Benki Kuu Iwamulike akina Madoff wa TANZANIA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Benki Kuu Iwamulike akina Madoff wa TANZANIA

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mwanaukweli, Mar 19, 2009.

 1. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2009
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Benki Kuu ina habari kama kuna Ponzi Schemes hapa Tanzania?

  Watanzania wanawekeza kwa wingi, wanaweka matumaini yao yote hapo, na wanaacha hata kazi za uzalishaji kwa matumaini ya Ponzi schemes kama za DECI.

  Je DECI ina uhalali Tanzania? Je Ponzi Scheme zinakubalika Tanzania? Lakini hatuwezi kujifunza kwa matukio ya huko kwa wenzetu?

  Wana JF maoni yenu.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Utaambiwa huwatakii watu neema bure.This is a ticking bomb.
   
 3. K

  Komavu Senior Member

  #3
  Mar 20, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 114
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35

  Mkuu your very right. hii DECI its purely a Ponzi Schemes na watu wanaikimbilia huku wakidhani itawatoa fasta kama zilivyo ndoto za wengi.

  Mbaya zaidi wengi wanaojiunga huko DECI uelewa wao ni mdogo na hata
  hawajui hiyo DECI inaendeshwa vipi. I am very sure hii kitu italeta tafrani
  muda si mrefu na wamiliki watavarnish.

  Wengi wanasikia tu bwana madoff amesababisha hasara ya mabilioni kwa
  wawekezaji lakini how sidhani kama wako very much aware. Mbaya zaidi
  wakina mama wa nyumbani ndo wanaipenda sana hii kitu DECI, .
   
 4. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Makao makuu yao yapo Mabibo Mwisho kwenye numba ya mama Kiwia. Company registration ni 61334 iliyotolewa 25/7/2007. Wanayo barua ya BOT wanayodai inawatambua na kuwaruhusu kukusanya fedha yenye Ref. DBS/B20/100/Voll. II/6. Simu za BOT zilizoonyeshwa kwenye barua hiyo ni 2110036, 2118021 na 21398161. Hii ya mwisho inaonekana imekosewa na hizo nyingine ukipiga unajibiwa ' namba hiyo haipo'.
  Nimejaribu kufuatilia BOT lakini kote nimekuwa directed sehemu mbalimbali, mara piga simu hii mara ile, hakuna aliyekiri kutoa barua hiyo.
  Kwa kufuatilia kumbukumbu (REF) ya barua hiyo, nadhani DBS stands for Director of Banking Supevision. Kwa kuwa ndani ya kitengo hiki kuna Deputy director - nonbanks supervision; nadhani ofisi hiyo au kitengo hicho ndicho kimetoa barua hiyo. Wanapaswa wauleze umma kuhusu DECI. Namba za simu kutoka kwenye website ya BOT (Bank of Tanzania (BOT): Home Page : Benki Kuu ya Tanzania) zinaonyesha kuwa ni 2235528/9 na 2235552/3.
  Naomba wana JF walio BOT watuhabarishe zaidi.
  Nimeona pia registration yao ya TRA lakini sikujishughulisha nayo kwa kuwa wao TRA wanachojali ni kuwa unalipa kodi. Kwao source of income whether legal or illegal is irrelevant (ukisoma Income Tax act utaona wazi kuwa taxable income is icome derived from whatever source).
  TUHABARISHANE
   
 5. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  DECI.......!
  PEOPLE GET MONEY EASILY....!
  ASK FOR DECI AND JOIN DECI.....!
  kuna makampuni mengi ambayo yameliza kuanzia wafanyabiashara na hata wafanyakazi. EASY FINANCE, BAY PORT N.K MENGINE HUTOZA RIBA HATA 600%
  Lakini yote haya hayaonekani isipokuwa DECI ambayo till now NO COMPLAIN from its members....!
  Sisi tulio nje na DECI (other financial institutions) ndo hasa tunaolalamika kwani DECI ameonekana ni ''ASIYEPIGIKA'' na hizi sekta nyingine za kifedha, sasa wana hofu ya kukimbiwa na MEMBAZ WAO....!
  NINYI SEKTA NYINGINE ZA KIFEDHA RIBA ZENU ZIKO JUU, DHAMANA ZISIZOWEZEKANA KWA KCC, MASHARTI MAGUMU, NA UKIRITIMBA ULIOKITHIRI na hata atakaye mkopo kwenu maofisa wenu hutaka kitu kidogo katika mikopo tunayohitaji ....!
  waacheni DECI wazidi kuwapoka wateja wenu kwani mmeshindwa ku-meet teir needs....!
   
 6. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2009
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Bado data zote zinaonesha DECI ni Ponzi scheme. Hata hizo ulizotaja tutazichunguza. Kama nazo ni Ponzi scheme, jukumu la serikali ni kulinda raia wake wasidanganywe na wenye uroho wa utajiri kama akina Madoff, hivyo kama Ponzi scheme zinaendelea TZ na zinafahamika, si kitu cha kunyamaza.
   
 7. T

  Tango Member

  #7
  Mar 30, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Jamani kama tunaweza kufahamishwa hiyo DECI ni nini na inamilikiwa na nani. Ina wafanyakazi wangapi na kuwa wanaivest wapi. Nadhali kwenye hili jamvi wapo wanahabari wengi wanaweza kufanya uchunguzi Watanzania tukapata kuhabarishwa. Napenda tu kusema kuwa the fact kwamba financial institutions nyingine hazijatajwa ama 'kuandamwa" kama Bayport (Post No 5) ni kuwa tunaangali ishu iliiyopo sasa na kwa wakati huu, pia unaangalia inawagusa nani. Hii DECI inawagusa Watanzania wa chini sana ambao hawana uelewa wa mambo ya fedha wala biashara.Kwa hiyo mtu akiambiwa anatoa laki moja inazaa sijui asilimia ngapi kwa wiki 12 anaona dili si ndio hili? Haulizi je faida inatoka wapi ya kumlipa yeye na kuwa machale hayamchezi kama anaweza kuibiwa na kuwa anaweka kidogo kidogo.

  Mwaka jana nilikutana na maagent wa DECI Arusha walikuwa wanachonga risiti kwenye kona. Wakasema wameokoka wamempokea bwana na kuwa wameajiriwa na DECI na kuwa wao walitumwa kuanzisha DECI Arusha. Mimi kidogo ninauelewa mpana wa mambo ya fedha na jinsi zinavyoweza kuleta mkanganyiko kwenye uchumi. Nikawaomba contact zao wakanipa lakini bahati mbaya nilikuwa busy sana sikuweza kufuatilia Dar es Salaam na nikawa nimehama kituo cha kazi kwa muda. Mimi nikajiuliza mawili matatu nikaachana sikupata jibu. Kwanza ni organization gani ya kifedha inaruhusu branches zao za Arusha kutengeneza risiti kienyeji tu mitaani hata kama watendaji wake wamempokea Bwana? Na nikajiuliza mbona hawa jamaa wanasema wanakusanya hela nyingi kwa siku lakini hawana uelewa wa mambo ya fedha? Na niliwauliza sasa nyie mnatengenezaje hela wakasema tumekupa contacts nenda Mabibo.

  Sisi tunaojiuliza kuhusiana na hiki chombo cha fedha hatuna interest yeyote wala pengine si kwamba hatutaki watu wasipate hela lakini tunaona kuwa hela haziwezi kutengenezwa kirahisi namna hiyo kuna ujanja ujanja unafanyika. Sasa tunataka kuokoa watu wengi zaidi wasiingie kwenye mkumbo.

  Mfano mwingine.. Mwaka jana nilikutana na Mama mmoja Nairobi akanielezea ni jinsi gani anapata hela kupitia mfumo wa kuuza sijui bio disk. Unaingia unanunua Bio disk unawaambia na watu wengine wanne..unajenga pyramid wakifikia kadhaa unaweza kupata mshiko wako. Mimi nikamwambia kwa mfano nikiingiza watu wote wa Tanzania kwenye huu mfumo nitapata hela nyingi sana lakini kila mmoja atakuwa ametoa $500 kununua bio disck ambayo ni illusion tu wanasema sijui inatibu magonjwa gani na gani. Je nchi yangu itakuwa imeendelea kiasi gani? Haitakuw anchi ya wajinga kweli kuamini kila mtu anaweza kuwa na bio disk ili upate hela? Akaona nimemshtukia. Tulikuwa airport akasema anawahi ndege yake nikamwambia haya kwa heri ukipata muda nitumie e-mail uniambie zaidi. Sikuwa na contact zake na sijapata e-mail yake. Ninajua kuna watu wameshaingia mkenge Tanzania wa Biodisk..kama bado hujaingia kwenye huo mkenge jihadhari.

  Sasa jiulize mfumo wa namna hiyo hiyo kwenye hiyo DECI.
   
 8. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2009
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Mkuu Heshima zote nakupa.

  Hapo Mkuu unakataa kuangalia misingi. Ponzi scheme kawaida zinaanguka ghafla.

  Kawaida hakuna complaints from Ponzi members mpaka siku ambayo scheme inaanguka. Ndivyo ilivyokuwa ya Charles Ponzi 1920, ndivyo ilivyokuwa ya Columbia Desemba mwaka 2008, na ya Bernard Madoff aliyefungwa hivi karibuni.

  Unapojenga hoja tetea MISINGI ya DECI, kwani katika Finance, kawaida institution inayoahidi faida kubwa, pia ina RISK kubwa.

  PONZI scheme hatima yake ni KUANGUKA tu, suala ni kuwa itaanguka lini. Inapoanguka, hasara huwa ni kubwa kwa wanachama, ndio maana nchi nyingi hupiga marufuku, nasi tunajiuliza kama hapa kwetu ni Ruksa???
   
  Last edited: Mar 31, 2009
 9. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wazo hili ni zuri,lakini nani amfunge paka kengele?

   
 10. A

  Audax JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuweni waangalifu na Huyo DECI,Kinga ni bora kuliko tiba, Fanyeni kazi kwa bidii.Vya bure cku zote gharama yake ni kubwa saana.
   
 11. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2009
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Hatimaye BoT wametoa tamko lao. Angalia attachment hii hapa.


  Lakini baada ya kutamka nadhani wangechukua hatua kwa wahusika kama Madoff alivyoshughulikiwa USA.
   

  Attached Files:

  • deci.pdf
   File size:
   193.9 KB
   Views:
   44
 12. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2009
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  USA Bernard Madoff ameliza watu kwa investment scheme kama hiyo hiyo ya Deci, na amefungwa miaka 120.

  Kenya DECI hiyo hiyo imeliza watu!!!!!

  Shida si DECI wala waendeshaji, shida ni PONZI schemes. Tukubali kujifunza.

  A wise man changes his mind sometimes but ......
   
Loading...