ya shilingi 2,000

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kakalende, Aug 30, 2009.

 1. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,260
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sijui kwanini wasibadili zote tusahau saini za MAFISADI kwenye pesa yetu?

  Benki Kuu yachapisha noti mpya ya shilingi 2,000

  Date: 8/29/2009
  Na Burhani Yakub  BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa noti mpya za Sh2,000 ambazo zitatumika sanjari na zilizopo kwenye mzunguko kwa sasa.

  Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alisema jana kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba, lengo la kutoa noti hizo mpya ni kukidhi mahitaji yake kwenye mzunguko wa fedha nchini.

  "Noti hizi mpya zinatofauti moja tu na zile ambazo zimo kwenye mzunguko kwa sasa nayo ni saini zilizopo.

  Saini zilizopo kwenye noti mpya ni za Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania,” alisema.

  Profesa Ndulu alisema kuwa noti hizo bado zina rangi ya kahawia, zikiwa na michoro inayoonyesha mandhari ya kitanzania kiuchumi, kiutamaduni pamoja na urithi wetu na mazingira.

  "Mbele ya noti, bado kuna picha inayoonyesha utajiri wetu wa kuwa na mojawapo ya wanyama pori wakubwa yaani simba ,alama ya kificho ya twiga ambayo bado ipo kama ilivyo katika noti nyingine zinazozunguka sasa" lilifafanua tangazo hilo.

  Alama nyingine zilizopo katika noti hiyo ambazo hazina tofauti na iliyopo kwenye mzunguko ni nyuma ya noti kuna picha inayoonyesha picha ya ngome kongwe illiyopo Forodhani jijini Zanzibar.

  Vile vile, alisema zina picha ya kinyago cha kuchonga na alama ya usalama inayobadilika rangi ikigeuzwa.

  ”Benki kuu inawashauri wananchi kuwa hakuna haja ya kubadili noti hizo kwani thamani yake ni ileile na kwamba haina mpango wa kuzifuta zilizokuwepo katika mzunguko wa awali.


  SOURCE: Mwananchi
   
 2. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,106
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  ila sioni kama BOT walikuwa na sababu ya kuchapisha noti mpya kwa sasa
   
 3. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,546
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  au ndio maandalizi ya uchanguzi..............mianya ya EPA labda imeziba!
   
 4. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,106
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  mkuu ilo linawezekana
   
 5. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  2010 imekaribia sana, vitafanyika vitu vingi sana.
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,577
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  Hiki ni kichekesho kingine cha design ya kifisadi??!!!! Kwani wametoa sababu zipi zilizopelekea kuchapisha note nyingine wakati ya 2,000 ipo na haina tatizo??? Nilifikiri labda wangefikiria 5,000 na 10,000 ambazo zinarudufishwa kila kukicha!!! Ohhh 2,000 ni minimal face value ambayo ni rahisi ku-tip maskini wa Tanzania!!!?? Maandalizi hayo????? Tehe tehe tehe tehe. Je tutafika kwa mtindo upi wakuu???!!!
   
Loading...