Benki Kuu ya Tanzania(BoT) yahamisha Mali na Madeni ya Bank M kwenda Azania Bank Ltd

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,877
Tunawakaribisha katika mkutano wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Waandishi wa Habari (Press Conference) unakaofanyika Benki Kuu jijini Dar es Salaam Jumanne tarehe
15 Januari 2019 saa 4.30 asubuhi.

Mkutano huu ni muhimu sana.
Imetolewa na:

Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
Januari 14, 2019

======

UPDATES:

11:15hrs Mkutano Unaanza.

76BA980E-4EE3-4D57-88BD-C52873A6A742.jpeg


Naibu Gavana Benard Kibese ndo msemaji mkuu kwa niaba ya Gavana

Rafael Naibu Gavana

Kibese:
Kama mnavyojua, Sheria ya fedha imeipa Benki Kuu ya Tanzania kusimamia shughuli zote za fedha nchini. Kutoa leseni kwa benki na taasisi za fedha.

Katika kutekeleza mamlaka yake, Benki Kuu ya Tanzania iliamua kuiweka chini ya uangalizi Bank M 2/8/2018 baada ya kupungukiwa ukwasi.

Bank M ilipewa leseni hapa nchini mwaka 2008.. Bank M ilikuwa na Matawi matano na mtaji wa Trilioni moja.

Kabla ya kuiweka chini ya uangalizi, Benki Kuu ilifanya mikutano ya mara kwa mara na Bank M. Pamoja na kupewa muda wa kutosha, jitihada hizo hazikuzaa matunda. Iliwekwa chini ya uangalizi kwa siku 90 na mnamo 2/11/2018, Benki Kuu iliongeza muda kwa siku 60.

Benki Kuu ya Tanzania inautaarifu umma kwamba, kwa mamlaka iliyopewa kwa sheria ya mabenk na taasisi za fedha kwamba mchakato wa kupata ufumbuzi juu ya bank M umekamilika.

Mali na madeni ya benk M yatachukuliwa na benki nyingine..

Benki Kuu imeamua kuhamisha kwa mujibu wa sheria mali na madeni ya Bank M kwenda Azania Bank Ltd. Kwa sasa bank kuu na Azania wanaendelea kuandaa taratibu za kisheria za kuhamisha Mali na Madeni kwenda Azania.

Wateja wenye amana na wadai wengine wa Bank M watataarifiwa ni lini watapata huduma kupitia Azania. Na wale wenye mikopo wanatakia kuendelea kulipa mikopo yao kulingana na mikataba yao, na Benki kuu italisimamia hili kwa karibu.

Mtaji wa Azania unatarajiwa kufikia kiasi Shilingi za kitanzania bil 164 kiwango ambacho ni cha juu sana. Mtaji unaotakiwa kiaheria ni bil 15.

Benki Kuu ya Taanzania itaendelea kulinda wateja wenye amana nchini. Tutaendelea kuimarisha uhimilivu katika sekta ya benki nchini.

Kwa wale ambao ni shareholders na wanadaiwa na Bank M wafike Benki Kuu ndani ya siku saba ili tukae pamoja tufanye makubaliano. Lakini kwa wengine wote wanatakiwa kwenda Azania Bank.

Mkurugenzi wa Azania atakapokuwa tayari atawaita na atutangazia umma ni lini wanafungua mlango kwa umma.

54253AF8-5FFF-4E2C-BE6D-71647353489A.jpeg

5B347D06-9960-46BB-9B24-38F57907E3C1.jpeg


SWALI: Hii ni benki karibu ya tatu kushindwa kutoa huduma ni nini tafsiri ya uchumi?

JIBU: Uchumi wa nchi unaimarika ikiwa na uimara wa taasisi za fedha. Ndo maana Benki Kuu ipo pale kuvisimamia hivi vyombo vya fedha. Benki inapoonekana kutetereka, Benki Kuu inaingilia kati kulinda amana za wateja.

MASWALI ZAIDI: Ni masharti yapi Bank M mlikuwa mmewapatia wakashindwa kuyatimiza? Hakuna kifungu cha sheria cha kuwasaidia hao Bank M kurudi hewani? Benki Kuu mna hela, kwanini msiwasaidie? Ni benki zipi nyingine zinaelekea kufa? Kwa miaka 10 ilikuwa na tril 1 lakini wamekuja zero? Kwanini?

MAJIBU:
Hizi lugha kidogo kuna kuchanganya. Asset ni mali. Ukwasi ni liquidity. Kwenye swali lako umechanganya. Hili tunalosema tril 1 ni mali sio ukwasi. Umesema tunatoa kwenye ukwasi wa 1 tril tunapeleka kwa 1 bil. Hizi data sio sahihi.

Benki yoyote inaweza kuanguka kwa sababu mbili; Inapoendeshwa kwa chini ya mtaji na Mtaji ukienda chini ya bil 15 utaanguka tu. Benki Kuu haipendi uanguke, itafanya juhudi mbalimbali usianguke.

Ukwasi ndio umeifanya Bank M ikatetereka na kujikuta ipo chini ya kiwango kilichowekwa na sheria hadi ikawa inashindwa kulipa madeni yake. Bank M haikuwa na uwezo wa kulipa madeni

Ukwasi wa Benki unaweza ukateteleka hadi ndani ya siku moja.

Vifungu vya kusaidia bank isianguke: Kama nilivyosema, Benk Kuu ilifanya juhudi mbalimbali ili kuinusuru Bank M. Tulifanya vikao vya wamiliki, wakurugenzi kwa muda wa mwaka mmoja tunatafuta namna gani tuinusuru. Benki Kuu inaingilia kati kumnusuru mteja wa nje, mimi na wewe ili wasitumie na kile chako. Yaani tusipoingilia, wanaweza wakaanza kutumia kile ulichoweka benki. Ili isifike hapo ndo maana Benki Kuu tunaingilia kati.

Benki gani nyingine: Kama kungekuwa na Benki nyingine inaelekea kibla tungeutangazia umma. Bank M haikiwa imekufa wala haikufilisika lakini ilikuwa inaelekea huko.

SWALI: Ni masharti yapi wameshindwa kutekeleza?

JIBU: Wameshindwa kufikia kiwango cha ukwasi kisheria.

MASWALI ZAIDI: Shareholder mmewapa siku 7, hamuoni sasa kutizima sheria upande wa mikopo? Inaonekana Bank M mikopo imeinyonga. Mtafanyaje? Je, hamuoni mmeibebesha mzigo mzito Azania Bank?

Naibu Gavana:
Bank M haijawa at liquidation point. Ingefikia, ingewekwa chini ya mufilisi na Benki Kuu ingeteua mufilisi.

Bank M kupelekwa Azania haikuwa sababu ya madeni. Tatizo kubwa la benk M ni Ukwasi wa kutosha. Madeni ya Bank M yalikuwa ni Bilioni 618 na hili kwa benki sio tatizo.

Benki Kuu inafanya juhudi zote ili kumlinda mteja ili benki isife.

Mkurugenzi Mkuu atakapokuwa amekamilisha makabidhiano, atafungua milango na kama ukikwama Bank M, Azania watakuhudumia. Yote haya tuyafanya kumlinda mtu wa chini.

Shareholder ni mwenye mali, mmiliki. Wamiliki wa ile Benki wao wanaweza wakakopeshana mle ndani. Waje watuambie namna watalipa hayo madeni. Wapo wengi tu... (anawataja)

4955777B-1452-4F6B-B7A9-3A9A44375A5A.jpeg

DEA1982D-DB87-4157-B2A3-CFDA2AF055AB.jpeg


NOTE: Wana hisa hawa wanatakiwa waende BoT waseme watalipaje hela walizokopa Bank M. Hawa aliowataja ni Shareholders waliokuwa na mikopo. Wanatakiwa kwenda ndani ya siku saba za kazi kuanzia kesho.

Naibu Gavana: Wamiliki wa Bank M walikuwa na mikopo ya ndani. Kuhamishia Bank M sio kichochoro cha wao kukwepa!

Bank M kupelekwa Azania Bank ni neema sio mzigo. Azania ilikuwa ni Bank ya kati kabla na kwa utaratibu huu Azania inaenda kuwa moja ya Benki tano kubwa Tanzania kwa kuwa na mtaji wa kutosha na ukwasi wa kutosha.

Benki yoyote inaitwa Benki na inapata faida kutokana na mikopo. Kuna mikopo mizuri na mikopo mibaya. Bank M wateja wao walikuwa wanalipa na tulipoweka chini ya uangalizi wa BoT tumeweza kukusanya Bil 42.

Bank M ilikuwa ni Benki ya wateja wakubwa, Azania ilikuwa na wateja wadogo na wakubwa, hivyo haitishwi mzigo hata kigodo. Naomba nitoe wasiwasi umma wa watanzania.

Sasa hivi azania inaingia kwenye kundi moja la Benki kubwa kama NBC, NMB, CRDB nk. Wateja wasije wakaikimbia Azania kwamba imetwishwa mzigo!
 
Ngoja nikafukue pesa zangu nilizokuwa nimezichimbia chini, niziwahishe benki, wanabadili note za elfu 10, uwiiiiii itakula kwangu.
 
Asante sana mkuu, huu mkutano ni very critical, nchi za wenzetu Gavana akiwa anaongea nchi nzima inasimama kwani kauli yake inaathiri kila kitu kuanzia masoko ya mitaji hadi riba za kukopa na uwekezaji.

Tafadhali endelea kutupatia updates

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo ni kwa nchi zenye kuheshimu utawala wa sheria lkn kwetu ni kinyume chake

In God we Trust
 
Kwanini wanahangaika?! Wafunge bank zote tuweke pesa majumbani. Waliifungua yao (TPB) lakini wananchi sijui hawaielewi naona kama haina wateja vile. Nadhani sasa tutalipuwa mishahara BOT moja kwa moja.
 
Hizo ni kwa nchi zenye kuheshimu utawala wa sheria lkn kwetu ni kinyume chake

In God we Trust
Mkuu hamia huko kwann ujisumbue kuishi nchi yenye kuongoza kwa kutoheshimu utawala wa sheria!!!

Sasa wewe umekutwa na kichaa unaogelea mtoni ama baharini halafu akachukua nguo zako ukaanza kumkimbiza ukiwa uchi sjui hapo kichaa atakuwa nani!!!

Ya nini ujipe adhabu!!!! Hamia huko ambako wananchi wake wanakula utawala wa sheria... Wameajiriwa na utawala wa sheria,, nchi imetulia hakuna cha vita wala vitisho kwani kuna utawala wa sheria.. Nenda ndg huko ambapo watu hawafanyi chaguzi kwani kuna utawala wa sheria ya nn sasa kufanya uchaguzi nenda mkuu nendaaa ambapo huko utakula, utakunywa na utaropoka kw uhuru kbsa kwani utawala wa sheria upo,,,,

Nenda kbsa ndg kwenye nchi ya utawala wa sheria ila ukiendelea kuishi Tanzania nchi ambayo kila siku ina vita,, watu hawana chakula, na hakuna kbsa utawala wa sheria utaishia kuugua madonda ya tumbo nendaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona bado upo jikoni unaota moto maana kama kila anayejiunga JF ukaamini kama yupo bongo basi nakupa pole sana
Mkuu hamia huko kwann ujisumbue kuishi nchi yenye kuongoza kwa kutoheshimu utawala wa sheria!!!

Sasa wewe umekutwa na kichaa unaogelea mtoni ama baharini halafu akachukua nguo zako ukaanza kumkimbiza sjui hapo kichaa atakuwa nani!!!

Ya nini ujipe adhabu!!!! Hamia huko ambako wananchi wake wanakula utawala wa sheria... Wameajiriwa na utawala wa sheria,, nchi imetulia hakuna cha vita wala vitisho kwani kuna utawala wa sheria.. Nenda ndg huko ambapo watu hawafanyi chaguzi kwani kuna utawala wa sheria ya nn sasa kufanya uchaguzi nenda mkuu nendaaa ambapo huko utakula, utakunywa na utaropoka kw uhuru kbsa kwani utawala wa sheria upo,,,,

Nenda kbsa ndg kwenye nchi ya utawala wa sheria ila ukiendelea kuishi Tanzania nchi ambayo kila siku ina vita,, watu hawana chakula, na hakuna kbsa utawala wa sheria utaishia kuugua madonda ya tumbo nendaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we Trust
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom