Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,802
- 11,961
Benki kuu ya Tanzania imeiadhibu NBC kiasi cha Tsh Bilioni moja kwa kosa la kudanganya kwamba inacho kituo kikubwa cha taarifa nchini. Baada ya ukaguzi kufanyika ilionekana NBC haina kituo kikubwa wala kidogo cha taarifa hapa nchini(Primary/Secondary data centre).
Hapo awali tarehe 23 Aug 2019, Benki Kuu ilizipa siku saba Benki na Taasisi za kifedha kuthibitisha kama zina kituo kikuu au kidogo cha taarifa nchini na taasisi itakayoshindwa kufanya hivyo itatozwa faini Tsh. Bilioni 5.
Aidha Benki kuu ilitoa miezi 3 kwa taasisi hizo kufungua vituo vikuu vya taarifa nchini na kwa watakaoshindwa kufanya hivyo ndani ya muda uliotolewa watatozwa Tsh. Milioni 500 kila mwezi hadi watakapo kamilisha vituo hivyo.
Zaidi, soma;

Benki Kuu: Benki au Taasisi ya fedha isiyo na kituo cha taarifa Nchini, kupigwa faini ya Bil 5/=
BENKI/TAASISI ZA FEDHA ZISIZO NA VITUO VYA TAARIFA NCHINI KUPIGWA FAINI Benki Kuu imezipa Benki na Taasisi za kifedha siku 7 kuthibitisha kama zina kituo kikuu au kidogo cha taarifa nchini na taasisi itakayoshindwa kufanya hivyo itatozwa faini Tsh. Bilioni 5 Aidha Benki kuu imetoa miezi 3 kwa...
www.jamiiforums.com