Benki Kuu Imefanikiwa Kushusha Inflation Rate Lakini Imetuacha na Maswali Mengi!

Benki Kuu ya Tanzania inapaswa kupongezwa kwa jitihada za mara moja walizofanya kushusha mfumuko wa bei nchini, na pia kupandisha thamani ya shilingi ya Kitanzania. Katika miezi mitatu iliyopita mfumuko wa bei za vyakula umeteremka kutoka 27.8% mpaka 26.7% na inflation kwa ujumla (general inflation rate) imeshuka kutoka 19.8% mpaka 19.4%. Pia thamani ya shilingi ya Kitanzania imepanda. Kiwango cha kubadilisha dola 1 ya kimarekani kwa shilingi ya kitanzania ilikuwa 1900, leo hii ni 1598. Hongera Gavana Benno Ndulu kwa kazi nzuri. japokuwa nadhani huu ni mpango wa muda mfupi na tusiutegemee sana kama Taifa kuwa utadumu. Lengo likiwa kushusha mfumuko wa bei mpaka tarakimu moja kufikia June (ahadi ya BoT), kwa vyovyote vile inabidi muumize kichwa zaidi, na zaidi ya yote tuweke mipango ya muda mrefu ya kuimarisha uchumi wetu na hususani kupunguza imports. Je watafanikiwa, sijui, lakini ni matarajio na matamanio yetu kuwa watafika; tunawaombea dua. Wenzangu na mie wanashindwa kukuelewa ukiwapa hizi tarakimu, wao wanataka waone tu bei ya dagaa, maharage na sembe imeshuka maana wengi wao hata sukari haiwahusu sana. Je, tunaweza kukiri kuwa tumeshindwa kuzalisha misosi kiasi cha kutosha kushusha bei za chakula nchini? Ama tumeshindwa kutengeneza mfumo mzuri wa kusambaza chakula nchini kiasi kwamba watu wa nyanda za juu kusini wanakosa pa kuweka chakula ilhali Nzega wanakufa na njaa?

Mkuu Kigwangalla,

Ni lini exchange rate ya TShs/US$ ilifika shilingi 1900? Nimeangalia exchange rate ya kuanzia Januari 2009 mpaka juzi Ijumaa 22/3/2012, sikuona hiyo rate. Kwa kuhakikisha naomba angalia hapa: Bank of Tanzania: Financial Markets - Interbank Foreign Exchange Market (IFEM)

Data za IFEM ndio ambazo huwa zinatoa indicative exchange rate kwenye Bureaux de Change na mara nyingi ukiangalia selling rate ya BoT inaweza kukupa mwelekeo mzuri kwa kuongeza margin ya kama shilingi 100 kwenye selling rate.

Kwa hiyo credit yako ina walakini mkubwa sana. Ndio nilisema analysis yako umeiandika kimtazamo wa ki-CCM zaidi kuliko uhalisia wenyewe. Unataka kutuonyesha kwamba Prof. Ndullu amefanya kazi kubwa sana lakini hakuna kitu, bado tunacheza huko huko na hali inazidi kuwa mbaya zaidi kila kukicha.
 
Most likely MBA after a degree in Medicine .. meant for a medical doctor want to be a Manager in a Hospital. Hawa huwa hawana ufahamu wa namna ya kumanage uchumi ..

kuna vitu vingine huihitaji kusomea uchumi ndo uelewe
yaani kutoka aslimia 19.8 mpaka asilimia 19.4...hata form four mwenye akili
hawezi kuita 'mafanikio'....let alone mbunge mwenye MBA...

huyu jamaa ana raise maswali meengi kumhusu yeye kuliko anachozungumza
 
Mbaya zaidi bwana hamisi ana MBA..sijui kachukulia wapi???
Sasa namba tumpe homework.....akapitie tena desa...alafu kesho J3 asubuhi aje atuambia hizo 19% ni mafanikio kwa factors zipi...aiseeee...
Bunge la tz hilo.....na hawa ndio wabunge wetu.....

nasikia alidesa pale mzumbe remix university..
 
Ulichokiandika ni sawa na kumfanyia operation ya kichwa mgonjwa alovunjika mguu, unajua Hyper inflation inaanzia asilimia ngapi?kama 19% ni mafanikio unajua impact yake kwenye uchumi,ni kweli una elimu ya Biashara au una cheti cha Biashara?ukiwa mbunge usidhani kuwa ndo mtaalam wa kila kitu,peleka mawazo yako kwa wataalam wa fani husika wakushauri,ni bora umeandika kwa kibantu as ungetumia lugha za kigeni ingenibidi nifanye kazi ya ziada kusafisha hadhi ya Taifa letu as wabeba box wenzangu wangenihoji kama wewe ni mbunge asie mbunge anafananaje kiakili,leo nmekubali kama chama chetu kina vijana wa style yako,lusinde,nchemba na Nape basi taifa lipo mochwari!
 
2a-kgdx-us-6m-Large.gif
Mkuu Kingwalangwala nakupa swali moja rahisi only kama unajua kuzisoma indexes na kuzitafsiri.
Je, huwa unapitia major indexes at least twice a week?....
Kama hapana, kaa kimya!
Kama ndiyo, tunaona dollar inanyoshuka thamani tangu September mwaka jana, na dhahabu kupanda thamani. Ukilinganisha proportionality ya hizo commodities mbili kwenye soko la dunia versus proportionality ya kupanda kwa thamani ya shilingi, unaona ni haki shillingi ikawa 1580?
 
Benki Kuu ya Tanzania inapaswa kupongezwa kwa jitihada za mara moja walizofanya kushusha mfumuko wa bei nchini, na pia kupandisha thamani ya shilingi ya Kitanzania. Katika miezi mitatu iliyopita mfumuko wa bei za vyakula umeteremka kutoka 27.8% mpaka 26.7% na inflation kwa ujumla (general inflation rate) imeshuka kutoka 19.8% mpaka 19.4%. Pia thamani ya shilingi ya Kitanzania imepanda. Kiwango cha kubadilisha dola 1 ya kimarekani kwa shilingi ya kitanzania ilikuwa 1900, leo hii ni 1598. Hongera Gavana Benno Ndulu kwa kazi nzuri.​
Tumpigie makofi Mheshimiwa...kuna msemo wa "ashibae hamjui mwenye njaa"

Hongera Mheshimiwa Dr.Hamisi Kigwangalla, MD,MPH,MBA kwa kutuelewesha kuwa mfumuko bado ni karibu ya 20%. Mfumuko ulio kwenye tarakimu mbili ni wa kupongeza?

Unanikumbusha utani wa CCM na makada wake wa "uchumi wetu unapaa".

Mantiki hasa ya "utani wako" ni nini?

Unataka kutuaminisha kuwa unafuatilia kwa karibu upaaji/uimarikaji wa uchumi wa TZ?
Au kuwa Shilingi imeimarika kulinganisha na US dollar?

Au unatuambia kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa za kimaendeleo?

Wananchi unaowawakilisha katika jimbo lako wanasemaje kuhusu mfumuko wa bei za chakula kutoka 27.8% hadi 26.7%?
Ni kuwa sasa wanamudu kununua mahitaji yao? Au ni kuwa makali ya njaa zao yamepungua kutokana na juhudi za Gavana Ndulu za kuhakikisha "maisha bora kwa kila mtanzania"?

Kwa hiyo, kupungua kwa mfumuko kumesaidia posho za wabunge kuongezeka thamani?
Hongereni waheshimiwa...sisi huku mtaani tunasaga meno!
 
Nakubaliana na The Boss huyu jamaa anatia shaka elimu yake,ndio maana elimu yake tangia primary alifeli akafoji jina la Hamis nina wasiwasi elimu yako ni ya magumashi.
 
Binafsi sijui kama naelewa vizuri haya mambo ila walau nayafahamu yale yanayonichoma kama jua la saa sita mchana!!

Mwaka 2005, nilikuwa nanunua ndoo ya lita 10 ya mafuta ya kupikia kwa shilingi 8000-9500. Sasa hivi ni shilingi 30,000.00.
Na unga ulikuwa shilingi 250-300, sasa hivi ni 800-1000; wakati mchele umetoka shilingi 450-600 hadi >2200.

Na kuna mabenki wanasema kuwa sasa hivi hawatoi mikopo kwa sababu ya inflation.

Sasa BoT wamefanya nini ili tukubali kwamba ni wataalamu wa magics??
 
Mkuu Kigwangalla,

Ni lini exchange rate ya TShs/US$ ilifika shilingi 1900? Nimeangalia exchange rate ya kuanzia Januari 2009 mpaka juzi Ijumaa 22/3/2012, sikuona hiyo rate. Kwa kuhakikisha naomba angalia hapa: Bank of Tanzania: Financial Markets - Interbank Foreign Exchange Market (IFEM)

Data za IFEM ndio ambazo huwa zinatoa indicative exchange rate kwenye Bureaux de Change na mara nyingi ukiangalia selling rate ya BoT inaweza kukupa mwelekeo mzuri kwa kuongeza margin ya kama shilingi 100 kwenye selling rate.

Kwa hiyo credit yako ina walakini mkubwa sana. Ndio nilisema analysis yako umeiandika kimtazamo wa ki-CCM zaidi kuliko uhalisia wenyewe. Unataka kutuonyesha kwamba Prof. Ndullu amefanya kazi kubwa sana lakini hakuna kitu, bado tunacheza huko huko na hali inazidi kuwa mbaya zaidi kila kukicha.

kweli hata mimi huwa na deal sana na dollars, hakuna kipindi imewahi fika 1900/= hapo ni uongo, dollar ilikuwa inasimama 1500/= ikapanda ghafla hadi kufika kitu 1830/= lakini sio 1900/= , imeshuka hadi 1598/= lakini hawajafikia kwenye thamani yake ya awali toka ilpopanda ghafla!!
 
Kingwalangwala,

Samahani sana nakuomba usiingilie fani usiyoijua kiufupi hakuna la kuwapongeza BOT exchange rate ya currency wala si inflation ya nchi. Exchange rate ya Tanzania tunafahamu ilipanda kutokana na speculators waliokuwa wakitegemea nchi itashindwa kumudu kutoa sarafu za kigeni na kuongezeka mahitaji ya fedha za kigeni hasa mahitaji ya mafuta nchi sarafu yetu ingeliyumba. Kwahivyo maamuzi ya BOT yalikuwa ni kumwaga fedha za kigeni katika soko kupunguza kupanda sarafu ya kigeni hasa dollar. Vile vile waliongeza interest rate ilikupunguza fedha nyingi walizokuwa wameprint katika soko kipindi cha 2010-2011.

Dollar imeshuka thamani duniani kutokana na matatizo ya madeni ya ulaya na gharama za mafuta. Mfano £-$ imeshuka kutoka 1£-$1.9867 to 1£-$1.5545. Pia Euro imeshuka kithamani vyote kwa pamoja kutokana na mdodororo wa kiuchumi na madeni ya nchi za ulaya.

Tukiangalia kushuka kwa thamani ya dollar kutoka 1.988 against the british pound to 1.555 ni dalili tosha upo uwezekano wa kuimarika kwa thamani ya shillingi pia kwani shillingi iliimarika kutoka Tshs 1800 kwa dollar hadi 1580 dhidi ya dollar. Hivyo utaona hakuna uhusiano wowote na hatua za BOT ilizozichukua kudhibiti sarafu yetu. Kwanini nasema hivyo kwasababu kwa kiwango cha uwekezaji katika sekta ya madini na mafuta pamoja na gesi asilia nilitegemea sarafu ya Tanzania kuimarika zaidi ya hivi ilivyo. Badala yake BOT waliamua tu kubana na kuwauzia sarafu wanunuzi wa mafuta na waagizaji hatua ambayo kwangu mie ni kutapatapa. Vile vile BOT wameshindwa kudhibiti matumizi haramu ya fedha za kigeni nchi yanayochangia kukua kwa kiwango kikubwa kuporomoka kwa thamani ya sarafu yetu.

Tukija katika inflation tunajionea vichekesho kwani inflation nchi za wenzetu kama ulaya na marekani inashuka kwa asilimia 2 hadi 5 sisi inflation yetu imetoka kwenye single digit hadi kufikia asilimia 20. Sasa hivi imeshuka chini kwa asilimia 0.6 ndio tunaita mafanikia are you joking muheshimiwa mbunge????

Wiki iliyopita tumeshuhudia jinsi gavana wa benki kuu ya Uingereza akipongezwa kwa kushusha inflation kutoka 5.5% to 2.9% haya ndio mafanikio na sio kushusha inflation iliyokuwa single digit sasa iko double digit ya 20% na imeshuka kiduchu tu kwa asilimia 0.6% tunapongezana huu ni upuuzi muheshimiwa sana. Hali ya maisha mijini Tanzania imekuwa inatisha. Vyakula havinunuliki, nyumba hazipangiki, mshahara hauna thamani halafu tunapongezana nini??????

Mwe wacha fanyeni kazi kuwashinikiza hao BOT wapambane na factors halisi zinazochangia sarafu ya Tanzania iporomoke na inflation kuwa juu.
 
Gavana ameshusha ama amepandsha Inflation Rate?
Unafuu wa maisha mbona hauonekani na mbaya zaidi gharama zinazidi kupanda?
Halafu ni kwa nini Serikali imefumbia macho hii biashara ya ardhi na nyumba ambayo inanufaisha wachache bila Serikali kupata chochote?
Eti wako bize kukimbizana na wamachinga wakitegemea kuongeza pato la Serikali kwa kodi za wamachinga..

Halafu, mwanzisha mada wewe ndiye tunakutegemea usaidie kutengeneza sera nzuri leo hii unakuja kushabikia kitu ambacho hakipo?

MP my foot
Damn!!
 
nasikia alidesa pale mzumbe remix university..
Mzumbe chuo kizuri hakuna noma..sema yeye hakuzingatia masomo vema.....kama kasoma mzumbe MBA basi semister ya kwanza lazima alisoma masomo ya market Strategies na managerial economics ambayo kwa kiasi kikubwa asingeweza kuandika nondo kama alizotoa hapo juu....
 
Mh. Kigwangala,

Mtundiko wako hauna mashiko na sioni kama kuna any significant change kwenye inflation ambayo mtu anaweza kutoa credit kwamba inflation imeshuka.

BOT inahusika na kushusha mfumko wa bei kwa kuthibiti fedha iliyo kwenye mzunguko. Beyond hapo, hawana jeuri ya kushusha mfumko wa bei.

Tatizo kubwa kwa sasa ni mfumo mzima wa uzalishaji, sera mbovu zilizojaa matobo ya kuachia fedha za kigeni ziende nje ya nchi bila kutumika kuimarisha shilingi yetu na matumizi mabaya ya serikali ambayo hayana tija pamoja na ubadhilifu.

Je, wewe ukiwa kama Mbunge umefanya nini ili kuisimamia serikali iweze kuboresha mfumo mzima wa uzalishaji na usambazaji wa bidhaa ambazo bei zake ndio zinapelekea mfumko wa bei? TANESCO inayumba na hakuna anayeibana serikali huko Bungeni ili itimize ahadi za kumaliza tatizo la mgao wa umeme.

Kuimarika kwa shilingi ni changa la macho, maana inachofanya BoT ni kuuza hifadhi ya fedha za kigeni ambazo sio nyingi na ndio maana kumekuwa na volatility kubwa ya exchange rate kwa kuwa wanauza kwa machale maana hawana uhakika kama reserve waliyo nayo inaweza kuendelea kuishikilia shilingi hapo ilipo. Ili shilingi iweze kuimarika tunahitaji kuzalisha zaidi exports ambazo zote tumewapa wawekezaji ambao wamepewa incentive ya kuweka fedha za kigeni kwenye accounts zao za nje na hivyo mauzo yote ya maua, madini na hata utalii, fedha za kigeni huishia majuu na huku Bongo zinakuja za kulipa gharama za ndani [mishahara ya wafanyakazi na gharama nyingine ndogo ndogo] halafu hao hao wawekezaji wamepewa misamaha kibao ya kodi.

The only source ya foreign exchange ambayo imebaki hapa ni mauzo ya mazao ya kilimo ambako kumejaa utapeli wa vyama vya ushirika na ubadhilifu kibao kiasi kwamba JK aliahidi kulipa madeni yote ya vyama vya ushirika na ahadi hiyo mpaka leo haijatekelezwa.

Kipindi cha Mkapa (1995 - 2000) sekta ya Kilimo ilimsaidia sana kwa kuwa hali haikuwa mbaya sana. Kuanzia 2000 na kuendelea kilimo kilipewa kisogo na kukumbatia sekta ya madini (ambayo kwa maoni yangu kwa jinsi ilivyo hakuna kitu tunapata zaidi ya kuneemesha wawekezaji na kujaza takwimu tu kwamba Tanzania inauza sana madini halafu fedha za mauzo hatuzioni).

Nilitegemea wewe kama Mbunge ungekuja kuomba maoni kwamba ni njia gani zitumike ili kushusha mfumko wa bei? Nina hakika unajua, ila kwa sababu unaangalia swala hilo ki-CCM zaidi, unataka kutoa credit mahali ambapo hapastahili.
Bravo! Very constructive one!!!!!
 
Benki Kuu ya Tanzania inapaswa kupongezwa kwa jitihada za mara moja walizofanya kushusha mfumuko wa bei nchini, na pia kupandisha thamani ya shilingi ya Kitanzania. Katika miezi mitatu iliyopita mfumuko wa bei za vyakula umeteremka kutoka 27.8% mpaka 26.7% na inflation kwa ujumla (general inflation rate) imeshuka kutoka 19.8% mpaka 19.4%. Pia thamani ya shilingi ya Kitanzania imepanda. Kiwango cha kubadilisha dola 1 ya kimarekani kwa shilingi ya kitanzania ilikuwa 1900, leo hii ni 1598. Hongera Gavana Benno Ndulu kwa kazi nzuri. japokuwa nadhani huu ni mpango wa muda mfupi na tusiutegemee sana kama Taifa kuwa utadumu. Lengo likiwa kushusha mfumuko wa bei mpaka tarakimu moja kufikia June (ahadi ya BoT), kwa vyovyote vile inabidi muumize kichwa zaidi, na zaidi ya yote tuweke mipango ya muda mrefu ya kuimarisha uchumi wetu na hususani kupunguza imports. Je watafanikiwa, sijui, lakini ni matarajio na matamanio yetu kuwa watafika; tunawaombea dua. Wenzangu na mie wanashindwa kukuelewa ukiwapa hizi tarakimu, wao wanataka waone tu bei ya dagaa, maharage na sembe imeshuka maana wengi wao hata sukari haiwahusu sana. Je, tunaweza kukiri kuwa tumeshindwa kuzalisha misosi kiasi cha kutosha kushusha bei za chakula nchini? Ama tumeshindwa kutengeneza mfumo mzuri wa kusambaza chakula nchini kiasi kwamba watu wa nyanda za juu kusini wanakosa pa kuweka chakula ilhali Nzega wanakufa na njaa?

kweli wewe ni ****

hujasema benchmark ilikua nini unakuja kuleta siasa za kipuuzi namna hii??? what was the projection ya inflation 3 years ago na je tuko kwenye like au nje ya like??

Mijitu kama hii inasababisha siasa idharaulike kabisa... nilitegemea mtu atakuja na critical analysis with timelines, benchmarks, causes na approaches za kusaidia, yeye kaja na vijineno viwili alivyo-quote sehemu

sasa hiyo inflation ilikua ngapi wakati dullu anaingia?? leo iko wapi??? unasifi mtoto aliyefeli kwa kupata swali la tatu la section A... PREVENTION WOOULD MAKE SENSE BTW

GROW UP AISEE
 
Kingwalangwala,

Samahani sana nakuomba usiingilie fani usiyoijua kiufupi hakuna la kuwapongeza BOT exchange rate ya currency wala si inflation ya nchi. Exchange rate ya Tanzania tunafahamu ilipanda kutokana na speculators waliokuwa wakitegemea nchi itashindwa kumudu kutoa sarafu za kigeni na kuongezeka mahitaji ya fedha za kigeni hasa mahitaji ya mafuta nchi sarafu yetu ingeliyumba. Kwahivyo maamuzi ya BOT yalikuwa ni kumwaga fedha za kigeni katika soko kupunguza kupanda sarafu ya kigeni hasa dollar. Vile vile waliongeza interest rate ilikupunguza fedha nyingi walizokuwa wameprint katika soko kipindi cha 2010-2011.

Dollar imeshuka thamani duniani kutokana na matatizo ya madeni ya ulaya na gharama za mafuta. Mfano £-$ imeshuka kutoka 1£-$1.9867 to 1£-$1.5545. Pia Euro imeshuka kithamani vyote kwa pamoja kutokana na mdodororo wa kiuchumi na madeni ya nchi za ulaya.

Tukiangalia kushuka kwa thamani ya dollar kutoka 1.988 against the british pound to 1.555 ni dalili tosha upo uwezekano wa kuimarika kwa thamani ya shillingi pia kwani shillingi iliimarika kutoka Tshs 1800 kwa dollar hadi 1580 dhidi ya dollar. Hivyo utaona hakuna uhusiano wowote na hatua za BOT ilizozichukua kudhibiti sarafu yetu. Kwanini nasema hivyo kwasababu kwa kiwango cha uwekezaji katika sekta ya madini na mafuta pamoja na gesi asilia nilitegemea sarafu ya Tanzania kuimarika zaidi ya hivi ilivyo. Badala yake BOT waliamua tu kubana na kuwauzia sarafu wanunuzi wa mafuta na waagizaji hatua ambayo kwangu mie ni kutapatapa. Vile vile BOT wameshindwa kudhibiti matumizi haramu ya fedha za kigeni nchi yanayochangia kukua kwa kiwango kikubwa kuporomoka kwa thamani ya sarafu yetu.

Tukija katika inflation tunajionea vichekesho kwani inflation nchi za wenzetu kama ulaya na marekani inashuka kwa asilimia 2 hadi 5 sisi inflation yetu imetoka kwenye single digit hadi kufikia asilimia 20. Sasa hivi imeshuka chini kwa asilimia 0.6 ndio tunaita mafanikia are you joking muheshimiwa mbunge????

Wiki iliyopita tumeshuhudia jinsi gavana wa benki kuu ya Uingereza akipongezwa kwa kushusha inflation kutoka 5.5% to 2.9% haya ndio mafanikio na sio kushusha inflation iliyokuwa single digit sasa iko double digit ya 20% na imeshuka kiduchu tu kwa asilimia 0.6% tunapongezana huu ni upuuzi muheshimiwa sana. Hali ya maisha mijini Tanzania imekuwa inatisha. Vyakula havinunuliki, nyumba hazipangiki, mshahara hauna thamani halafu tunapongezana nini??????

Mwe wacha fanyeni kazi kuwashinikiza hao BOT wapambane na factors halisi zinazochangia sarafu ya Tanzania iporomoke na inflation kuwa juu.

TATIZO NI SIASA IMEWAFANYA WABUNGE KUDHANI WANAJUA KILA KITU............ THIS DUDE IS THE JACK OF ALL TRADES, which translate to msema ovyo
 
In any case inflation rate ya double digits ni mzigo mkubwa mno kwa Mtanzania mmoja mmoja. Hali ni mbaya majumbani, watu wamepunguza idadi ya milo kwa siku toka milo 2 au 3 hadi mlo 1 tena usioeleweka. Ni kama tumerudi enzi za 'kufunga mikanda'
 
Tatizo watu wengi ni wavivu wa kusoma, sina shaka hamkufika mwisho mwa post yangu...maana comments zinazotoka ni tofauti kabisa na mtazamo nilioutoa kwenye post yangu. Anyways kalagabaho

Pia kale kautaratibu kakumuattack mtu aliyeandika hoja badala ya hoja yenyewe kanaonesha utoto na uwezo mdogo wa kujadili mambo...

Sikusomea MBA yangu Mzumbe, nimesoma nje na nimesoma program intense na yenye uwezo mkubwa wa kuniandaa kuwa analyst mzuri kuliko wengi mnavyofikiria. SIkujiandaa kuwa Meneja hospitalini wala popote, nilisoma ili kuwa meneja wangu mwenyewe...mind you 'I am an entrepreneur!'

Ukiongelea elimu, hapa sahau tu boss, maana ninauwezo wa kusoma kitu chochote na ku-excel FYI sasa hivi nipo kwenye mchakato wa ku-rejista Ph.D ya Uchumi, sijui na hapo utasemaje
 
Changanua mambo kama msomi tafadhali, wasiliana na wataalamu kabla ya ku post kitu kama hiki kuongeza uelewa wako
 
..............
Ama tumeshindwa kutengeneza mfumo mzuri wa kusambaza chakula nchini kiasi kwamba watu wa nyanda za juu kusini wanakosa pa kuweka chakula ilhali Nzega wanakufa na njaa?

Ktika hali ambayo serikali ya kupitia wizara ya miunobinu Iko katika kufanya "maigizo" ya kuanzisha na kujenga Internenatinala Airport huku ikiachamashirikakama TAZARA yakiwa hoi unategemea nini kwenye usafirishaji wamazo

Hivi viwanja vya ndege
  • ni kwa matumizi ya wanachi gani? na
  • ton ngapi za hayo mazao na mzigo zitasafirishwa kwa anga ?

Tatizo mpaka sasa hatuna vipaumbele sahihi.Kama vipo ni vya kisiasa tu. Kwa issue ya mazao RELI ilitakiwakuwa mhimili then barabara zinazajazia
 
Back
Top Bottom