charles mususa
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 297
- 144
Profesa Benno Ndullu
Gavana
Beni kuu ya Tanzania
Sub: Huduma za Benki zitazamwe upya
Mh. Proffesa
Kwa niaba ya watumiaji wengi wa benki naomba kutoa dukuduku langu kufuatia matatizo mengi ya huduma za kibenki.Watumiaji wengi wa huduma za benki Tanzania wamegeuzwa wahanga na kuwa watumwa wa mabenki hayo huku msimamizi Benki Kuu ya Tanzania wakiwa kimya wakati wateja wa benki wanaumizwa na mambo mengi ya huduma za kuumiza wateja zinazotolewa na benki hizo.Wateja wanaumizwa na mabenki kwa riba kubwa ambazo zinapangwa na mabenki kwa faida kubwa zinazowafaidisha wao.Mabenki yanatoza riba mengine mpaka 30, kwa mikopo na benki kuu imekaa kimya.Ukiacha upande wa mikopo fees/bank charges zinazotozwa kwenye deposit zimekuwa ni kubwa mno si ajabu mtu aliyeweka pesa yake benki kwenye saving deposit akaunti akijisahau kidogo atakapoenda akakuta pesa hiyo imepungua sana au imeisha kabisa na kwenda kwenye negative kwa sababu ya kinachoitwa bank charges.Kinachotokea ukiweka pesa yako wao wanailamba tena bila aibu.Mimi nimekuletea pesa yangu unaitumia kwa biashara yako na sipati chochote bado pesa hiyo unaipunguza kwa gharama zinazoitwa ledger fees au jina linalofanana na hilo je huu umekuwa wizi mwingine. Je ni kwa nini loan interest za benki na microfinance haziwi regulated nadhani inabidi tuliangalie hili.
Kwenye mikopo ndio sasa ni balaa benki ,wakati mteja anapokopa mikopo mingi ya mikopo gharama ya riba haiendani na ulipaji wa mkopo kwani kwa uelewa wa kawaida marejesho na riba yanapaswa kupungua lakini formulae zao ziko compounded mtu anakopa milioni let say 90 wakati mkopo unaonekana kupungua kila mwezi kwa marejesho na riba, kiasi cha marejesho na riba hakipungui mpaka mteja anapomaliza mkopo huu ni ujanja wa kuwaumiza wateja .Mfano nimekopa milioni 90,000,000 na marejesho na riba labda ni 3,000,000 basi kiasi hicho kitaendelea kulipwa kwa muda wote japo kwenye repayment schedule mkopo utakuwa unapungua , swali kama mkopo unapungua kwa nini kiasi cha kulipa ni kilekile? nazinauza nyumba za watu , imekuwa kama wateja waliokopa benki ndiyo wameenda kumwambia Magufuli achukue pesa za serkali na kuzipeleka benki kuu.Hawajali tena kama biashara zimevurugika na wanapaswa kuwasaidia wateja wao ambao nao kama wao benki walivyovurugwa na wao biashara zao zimevurugika.Sasa hivi ni afadhali kukopesha kwa vikoba na SACCOS kuliko kuhangaika na mabenki, pia ni shida kuendelea kupeleka pesa benki wakati pesa hiyo eventually benki wanajifaidisha wenyewe.Watumiaji wa benki tuweni macho tujikomboe