Benki Kuu ya Tanzania tafadhalini ingilieni kati madeni ya Wananchi

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
Benki Kuu ya Tanzania tafadhalini ingililieni kati madeni ya watu wanayodaiwa na benki kwa muda hata wa miezi 3 tu.

Kuna mameneja wa baadhi ya bank sio waminifu hawataki kuwasikiliza wateja wao wanaodaiwa hata kipindi hiki cha huu ugonjwa wa Corona.

Kuna baadhi ya watu unakuta walikuwa wanadaiwa Tsh. milion 400 wamelipa Tsh. milioni 390 imebaki milion 10 tu lakini mameneja wa benki wanataka kuuza mali za mteja.
 
Huko mbeleni mameneja wa bank wenye tabia hizo wasipoacha uhuni wao tutawataja kwa majina pamoja na bank zao
 
Kama bili za maji na umeme serikali kuu inashindwa kusamehe wananchi wake kipindi hiki cha Korona.

Wewe unawaza kusamehewa marejesho ya mkopo uliokopa kwa raha zako?

Tupo kwenye right track tembea kifua mbele na uchape kazi kwelikweli.
 
mi nina mkopo na kila rejesho nalipa bila shida,

Unaelewa maana ya janga lakini? Tunaongelea jamii au wananchi kwa ujumla.

Hii hoja iangaliwe kwa umakini namna ya kuwasaidia watu. Kuna tofauti kubwa sana mtu aliyekopa kwa kutegemea marejesho ya mshahara na yule anaefanya biashara,huu ugonjwa unesababisha biashara nyingi kudorora, hiyo imeathiri mapato na hali kadhalika marejesho ya mikopo ya wafanya biashara.

Kuna mabenki wameshawatumia aarifa wateja wao kusamehe marejesho kwa miezi mitatu, ikimaanisha muda wa marejesho utasogezwa mbele zaidi kufidia marejesho ya hichi kipindi.

Ushauri, unapochangia hoja, iangalie kwa mapana yake kwa maslahi ya taifa.
 
Mfano mtu alikuwa amekopa biashara yake ni bar au hotel ya kitalii je atawezeje kulipa mkopo wake?

Sina maana biashara zingine haziathiria hapana nimetoa Kama mfano tu
 
Mkuu.

Usitegemee huruma yoyote ya hii serikali, pambana mwenyewe nyumba itauzwa.

Serikali haijasimamisha shughuli zozote za kiuchumi. Hakuna LOCKDOWN wala CURFEW sasa hapo unategemea huo Mkopo watausimamisha kwa gia gani wakati wanaona shughuli zinaendelea kama kawaida ?

Kwenye mambo ya pesa kaa mbali na Magufuli hakupi hata MIA MBOVU hata kama unastahili na haki yako
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom