Benki Kuu ya Tanzania imetolea ufafanuzi alama zilizoko kwenye noti zetu hasa alama ya nyoka kwenye noti ya Shilingi 500

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,904
MAELEZO KUHUSU BAADHI YA ALAMA KATIKA NOTI NA SARAFU

Kumekuwa na mijadala kuhusu alama zilizopo katika noti na sarafu za Tanzania, hususan alama ya nyoka inayoonekana kwenye noti ya shilingi 500. Benki Kuu ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:

Utengenezaji wa noti na sarafu za nchi yoyote ile huanza baada ya kukamilika kwa mchakato wa usanifu na michoro ya fedha husika.

Usanifu huo unahusu, michoro na alama mbalimbali ambazo zinaelekeana na nchi husika.

Katika kutekeleza jukumu la kuamua nini kitumike au kisitumike katika kutengeneza fedha, nafasi ya wananchi huzingatiwa. Hapa nchini, Benki Kuu ya Tanzania ina jukumu kubwa katika maamuzi hayo.

Alama za kawaida katika noti na sarafu nyingi hapa duniani ni kama picha za watu mashuhuri, picha zinazoonesha shughuli za kiuchumi, mali asili kama milima na maziwa, majengo marefu na wanyama.

Alama na michoro inayokuwa katika noti na sarafu ina maana halisi ili kuepusha tafsiri potofu ambazo zinaweza kutokea.
Ni wajibu wa Benki Kuu ya Tanzania kuhakikisha kwamba picha, michoro na alama zozote zinazoleta ukakasi zinaepukwa.
Kiwango cha elimu na namna ya utunzaji wa pesa kinachangia namna fedha ilivyo pamoja na alama zake.

Inatakiwa namna fedha ilivyo na alama zake ziwe zinaelekeana na kuwa rahisi kuzitambua.

Hivyo, alama ya nyoka aliyejiviringisha katika fimbo ambayo inaonekana na katika noti ya shilingi 500, inamaanisha utoaji wa huduma za afya.

Hii ni alama ya huduma ya tiba inayotumika karibu duniani kote, zikiwemo taasisi za afya za hapa nchini na za kimataifa. Benki Kuu ya Tanzania iliweka alama hiyo katika noti ya shilingi 500 kuonesha umuhimu ambao serikali inaweka katika huduma za afya.

Upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi, wakiwemo watoto, ni suala ambalo linapewa kipaumbele na Serikali. Hili linajidhihirisha wazi katika mgawanyo wa bajeti ya serikali ambapo sekta ya afya inapata rasimali ya kutosha.

Imetolewa na:
Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
24 Agosti 2018
 
Kwa maelezo yao wao wameichukua wizara ya afya, je walaumiwe wizara au BOT?

Kuna vitu hata ujivike uwendawazimu utetezi wake ni mgumu sana! Nyoka itabaki kuwa. I alama ya shetani tu, na maana yake hatutakuja kuelezwa hadharani! Wso wanajua na wale wanajua!
 
Kwani ni lazima kuweka hiyo alama ya nyoka ambayo kwa kuonekana kwake kwenye noti jamii imekuwa na tafsiri tofauti zenye utata? Kama suala ni kuonyesha kwamba taifa linajali afya ya wananchi wake basi si bora wangeweka hata picha ya hospitali kubwa nchini mfano kwa sasa hospitali kubwa ya Mlonganzila au kitu chochote kingine kinachohusiana na mafanikio ya taifa katika utoaji wa huduma ya afya lakini kisicho na utata kitafsiri.

Mbona katika kuonyesha kwamba taifa linajali elimu kwenye noti hiyo hiyo ya 500 imeweka jengo la pale chuo kikuu cha Dar es Salaam na siyo alama nyingine yenye utata inayohusu utoaji wa elimu?

Vipi kuhusu uwepo wa picha ya majengo pacha ya BOT kwenye noti ya 10,000/= yaliyojengwa kifisadi ni alama au ishara ya kumbukumbu ya ufisadi uliogubika ujenzi wa majengo hayo au ufisadi kwa ujumla uliotapakaa nchini?
 
acha tanzania iendelee kuwa masikini tu maana watanzania wengi ni watu wenye akili finyu sana, kila kitu kwao ni uchawi/ushetani, vitu ambavyo havina uhalisia wowote. alama hiyo ya nyoka (mnyoo) iko dunia nzima kwenye sekta ya afya na haina uhusiano wowote na vitu vya kufikirika kama "shetani"

kwa ufupi:
huyo nyoka anaitwa "the rod of Asclepius", kwenye hekaya za kigirigi Asclepius alikua ni mungu wa uponyaji na tiba hivyo chimbuko lake ni ugiriki katika fani ya utabibu.


maelezo mbadala:
kuna watu wanaelezea huyo nyoka kuwa ni mnyoo, na kujikunja kwake kwenye huo mti kunawakilisha mchakato wa kumtoa huyo mnyoo kwenye mwili wa mgonjwa kama ambavyo hufanyika kwa mamia ya miaka
Dracunculus_medinensis.jpg

mnyoo unavyotolewa mwilini mwa mgonjwa

440px-Flag_of_WHO.svg.png

bendera ya WHO
 
Watoe alama ya nyoka waweke picha ya" Sewahaji" yule "Founder" wa Hospital ya Muhimbili!
 
acha tanzania iendelee kuwa masikini tu maana watanzania wengi ni watu wenye akili finyu sana, kila kitu kwao ni uchawi/ushetani, vitu ambavyo havina uhalisia wowote. alama hiyo ya nyoka (mnyoo) iko dunia nzima kwenye sekta ya afya na haina uhusiano wowote na vitu vya kufikirika kama "shetani"
We jamaa nae ni shida tu yaani ile alama ya nyoka we unaona ni mnyoo? Mnyoo gani unaopanda kwenye mti rafiki yangu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna mtu aliwahi niambia kuwa magambo ya nyoka aina ya Anakonda ndo hutumika kutengeneza noti, ndo maana hata uifulie kwenye jinsi noti haiwezi kuharibika.
 
Yule ni mnyoo na sio nyoka,na huo mti aliyojiviringisha ndio uliotumika kumtoa mwilin mwa binadamu,kwa wale waliopitia Medical school wanaelewa vzr somo la Parasitology....hiyo ilikua tiba miaka ya zamani kabla science ya tiba haijakuwa.
 
Kwanini wasiweke kitu ambacho ni rahisi kila m TZ kukielewa,wangetuekea sindano na panadol
 
Back
Top Bottom